Jinsi ya kutambua Tangazo la kazi la kitapeli

moyafricatz

JF-Expert Member
Nov 27, 2015
2,900
4,865
Wakuu mmeamkaje?

Nimeona tahadhari nyingi zikitolewa humu kuwaasa watu Wasiingie kwenye mitego ya matapeli wa ajira lakini hatuwaoneshi waombaji wa kazi kwa vitendo kuhusu mbinu au documents zenye mfanano na documents au matangazo (Genuine)halisi ya kazi .

Ntakua nina series hapa za kuleta matangazo feki ya kazi ambayo yanazunguka kwenye magroup ya kutafuta kazi niliyopo.

Kwenye moja ya group nililopo kuna mtu kapost hili tangazo na akiamini kabisa hili ni tangazo legit so kwa niaba ya wote naomba twende pamoja ndugu zangu tuelimishane namna ya kujua tangazo la kitapeli.

Inawezekana nisitaje elements zote kadri navyo observe lakini wasomaji pia mtakua mnaongezea vitu ambayo mme-observe kwenye hii document.

Document iko chini hapo nime upload.

Observation ya kwanza:
Tangazo hili ni feki sababu ya kwanza ni Nembo za wahusika (Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii), kama ujuavyo matangazo mengi ya serikali huwa yana NEMBO YA TAIFA yaani bibi na bwana pale katikati ya document.

Hili ni feki sababu lina nembo mbili, ya WHO kushoto na nembo ya taifa kulia hata kama wamefanya partnership ya hizi taasisi mbili lakini mtangazaji wa tangazo ndo ana haki ya kuweka nembo yake pale juu.

Na serikali huwa kwenye matangazo yao wanaweka nembo ya bibi na bwana pale kati cheki matangazo yote .

Observation Ya Pili:
Font size iliyotumika (Yaani ukubwa au udogo wa maandishi uliotumika pamoja na staili ya kukoleza maandishi kwenye tangazo )

Kichwa cha tangazo yaani JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, Wizara ya afya na maendeleo ya jamii ,jinsia na Watoto ....." haya maneno yana font size tofauti na wanazotumia serikali na hata upangaliaji wake ni wa tofauti sasa hawa matapeli inabidi wawe makini kwenye kuiga, wasidhani watu wote ni vilaza.

Pia utakuta kwenye tangazo wame bold (koleza kwa wino mweusi) baadhi ya maneno mfano Kwenye sentensi "Wizara ya afya chini ya shirika la afya Duniani WHO" unaona neno "wizara ya afya limekozwa ili kukufanya au kukuaminisha ni tangazo la serikali au la wizara husika wakati ni feki.

Observation ya TATU:
Ukosefu wa ujuzi wa uandishi wa Lugha ya kiswahili kwenye tangazo.

Kifupi tapeli aliyeandika hili tangazo ni mtu wa form 2 au darasa la saba sababu ana matatizo ya grammar au muundo wa sentensi mfano anatumia maneno ya kiswahili lakini bado anayakosea ,twende pamoja mfano neno "TANGAZO LA AJIRA ZA MDA-2022" neno MDA limetumika badala ya neno "MUDA".

Neno "Gonjwa la mlipuko" badala ya "Ugonjwa wa mlipuko"

Sentensi "kwa mikoa yote ILIOPO Tanzania bara na visiwani " usahihi ilitakiwa Iwe ,kwa mikoa yote ILIYOPO.

Pia pale kwenye sifa za muombaji , amendika "Awe na Umrini kuanzia mika (18-30).Unaona kabisa huyu tapeli ni low thinker and writer usahihi maneno "Umrini" na "mika" yamekosewa kisarufi...kudhulumu watu sio kazi rahisi jamani .

Pia sentensi "Awe na afya ilio bora",neno ilio limekosewa.

Pia pale sehemu B ,neno viambatanishi vinavyohitajika ..unaona kabisa neno "VINAVYO HITAJIKA" limeandikwa kama maneno mawili kumbe ni neno moja .

Pia "vyeti vya Taama" badala ya "vyeti vya Taaluma"

Pia kwa kumalizia tapeli anasema andika barua kwa katibu mkuu na akatoa anwani lakini hakuna anwani pale zaidi ya usanii...

Angalia anasema andika kwa
KATIBU MKUU
WIZARA YA AFYA KITENGO MAALUMU
DODOMA -TANZANIA

Na wakati ukiweka anwani basi weka na namba za sanduku la posta .

Mfano tu naandika mimi hapa .

KATIBU MKUU
WIZARA YA AFYA,MAENDELEO YA JAMII ,JINSIA NA WATOTO,
KITENGO MAALUMU
SLP 3333333333
DODOMA
TANZANIA.

Kutoweka kwake anwani ya namba pamoja n upangiliaji sahihi wa anwani inaonesha nafsi yake ikimsuta kutapeli vijana wenye kiu ya kutafuta maisha.

Pia neno "waombaji wetu watakao fuzu, badala ya neno "watakaofuzu",

Pia neno "mda" kama tulivyoona mwanzo limerudiwa badala ya neno " muda".

Observation 4:
Utumiaji wa barua pepe feki kwenye tangazo.

Ndugu zangu hii ni element moja muhimu sana kwenye kujua tangazo kama ni legit au feki.

Taasisi binafsi pamoja na serikali huwa wanatumia email (barua pepe) zenye domains zao mfano shirika la ndege la precision wanatumia domain yao (precisionairtz.com) hivyo email zao zitakua hurumajohn@precisionairtz.com na kadhalika.

Au tamisemi zile za tamisemi.go.tz watakua na domain zao mfano jumah@tamisemi.go.tz

Hivyo basi tunategemea kwa tangazo lofoten halisi la kazi liwe na barua pepe halisi za kampuni husika na taasisi au makampuni yasiyo na hizi domain zao wanashauriwa wawe nazo ili tangazo au matangazo yao yawe na legitimacy mbele ya jamii.

Kampuni, taasisi ,asasi ziwe za kiraia au ki serikali hazitakiwi kutumia barua pepe zenye domain za kiraia...mfano Gmail, yahoo, Hotmail, AOL na kadhalika .

Sasa tunategemea Wizara ya afya iwe na domain yao ya waombaji kupeleka mambo hayo ya kazi za muda.

Twende pamoja hapa kuchambua mtego mkubwa ambao tapeli huyu ameutega na naamini baadhi ya waombaji watakua wameingia mkenge lakini sio wote.

Tapeli huyu amendika na namnukuu "Maombi yote yatumwe kwenye barua pepe maalumu

Special recruitment.afya.go.tz gmail.com

Mpuuzi sana huyu,anajua kabisa waombaji wanajua domain za serikali kwa hiyo pale kwenye email ule upande wa kwanza kaadindika domain ya serikali Special recruitment.afya.(go.tz) hiyo (go.tz) inatosha kumuanisha muombaji na akasema niliona domain ya serikali lakini SI KWELI...

Mtego uliopo hapo ni kwamba domain ya hiyo barua pepe ama email ni bado feki kwa wizara ya afya....domain hapo ni "GMAIL.COM"

Jamani domain ni ile inafata badala ya jina la muhusika kwenye email na nikatoa mfano hapo juu " jumah@tamisemi.go.tz" domain ni baada ya hiyo alama @ so kwa email address ya jumah domain yake ni tamisemi.go.tz maana yake anafanyia kazi tamisemi.

Nikatoa pia mfano hurumajohn@precisionairtz.com huyu kaka hurumajohn anafanyia kazi precision air....nasisitiza domain ni badala ya alama @

Sasa tukirudi kwenye mtego wa tapeli kaandika afya.go.tz ili akuchote alafu kamalizia na domain yake gmail.com .

KWa barua pepe hiyo ya Special recruitment.afya.go.tz gmail.com basi maombi yote ya kazi mtakayotuma yatakua yanaingia kwenye email yake na mtaombwa hela huko,atakuchota huko maana ataona he or she is smarter than you maana amekuchota kwenye mtego wake wa kwanza so mtego wa pili ni huko kwenye email na wa tatu ,wanne atauleta kwako na eventually ATAKUTAPELI na utakuja kulalamika hapa JamiiForums.

Kuna watu wengine wanashea haya matangazo wakiwa HAWAJUI kama ni ya kitapeli.

Wanashare in good faith.. lakini kama unajua ni la kitapeli achana nalo usishee na wenzako maana Wengi watalizwa.

Tapeli amecheza vizuri na rangi za nembo ya WHO pamoja na Nembo ya wizara ya Afya

Rangi zinavutia na kuaminisha kwamba Tangazo liko okay sio la kitapeli...WASHINDWEEEE.

Nimejitolea muda na ujuzi kwenye kutoa elimu ya namna ya kugundua matangazo ya kitapeli na nawashukuru Jamiiforum kwa kutupa jukwaa kama hili la kuwafikia wengi.

Tutakua na series ya uchambuzi wa matangazo feki ya kazi (Fraud adverts) so niwaombe kama kuna tangazo unakutana nalo ni feki au unahisi ni feki basi lilete kwangu kupitia PM yangu au email yangu felixharrymoya@gmail.com ili nililete hapa tulichambue kwa pamoja na iwe faida kwa wengine waweze faidika na wawe msaada kwa wengine.

Inauma sana napoona kijana mtafutaji kazi anadhulumiwa kiasi kidogo alichopata kwa shida ili ku facilitate applications feki.

MATAPELI SASA BAAAAS
JIUNGE NAMI KWENYE KAMPENI HII YA KUTOKOMEZA MATEPELI WA AJIRA KWA VIJANA.

Till next bandiko.

IMG-20210209-WA0015.jpg
 
Ahsante sana mkuu kwa kutufumbua macho.

Pia tunaweza kuwabaini kwa kutuma nyaraka zozote kupitia email yao
Nakunuu "pia tunaweza kuwabaini kwa kutuma nyaraka zozote kupitia email yao???

Nyaraka zozote unamanisha nyaraka zipi????
 
Mkuu,hayo makosa unayosema ni makosa ni sehemu ya mkakati wao wa kuhakikisha kwamba only fools and despearte people ndo wanaomba na wala sio kwamba ni uzembe au ujinga.Wanajua kwamba wakiweka tangazo lika proffessional sana serious people wataomba na chances are hawataweza kuwaibia so the best they can do is screen the smart ones out through those not so stupid errors.
 
Exactly ndo mana nikasema pale juu "hao fools na desperate wakishaomba".

Unakua umeshajipambanua kwao kwamba wewe ni kilaza hence wanaanza kwenda na ww kwenye stage ya pili ,ya tatu na Ya nne ya utapeli.

So uko sahihi kabisa mkuu...only fools na desperate wataomba.
 
Hata mtoto wa la saba wa mwaka jana aliyefeli anagundua hilo tangazo limeandikwa na mtu mpumbavu wa cheo cha chini katika ulimwengu wa wapumbavu
 
Wakuu mmeamkaje?

Nimeona tahadhari nyingi zikitolewa humu kuwaasa watu Wasiingie kwenye mitego ya matapeli wa ajira lakini hatuwaoneshi waombaji wa kazi kwa vitendo kuhusu mbinu au documents zenye mfanano na documents au matangazo (Genuine)halisi ya kazi .

Ntakua nina series hapa za kuleta matangazo feki ya kazi ambayo yanazunguka kwenye magroup ya kutafuta kazi niliyopo.

Kwenye moja ya group nililopo kuna mtu kapost hili tangazo na akiamini kabisa hili ni tangazo legit so kwa niaba ya wote naomba twende pamoja ndugu zangu tuelimishane namna ya kujua tangazo la kitapeli.

Inawezekana nisitaje elements zote kadri navyo observe lakini wasomaji pia mtakua mnaongezea vitu ambayo mme-observe kwenye hii document.

Document iko chini hapo nime upload.

Observation ya kwanza:
Tangazo hili ni feki sababu ya kwanza ni Nembo za wahusika (Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii), kama ujuavyo matangazo mengi ya serikali huwa yana NEMBO YA TAIFA yaani bibi na bwana pale katikati ya document.

Hili ni feki sababu lina nembo mbili, ya WHO kushoto na nembo ya taifa kulia hata kama wamefanya partnership ya hizi taasisi mbili lakini mtangazaji wa tangazo ndo ana haki ya kuweka nembo yake pale juu.

Na serikali huwa kwenye matangazo yao wanaweka nembo ya bibi na bwana pale kati cheki matangazo yote .

Observation Ya Pili:
Font size iliyotumika (Yaani ukubwa au udogo wa maandishi uliotumika pamoja na staili ya kukoleza maandishi kwenye tangazo )

Kichwa cha tangazo yaani JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, Wizara ya afya na maendeleo ya jamii ,jinsia na Watoto ....." haya maneno yana font size tofauti na wanazotumia serikali na hata upangaliaji wake ni wa tofauti sasa hawa matapeli inabidi wawe makini kwenye kuiga, wasidhani watu wote ni vilaza.

Pia utakuta kwenye tangazo wame bold (koleza kwa wino mweusi) baadhi ya maneno mfano Kwenye sentensi "Wizara ya afya chini ya shirika la afya Duniani WHO" unaona neno "wizara ya afya limekozwa ili kukufanya au kukuaminisha ni tangazo la serikali au la wizara husika wakati ni feki.

Observation ya TATU:
Ukosefu wa ujuzi wa uandishi wa Lugha ya kiswahili kwenye tangazo.

Kifupi tapeli aliyeandika hili tangazo ni mtu wa form 2 au darasa la saba sababu ana matatizo ya grammar au muundo wa sentensi mfano anatumia maneno ya kiswahili lakini bado anayakosea ,twende pamoja mfano neno "TANGAZO LA AJIRA ZA MDA-2022" neno MDA limetumika badala ya neno "MUDA".

Neno "Gonjwa la mlipuko" badala ya "Ugonjwa wa mlipuko"

Sentensi "kwa mikoa yote ILIOPO Tanzania bara na visiwani " usahihi ilitakiwa Iwe ,kwa mikoa yote ILIYOPO.

Pia pale kwenye sifa za muombaji , amendika "Awe na Umrini kuanzia mika (18-30).Unaona kabisa huyu tapeli ni low thinker and writer usahihi maneno "Umrini" na "mika" yamekosewa kisarufi...kudhulumu watu sio kazi rahisi jamani .

Pia sentensi "Awe na afya ilio bora",neno ilio limekosewa.

Pia pale sehemu B ,neno viambatanishi vinavyohitajika ..unaona kabisa neno "VINAVYO HITAJIKA" limeandikwa kama maneno mawili kumbe ni neno moja .

Pia "vyeti vya Taama" badala ya "vyeti vya Taaluma"

Pia kwa kumalizia tapeli anasema andika barua kwa katibu mkuu na akatoa anwani lakini hakuna anwani pale zaidi ya usanii...

Angalia anasema andika kwa
KATIBU MKUU
WIZARA YA AFYA KITENGO MAALUMU
DODOMA -TANZANIA

Na wakati ukiweka anwani basi weka na namba za sanduku la posta .

Mfano tu naandika mimi hapa .

KATIBU MKUU
WIZARA YA AFYA,MAENDELEO YA JAMII ,JINSIA NA WATOTO,
KITENGO MAALUMU
SLP 3333333333
DODOMA
TANZANIA.

Kutoweka kwake anwani ya namba pamoja n upangiliaji sahihi wa anwani inaonesha nafsi yake ikimsuta kutapeli vijana wenye kiu ya kutafuta maisha.

Pia neno "waombaji wetu watakao fuzu, badala ya neno "watakaofuzu",

Pia neno "mda" kama tulivyoona mwanzo limerudiwa badala ya neno " muda".

Observation 4:
Utumiaji wa barua pepe feki kwenye tangazo.

Ndugu zangu hii ni element moja muhimu sana kwenye kujua tangazo kama ni legit au feki.

Taasisi binafsi pamoja na serikali huwa wanatumia email (barua pepe) zenye domains zao mfano shirika la ndege la precision wanatumia domain yao (precisionairtz.com) hivyo email zao zitakua hurumajohn@precisionairtz.com na kadhalika.

Au tamisemi zile za tamisemi.go.tz watakua na domain zao mfano jumah@tamisemi.go.tz

Hivyo basi tunategemea kwa tangazo lofoten halisi la kazi liwe na barua pepe halisi za kampuni husika na taasisi au makampuni yasiyo na hizi domain zao wanashauriwa wawe nazo ili tangazo au matangazo yao yawe na legitimacy mbele ya jamii.

Kampuni, taasisi ,asasi ziwe za kiraia au ki serikali hazitakiwi kutumia barua pepe zenye domain za kiraia...mfano Gmail, yahoo, Hotmail, AOL na kadhalika .

Sasa tunategemea Wizara ya afya iwe na domain yao ya waombaji kupeleka mambo hayo ya kazi za muda.

Twende pamoja hapa kuchambua mtego mkubwa ambao tapeli huyu ameutega na naamini baadhi ya waombaji watakua wameingia mkenge lakini sio wote.

Tapeli huyu amendika na namnukuu "Maombi yote yatumwe kwenye barua pepe maalumu

Special recruitment.afya.go.tz gmail.com

Mpuuzi sana huyu,anajua kabisa waombaji wanajua domain za serikali kwa hiyo pale kwenye email ule upande wa kwanza kaadindika domain ya serikali Special recruitment.afya.(go.tz) hiyo (go.tz) inatosha kumuanisha muombaji na akasema niliona domain ya serikali lakini SI KWELI...

Mtego uliopo hapo ni kwamba domain ya hiyo barua pepe ama email ni bado feki kwa wizara ya afya....domain hapo ni "GMAIL.COM"

Jamani domain ni ile inafata badala ya jina la muhusika kwenye email na nikatoa mfano hapo juu " jumah@tamisemi.go.tz" domain ni baada ya hiyo alama @ so kwa email address ya jumah domain yake ni tamisemi.go.tz maana yake anafanyia kazi tamisemi.

Nikatoa pia mfano hurumajohn@precisionairtz.com huyu kaka hurumajohn anafanyia kazi precision air....nasisitiza domain ni badala ya alama @

Sasa tukirudi kwenye mtego wa tapeli kaandika afya.go.tz ili akuchote alafu kamalizia na domain yake gmail.com .

KWa barua pepe hiyo ya Special recruitment.afya.go.tz gmail.com basi maombi yote ya kazi mtakayotuma yatakua yanaingia kwenye email yake na mtaombwa hela huko,atakuchota huko maana ataona he or she is smarter than you maana amekuchota kwenye mtego wake wa kwanza so mtego wa pili ni huko kwenye email na wa tatu ,wanne atauleta kwako na eventually ATAKUTAPELI na utakuja kulalamika hapa JamiiForums.

Kuna watu wengine wanashea haya matangazo wakiwa HAWAJUI kama ni ya kitapeli.

Wanashare in good faith.. lakini kama unajua ni la kitapeli achana nalo usishee na wenzako maana Wengi watalizwa.

Tapeli amecheza vizuri na rangi za nembo ya WHO pamoja na Nembo ya wizara ya Afya

Rangi zinavutia na kuaminisha kwamba Tangazo liko okay sio la kitapeli...WASHINDWEEEE.

Nimejitolea muda na ujuzi kwenye kutoa elimu ya namna ya kugundua matangazo ya kitapeli na nawashukuru Jamiiforum kwa kutupa jukwaa kama hili la kuwafikia wengi.

Tutakua na series ya uchambuzi wa matangazo feki ya kazi (Fraud adverts) so niwaombe kama kuna tangazo unakutana nalo ni feki au unahisi ni feki basi lilete kwangu kupitia PM yangu au email yangu felixharrymoya@gmail.com ili nililete hapa tulichambue kwa pamoja na iwe faida kwa wengine waweze faidika na wawe msaada kwa wengine.

Inauma sana napoona kijana mtafutaji kazi anadhulumiwa kiasi kidogo alichopata kwa shida ili ku facilitate applications feki.

MATAPELI SASA BAAAAS
JIUNGE NAMI KWENYE KAMPENI HII YA KUTOKOMEZA MATEPELI WA AJIRA KWA VIJANA.

Till next bandiko.

View attachment 1698898
Njia rahisi ya kugundua tangazo la kazi feki ni pale tu unapoambiwa TUMA NA YA KUTOLEA
 
mkuu siku hao jamaa mpaka wanatengeneza tovuti ya kampuni kabisa niliona moja sbc ya pepsi hilo tangazo walilipia kabisa facebook wakapromote....bila shaka kuna watu wanapigwa ndio maana wanaendelea
 
Duuh
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom