Jinsi ya kutambua MATAPELI wanaotangaza AJIRA.

Aug 17, 2016
73
39
Kumekuwa na wingu kubwa la matapeli ambao wamekuwa wakijifanya kuwa wao ni waajiri ama ni recruitment agency lakini lengo lao ni kutapeli wanaotafuta ajira. Wengi wao hutumia nafasi walizo nazo kujiongezea kipato. Ni wengi wamekumbwa na janga hili.

Zifuatazo ni namna mbali mbali zitakazokuwezesha kutambua matapeli hao wa ajira.

1. Pesa mbele, wacha mchezo na pesa, uonapo mwajiri huyo anakudai fedha eti ni ya fomu ya kiingilio, ama gharama za usaili, au gharama za mafunzo. Hakuna wakala wa ajira wa kihalali ambaye atakuchaji gharama za usaili. Hii ni kinyume na sheria ya kazi ya Tanzania. Hivyo uonapo dalili kama hii KIMBIA UPESI EPUKA UTAPELI.

2. Fanya utafiti juu ya kampuni hiyo. Ingia kwenye tovuti (website) yao kisha tafuta mawasiliano yao. Fananisha barua pepe uliyotumiwa taarifa na iliyopo kwenye website. Iwapo kampuni haina tovuti (website) kuwa makini. Recruitment agency zilizohalali zina tovuti iliyo na taarifa zao zote.

3.Barua pepe; Ukiona hiyo recruitment agency inatumia hizi barua pepe za bure mfano Gmail,Hotmail, Yahoo and Live ujue hapo kuna walakini. Recruitment agencies zilizo halali hutumia corporate email adresses. Yaani mfano careers@jina la kampuni.com au jobs@jina la kampuni.co.org pia jina la mtu@jina la kampuni.com

4. Hebu chunguza jina la kampuni mtandaoni, jaribu kuangalia kama utapata taarifa zozote kuhusu hiyo kampuni.

5.Kupokea taarifa umepatiwa kazi ilihali wewe hujawahi kuomba kazi popote, na wala hawana CV yako. Huo ni nusu ya muujiza. Ila Mbaya zaidi ni pale watakapokwambia lipia kiasi fulani ili ukaanze kazi . KIMBIA UPESI.

6.Kufanyia kazi ukiwa nyumbani, wengine watakwambia hakuna haja ya kwenda ofisini utakuwa ukifanyia kazi nyumbani. Hii inawezekana hata kwa kampuni halali ipo, lakini pale ambapo utaambiwa huna haja ya kutafuta ofisi ilipo kwani utafanyia nyumbani hata interview itakuwa mbali na ofisi halafu kisha utalipia.

7.Maelezo ya utendaji kazi (Job description) unakuta JD unaisoma hadi mwisho lakini huelewi ni kazi ya namna gani au inaelezea nini.

HEBU ONGEZEA NAMNA NYINGINE YA KUTAMBUA WAAJIRI FEKI. TUJIFUNZE WOTE TUWE MAKINI.
 
Hiyo namba 3,nikikuta email za design hiyo wala sihangaiki unless kama hiyo organization naifahamu maana zingine huwa ni local organization hivyo issue za email address wanatumia za kawaida
 
boss nkushukuru kwa hii thread ..nmeingia kwe website yenu mpo vizuri nmeregister kwa diploma nadhani itanisaidia kwe hii current role yangu.nataka nipate some hints naja pm mkubwa
 
Serikali za mitaa na vitongoji zihusike pia. Mwezi uliopita vijana wa Kigoma, Kasulu na Kibondo waliingizwa mkenge wakalipa sijui ada gani na siku ya interview wakaambiwa wajipange kwenye vituo vya magari basi litawafuata ulipofika muda wa kuwachukua 'namba ya mteja unayempigia haipatikani'. Tangazo la hizo ajira zilikuwa kwenye nguzo kwa muda mrefu tu lakini hakuna aliyeshtukia utapeli huu. Serikali ifanye kazi ya ulinzi na usalama wa raia na mali zake tafadhali.
 
nyie pia walewale. Shituka kijana
Huna haja ya kudhania tuu, tafadhali tafuta taarifa zaidi kabla husaema lolote. Tembelea tovuti yetu kwa maelezo zaidi. Waweza pia kufika katika ofisi zetu ili kuweza kutufahamu vzuri. Pengine itakusaidia kuondoa mashaka.
 
Back
Top Bottom