Jinsi ya kutafuta kazi sehemu ya kwanza

Jul 1, 2018
8
14
Wakuu salam ! Naomba nitumie fursa hii kuandika machache kadili ninavyofahamu kuhusu namna ya kupata kazi hasa kwenye fair competition. Najua kutafuta kazi inaweza kuwa kati ya vitu vigumu sana kwa sasa hasa ukizingatia uchache Wa kazi zenyewe. Kitu kilichonifanya nisukumwe kufanya hivi ni kwa kuwa nimetambua watu wengi ambao ni watafuta kazi wanashida ya kutokujua baadhi ya mambo na nikawaza kuna vitu wanavihitaji kujua zaidi kuliko hata kupata kazi kwenyewe. Nitaanza kuelezea mambo mbalimbali pasipo mpangilio maalumu katika sehemu ya kwanza mpaka ya tano wewe mwenyewe utachagua kivi kinakufaa. Mambo ya msingi kabla ya kuomba kazi.

1. Andaa dokumenti zako kwa usahihi. Hapa namaanisha weka makabrasha yako kwa uzuri kama ni kuandaa wasifu wako, vyeti na kadhalika yaani uwe navyo hard copy na soft copy hii itakusaidia kuwa very quick katika kufanya maombi pale unavyotaka kufanya hivyo hata hivyo kwenye upande Wa wasifu hakikisha umeandaa vizuri tena vizuri hasa na jaribu kushare wasifu wako na watu kadhaa wakupe ushauri namna nzuri ya kuandaa wasifu wako (Waajiri wengi wanalalama watu wana wasifu za hovyo sana ) wasifu Wa hovyo maana yake umeandaliwa hovyo hovyo hata kama yaliyomo ni mazuri pia lazima ujue there is no such a thing as perfect resume but it is entirely contingent upon the position you are applying for , kusema hivyo wasifu ulioupeleka kwa kazi A unaweza usiwe sahihi kwa kazi B hence inatakiwa uwe unahariri Mara kwa Mara watu wengi wanatumia wasifu huo huo kwa maelfu ya maombi my friend hakuna bahati kwenye kupata kazi hasa kwenye equal opportunity organizations.

1. Tafuta Taarifa za kazi zinakopatikana .
Mara zote njia inayofanya kazi zaidi kwenye kutafuta kazi ni kufanya maombi, na huwezi kufanya maombi pasipo kuwa na taarifa. Mara nyingi kwa sasa mtandao umekuwa ni sehemu nzuri kwa watu kupata taarifa hizo za kazi sasa basi jua tovuti nyingi huwezavyo ambazo zinataarifa za kazi . Baadhi kama zoom, brighter Monday , cv people , LinkedIn na nyingine nyingi sina haja ya kuelezea sana . Pia kama nilivyosema awali mitandao umekuwa sehemu nzuri sana kupata taarifa na wakati mwingine hata mitandao ya kijamii hivyo unatakiwa kutumia mitandao kwa nidhamu ya hali ya juu sana mambo tunayoyafanya mitandaoni yanaonwa na kukaa kama kumbukumbu kwa muda mrefu hivyo kama ni kubishana mitandaoni bishana kwa hoja na siyo kutoa ligha za matusi hii inaweza kukuathiri mahala fulani kwasababu huwezi jua unayemtukana kwenye mitandao ni nani wakati mwingine mwajiri wako yupo kwenye rafiki Wa rafiki yako au hata miongoni mwa rafiki zako discipline is the key .

3. To be continued.
 
Uzi mzuri sana huu aisee, kwa kipengele cha kwanza na cha pili umeelezea vizuri sana... Hongera na hivi ndio jamiiforums inapaswa kutumiwa na great thinkers
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom