Jinsi ya kusoma ujumbe wa Whatsapp kisiri bila ya aliyekutumia kujua kama umesoma ujumbe wake

embryo

Member
Apr 24, 2015
95
121
Jinsi ya kusoma ujumbe wa Whatsapp kisiri bila ya aliyekutumia kujua kama umesoma ujumbe wake
WhatsApp-Last-Seen-Timestamp-on-your-iOS-and-Android-devicesVitiki viwili vya bluu katika Whatsapp vinavyoashiria ujumbe umesomwa vina faida na hasara zake hasa linapokuja suala la kazi au mapenzi.
Kuna muda unajikuta upo busy na mihangaiko ya kimaisha na mmoja kati ya jamaa zako anaamua kukutumia sms Whatsapp, kwa haraka unaiangalia ile sms alafu unaiweka simu mfukoni ukisema nitaisoma baadae. Upande wa mtumaji anapata zile tiki mbili za bluu kuonyesha kama ujumbe wake tayari umesomwa, anakaa kwa hamu kusubiri majibu kutoka wako bila mafanikio. Hapo ndipo chuki zinapoanza kwa kuona kama umedharau ujumbe wake.
Chukulia kama aliyekutumia ujumbe huo ni mama mkwe, au baba mwenye
nyumba yako, au bosi wako ama mpenzi wako. Hapo utaona kuna umuhimu wa kuweza kuzima hizi alama za blue zinazoonyesha kusomwa kwa ujumbe.
Tayari tulishaelekezana hapa jinsi ya kuzima last seen, read receipt na kutoa profile picha katika makala iliyopita.
Leo ngoja tuangalie njia ya haraka tu ya kukuwezesha kusoma message za whatsapp bila mtumaji kujua kuwa umeshazisoma.

Pale message ya Whatsapp inapoingia usiifungue kwanza, nenda kwenye settings kisha weka airplane mode on, au bonyeza kitufe cha power moja kwa moja ili kupata menyu ya kuzima data kabisa
Ni muhimu kuzima data au kuweka simu katika airplane mode ili isiwe na uwezo wa kutuma na kupokea data kwa wakati huo. Hii ni kuzuia ujumbe wa kusomwa kwa mesage usirudi kwa mtumaji na kumwonyesha tiki mbili za bluu kwa sababu data ndio inayosafirisha ujumbe huu.
Baada ya hapo fungua application yako ya whatsapp na soma jumbe zako kwa amani.
Ukimaliza kusoma hakikisha unazima application ya Whatsapp kabisa kwa kutumia application manager yoyote uliyokuwa nayo, kisha washa data au zima airplane mode na mtu aliyekutumia atashindwa kuona zile tiki za bluu.

Angalizo: Ni muhimu kuhakikisha unazima data kabisa au unaweka airplane mode ili kuepusha kutumwa kwa ujumbe wa kusomwa kwa message yako. Unapomaliza kusoma hakikisha unaizima kabisa application ya whatsapp.
Tete Wenzeslaus
 
Afu cjaona hata faida yake jiamin cyo kuish kama jisi la ......nikajua somo zuri tena nikiwa na drive nimepaki gari yangu mayai pembezo japo nisome ujumbe mrefuuu wenye negative altitude kwangu na wengne kama mm hahaha huyu naye!!
 
Jinsi ya kusoma ujumbe wa Whatsapp kisiri bila ya aliyekutumia kujua kama umesoma ujumbe wake
WhatsApp-Last-Seen-Timestamp-on-your-iOS-and-Android-devicesVitiki viwili vya bluu katika Whatsapp vinavyoashiria ujumbe umesomwa vina faida na hasara zake hasa linapokuja suala la kazi au mapenzi.
Kuna muda unajikuta upo busy na mihangaiko ya kimaisha na mmoja kati ya jamaa zako anaamua kukutumia sms Whatsapp, kwa haraka unaiangalia ile sms alafu unaiweka simu mfukoni ukisema nitaisoma baadae. Upande wa mtumaji anapata zile tiki mbili za bluu kuonyesha kama ujumbe wake tayari umesomwa, anakaa kwa hamu kusubiri majibu kutoka wako bila mafanikio. Hapo ndipo chuki zinapoanza kwa kuona kama umedharau ujumbe wake.
Chukulia kama aliyekutumia ujumbe huo ni mama mkwe, au baba mwenye
nyumba yako, au bosi wako ama mpenzi wako. Hapo utaona kuna umuhimu wa kuweza kuzima hizi alama za blue zinazoonyesha kusomwa kwa ujumbe.
Tayari tulishaelekezana hapa jinsi ya kuzima last seen, read receipt na kutoa profile picha katika makala iliyopita.
Leo ngoja tuangalie njia ya haraka tu ya kukuwezesha kusoma message za whatsapp bila mtumaji kujua kuwa umeshazisoma.

Pale message ya Whatsapp inapoingia usiifungue kwanza, nenda kwenye settings kisha weka airplane mode on, au bonyeza kitufe cha power moja kwa moja ili kupata menyu ya kuzima data kabisa
Ni muhimu kuzima data au kuweka simu katika airplane mode ili isiwe na uwezo wa kutuma na kupokea data kwa wakati huo. Hii ni kuzuia ujumbe wa kusomwa kwa mesage usirudi kwa mtumaji na kumwonyesha tiki mbili za bluu kwa sababu data ndio inayosafirisha ujumbe huu.
Baada ya hapo fungua application yako ya whatsapp na soma jumbe zako kwa amani.
Ukimaliza kusoma hakikisha unazima application ya Whatsapp kabisa kwa kutumia application manager yoyote uliyokuwa nayo, kisha washa data au zima airplane mode na mtu aliyekutumia atashindwa kuona zile tiki za bluu.

Angalizo: Ni muhimu kuhakikisha unazima data kabisa au unaweka airplane mode ili kuepusha kutumwa kwa ujumbe wa kusomwa kwa message yako. Unapomaliza kusoma hakikisha unaizima kabisa application ya whatsapp.
Tete Wenzeslaus

Pole sana umetumia muda mwingi kuandika na kuwaelezea watz ila ulisahau kwamba Watz 85% ni vilaza, ona sasa wanavyokushambulia, jifunze siku nyingine usipoteze muda wako!
 
Kwenye iOS unaweza kuncheck read message kwenye settings tu na hata kwenye window phone kuna njia rahisi kuliko hiyo uloyoisema. Ila kwenye android ndio sijajua unaweza kuziondoa vipi kwa urahisi
 
Hata android ipo
 
Nadhani ulikuwa upo sahihi mpaka pale uliposema azime whatsapp kwa app manager, at least kwenye Android App zinaweza kusikiliza matukio kwenye simu yako na kujiwasha zanyewe, so kama WhatsApp inasikiliza pale simu itakapopata internet inajiwasha yenyewe kwenye background na kuanza kutuma na kupokea data, pia ukitumiwa msg hii inaingia kwa njia ya push na itaiamsha WhatsApp hata kama umeiua na task manager.

Kama una app ya firewall unaweza kuizuia WhatsApp isipate internet access wakati App zengine unaendelea kuzitumia.

Pia unaweza kuzima read notifications kwenye settings za WhatsApp aliyekutumia atakua haoni hizo tick ila na wewe hautaona tick kwenye msg unazowatumia watu.
 
Hii njiq itarumiwa sana na wanawake... Maana wao utakuta papuchi hataki kutoa ila hela za jamaa anazipenda hivyo anamzungusha na kumchuna tu jamaa wa watu...jamaa anabembeleza kwa kutuma message lakini message ikifika kwa mdada haifuti bila.kusoma ila anaisoma na hajibu kumbuka hajamblock jamaa kwa sababu anapenda pesa zake.lakini papuchi.kutoa sasa ndio.shida
 
Back
Top Bottom