Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mchaga

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
1,378
202
Wana JF naomba mwenye taarifa za taratibu za kusajili kampuni ya madini pale nyumbani Tanzania anisaidie.

Natanguliza shukrani zangu.

BAADHI YA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU:
UTANGULIZI
Kuanzia tarehe 1 Februari 2018 #BRELA ilitangaza kuanza kutumika kwa mfumo wake wa kuwawezesha wamiliki wa makampuni kusajili na kuwasilisha returns BRELA. Pia BRELA ilishatangaza kwamba mnamo tarehe 25 Machi 2018 mfumo wake wa awali wa OBRS uliokuwa unaruhusu kusajili jina la biashara na kufanya clearance ya jina la kampuni kupitia website ungefungwa rasmi ili kuuruhusu mfumo mpya wa ORS wenye uwezo wa kusajili majina ya biashara na makampuni kufanya kazi rasmi.

Hatua 10 za kufuata ili kusajili kampuni imeelezwa hapa chini, tafadhali fuatilia.

Kwa wale wanaohitaji kusajiliwa kampuni au jina la biashara chapu chapu tafadhali wasiliana nami kupitia kwenye ukurasa huu wa mawasiliano

HATUA 10 ZA USAJILI
Hatua #1: Taarifa za msajili

Ili kutumia mfumo huu mpya wa ORS mteja (msajili) anayetaka kusajili jina la kampuni anatakiwa kuwa na taarifa za msajili (msajili anaweza kuwa ni mmoja wa wakurugenzi, Katibu au Wanachama/Wenye hisa wa Kampuni tarajiwa).

Taarifa zenyewe ni:-
  1. Kitambulisho cha Taifa kwa wenyeji na Passport kwa wageni
  2. Simu ya kiganjani
  3. Barua pepe yaani email
Hatua #2: Taarifa za kampuni
Taarifa za kampuni zinazotakiwa ni:-
  1. Aina ya kampuni kama ni ya hisa au isiyo na hisa, ya binafsi au ya uma nk
  2. Jina la kampuni
  3. Tarehe ya kufunga mahesabu - mfano 31 Desemba
  4. Kumbuka: TIN No., Namba ya usajili zitawekwa na mfumo automatically
Hatua #3: Ofisi za kampuni
Taarifa za ilipo au itakapokuwa ofisi za kampuni ambazo ni:-
  1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
  2. Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
  3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namaba ya kiwanja, kitalu na nyumba,
  4. Sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
Hatua #4: Shughuli za Kampuni
Hatua #5: Taarifa za wakurugenzi
Taarifa zinazotakiwa za Wakurugenzi ni:-
  1. Aina ya mkurugenzi kama ni mtu au taasisi
  2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
  3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
  4. TIN
  5. Simu ya kiganjani
  6. Barua pepe yaani email
  7. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
    1. Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
      1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
      2. Kama halijapimwa tayarisha anuanii ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
      3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namaba ya kiwanja, kitalu na nyumba,
  8. Simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
Hatua #6: Taarifa za katibu wa kampuni
Taarifa za katibu wa kampuni (company secretary) zinazotakiwa ni:-
  1. Aina ya mtu kama ni mtu asili au taasisi
  2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
  3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
  4. Simu
  5. Barua pepe - email
  6. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
    1. Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
      1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
      2. Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
      3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, kitalu na nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
  7. Simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email na (sanduku la posta kwa ajili ya memart)
Hatua #7: Taarifa za wanachama/wenye hisa
Taarifa za wanachama au wenye hisa zinazotakiwa ni:-
  1. Aina ya mtu kama ni mtu au taasisi
  2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
  3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
  4. Simu
  5. Barua pepe - email
  6. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
    1. Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
      1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
      2. Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
      3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya
Hatua #8: Viambatanisho (Attachments in PDF)
Viambatanisho vinavyotakiwa kuambatanisha kwenye maombi (zote katika pdf) ni:-
  1. Memorandum and articles of association iliyosainiwa na wanachama/wenye hisa pamoja na mwanasheria wa uma (Notary Public)
  2. Form 14b iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi na mwanasheria wa uma (Notary Public)
  3. Ethics and Integrity Forms iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi
  4. Company consolidated form iliyosainiwa wakurugenzi wote na katibu wa kampuni
Hatua #9: Ada za usajili na kufaili (Different Fees)
Aina za ada ni kama ilivyoonyeshwa hapa chini
  1. Kusajili kampuni
  2. Kuhifadhi nyaraka na
  3. Stamp Duty
Hatua #10: Namna ya kulipa ada (Payment Methods)
Malipo ya ada yanafanyika kwa njia kuu tatu ambazo ni
  1. Kuweka Benki: Kwa njia y kuweka Fedha kwenye Tawi la Benki /Wakala wa Benki
    Nenda kwenye Tawi lolote la Benki / Wakala wa Benki ya CRDB /NMB kwa kutumia Namba ya Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
  2. Kwa njia ya Simu ya Mkononi: Tumia mtandao wa simu wa AirTell Money / Tigopesa/ MPesa/ HalloPesa kwa kuweka namba ya Kampuni 888999 na Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
  3. Kwa njia ya Kuhamisha Fedha: Unaweza kuhamisha Fedha moja kwa moja kutoka katika Benki yoyote kwenda kwenye Akaunti zetu zilizoko katika Benki ya NMB/ CRDB kwa njia ya TISS /SWIFT kwa kujaza: Namba ya Akaunti na Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
Kumbuka: Utaratibu wa malipo aidha kwa simu au benki utapewa ukishafikia hatua husika ya malipo

Soma zaidi kuhusu jinsi ya kufanya malipo BRELA Kupitia Simu Yako

HITIMISHO NA USHAURI
Brela sasa hivi hawataki usajili kwa njia ya zamani, yaani kupeleka makaratasi ngumu na kusubiri mlangoni kwa siku 6. Pia BRELA hawakubali mtu asiye na kitambulisho cha Taifa yaani #NIDA kusajili kampuni au jina la biashara.
Taarifa zilizotolewa hapo juu ni zile za lazima ambazo bila hizo huwezi kumalizia usajili na au usajili unaweza kukawia

Nashauri yafuatayo:
  1. Nashauri kama unataka kusajiliwa kampuni au jina la biashara kwa haraka wasiliana nasi kwa kutumia mawasiliano
  2. Kama huna kitambulisho cha Taifa na umeshaandikisha ili kupata kitambulisho cha Taifa, tembelea ofisi zozote za NIDA karibu na wewe ili wakupe angalau namba yako ya kitambulisho ili uweze kukitumia ukiambatanisha na Kibali cha BRELA ili Kupata Kitambulisho cha NIDA kwa haraka.
  3. Nashauri pia kama bado hujajiandikisha ni vyema ukawahi, hata kupitia kwenye eneo ambalo zoezi linaendelea ili uwahi kwa maana serikali imeanza kuzuia kupata huduma za public kama huna kitambulisho. ambatanisha pia Kibali cha BRELA ili Kupata Kitambulisho cha NIDA kwa haraka.
  4. Mwisho nashauri hizi taarifa zote uwe nazo mkononi kwa sababu huu mfumo wa usajili wa ORS unakupa siku sita (6 days) tu kukamilisha usajili kama baada ya hizo siku bado, taarifa zote zinafutika na itakubidi uanze upya from the scratch.

Bofya hapa: Hatua 10 Rahisi za Kusajili Jina la Biashara Kupitia Website ya BRELA
===
Taratibu za kisajili Kampuni, Tanzania.

Usajili wa kampuni (BRELA)na masuala mengine mengi kama vile Leseni ya biashara, hati miliki; hufanywa kwa mfumo wa wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS)
Hatua za lazima za kuingia kwenye mfumo wa ORS ni kama zifutazo;

(i) Kuwa na namba ya Utambulisho wa Utaifa inayotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
Namba ya Utambulisho wa Utaifa ndiyo kitambulisho pekee cha kuingia kwenye mfumo wa ORS. Wakurugenzi na Makatibu wa Kampuni pamoja na Namba ya Utambulisho wa Utaifa ni lazima pia wawe na Namba ya utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) na kama siyo watanzania wanapaswa kuwa na namba ya pasi ya kusafiria.

Kama ni mgeni (siyo Mtanzania) ambaye anatarajia kusajili Kampuni Tanzania anatakiwa awe na namba ya pasi ya kusafiria (Passport Number) au namba ya kitambulisho cha utaifa kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

(ii) Wakati unaandaa Malengo na Katiba ya Kampuni (Memorandum and Article of Association) hakikisha malengo unayojiwekea yameendana na shughuli unazozichagua kwenye mfumo wa ORS kwa mujibu wa ‘ISIC classification’ ambayo inapatikana kwenye mtandao na kwenye Tovuti ya BRELA www.brela.go.tz

Ili kuepuka usumbufu na kuchelewa hakikisha unakuwa na namba ya utambulisho wa Utaifa pamoja na namba ya utambulisho wa mlipa kodi kabla ya kuanza taratibu za usajili. Kwa kampuni zilizosajili zilizowasilisha maombi ya kusajiliwa kabla ya tarehe 1 Februari 2018, tafadhali zingatia yafuatayo:-

(i) Kuwa na Namba ya Utambulisho wa Utaifa (National Identification Number (NIN) inayotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

(ii) Wakurugenzi na Katibu wa kampuni kuwa na Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) na Namba ya Utambulisho wa Utaifa (NIN), kwa wasio Watanzania wawe na namba ya pasi ya kusafiria.

(iii) Ingia kwenye mfumo na uchague ‘Filing Annual Returns/ Accounts ingiza taarifa muhimu.

(iv) Kuhakiki taarifa za kampuni yako katika ofisi ya Msajili wa Makampuni ikiwa nyaraka kwenye jalada lako hazijasajiliwa au hujawasilisha Mizania (annual returns) ya miaka ya nyuma.
Note:Bila kuweka nyaraka zako kwenye mfumo, hutaweza kuwasilisha taarifa/mizania ya Mwaka, kubadilisha Makatibu wa kampuni, taarifa za benki na kadhalika.
===
Mkuu, ina kubidi kwanza uamue ni kampuni aina gani unayo taka kuanzisha.
Una weza kufanya biashara hiyo kwa kutumia jina lako binafsi, yaani bila ku-register jina la biashara. Hii utahitajika upate barua kutoka kwa mjumbe wa pale ofisi yako ilipo uipeleke pamoja na kitambulisho chako kwa mtendaji atakaye andika barua ya utambulisho kwa watoa leseni wilayani kwako. Baada ya kupata leseni utaenda ofisi za TRA husika kati ka eneo lako ili kupata TIN certificate. Hapo tayari unaweza kuanza kufanya biashara yako.

Unaweza pia kuanza kwa kusajili jina la biashara (Business name)
Business name una weza kusajili kama sole proprietor (una endesha biashara mwenyewe)
au partnership (ya watu wawili au zaidi). Unaweza pia kusajili Limited Company.
Usajili huu wa business name, partnership au Ltd Company utafanyika kwenye ofisi za BRELA zilizopo jengo la Ushirika, mnazi moja, Dsm. Utaandika barua ya kuomba usajili wa kampuni alafu watakujulisha kama hilo jina limesha sajiliwa tayari. Kama bado watakupa fomu za kujaza ili wakutengenezee vyeti vya usajili. Kwenye partnership na Ltd Company utahitaji usaidizi wa wakili ili kutengeneza Partnership deed au Memorandum and articles of Association ya Limited Company.

Kwenye bajeti ya juzi waziri alisema mtu binafsi ata ruhusiwa kusajili na kuanzisha Limited company hata akiwa mwenyewe. Sijui kama hili limesha pitishwa lakini limited company ilikuwa inahitaji watu wawili na zaidi.

BRELA watakupatia vyeti viwili, certificate of registration itakayo onyesha tarehe, jina na namba ya usajili ya kampuni yako na extract from register itakayo onyesha majina ya wenye kampuni. Watapiga mihuri yao pia kwenye partnership deed au Memorandum and articles of association kutegemea kama kampuni ni partnership au Ltd company.

Kama uliamua kutumia business name kwenye leseni hapo juu basi utaambatanisha certificate of registration na extract from register unapofuatilia kwa mtendaji, wilayani na TRA. Katika kila hatua kuna hela utalipia kwenye ofisi husika (Sina hakika sasa hivi ni kiasi gani- lakini sio hela nyingi), TRA ndio nadhani bado hawalipishi chochote kutoa TIN certificate.

Mkuu, usiogope kwenda ofisi yeyote kwa ajili ya kufuatilia usajili wa biashara yako. Kuna watu ambao wameajiriwa na serekali ili wakusikilize na wakuhudumie wewe. Maendeleo ya nchi hii pia inaanza na watu wenye uamuzi kama wako. Kuwa mjasiri na ujiamini kwa kila jambo na utafanikiwa. Nakutakia vyema.
===
1. Kwanza chagua jina halafu nenda Brela kasajili jina. It's a one day process.

2. Baada ya kupata 'OK' ya jina. Nenda kwa mwanasheria akuandalie documents mbili muhimu. Hii ni The Memorandum of the Company na Articles of Association copy nne nne. This is a Two days Job.

3. Unarudi Brella na kujaza forms na ku-submit na hizo documents na unalipia - applicable fees. This is another two days job.

In total 5 working days zinatosha kusajili kampuni. Ukianza Jumatatu, unamaliza Ijumaa. Kama una mkono mrefu, unaweza kufanyiwa kwa Fast Track na ukamaliza mambo yote in a day or two.
===
Habari zenu wanajamii napenda kukupa muongozo mfupi ikiwa wewe unahitaji kusajili kampuni yako au jina la biashara yako au nembo yako brela fuata taratibu hizi kwa:

1.COMPANY
-pendekeza jina la kampuni yako angalau majina matatu
-kuwa namba yako ya nida na washirika wenzako(shareholder/directors)
-TIN number zenu-hakikisha umehakiki TIN yako na mamlaka husika TRA
-Memorandum-andaa na hakikisha iko katika mpangilio unaofaa
-email address zenu wote
-namba zenu za simu wote
-anuani ya ofisi
-anuani ya makazi yenu wote

2.JINA LA BIASHARA
-Hatua hii haikuhitaji uwe na vitu vingi tofauti na ilivyo kwa upande wa kampuni hapa utaapaswa kuwa na majina pendekwa ya biashara yako uanayotaka kuisajili,Anuani ya biashara yako na makazi yako kwa maana ya mkoa ,wilaya,kata,mtaa,plot ,blok na house no na endapo unapoishi au biashara yako hapaja pimwa basi elezeza au tja kitu maarufu katika eneo hilo

NB:HAKIKISHA UNAPELEKA NYARAKA ZAKO KUPITIWA NA MWANASHERIA KABLA YA KUANZA PROCESS ZA KUSAJILI KAMPUNI YAKO IKIWA ZIMESAINIWA NANYINYI WOTE ZILE ZINAZOHITAJI KUFANYA HIVYO [PIA KUEPUKA ADHA YA KUBADILI JINA LA KAMPUNI YAKO UNAWEZA KUTUMIA NJIA HII YA KUSAJILI JINA LA BIASHARA KWANZA KISHA BAADAE UTALIPELEKA KATIKA USAJILI WA KAMPUNI]
Kwa msaada zaidi usisite kuwasiliana nasi +255764530882 na whtspp pia au tuandikie etj.prof@gmail.com
 
Uko nje ya nchi...unataka kuchimba madini...this is latest point ya mining....kwa maana halisi ni kwamba labda useme unataka kufanya exploration ya madini..tanzania..na hapo unasajili company ya exploration....

Unafanya utafiti maeneo yako then ukisha pata deposit ya kutosha ya madini kuweza kuchimba kwa mfani 5-10 Million Oz..(kipimo cha Gold)then unaweza ku apply Mining license.Ila unaweza at the same time ukawa na license mbili katika company moja nimeona kwenye company moja Tanzania royality company hawa wana licence ya mining and exploration..ila wamefanya kaujanja kamoja ka kuwa na company mbili katika mwamvuli mmoja.Moja ikiitwa mama na nyingine dada.

Kwa ushauli exploration mining tanzani ni ngumu sana hata ma kampuni makubwa sasa yanatapata shida kufanya kwa kuwa eneo kubwa la tanzania limeshafanyiwa utafiti unawe zakuwa na PL 100,100% ownership lakini ukifanya exploration kwa level ya kwanza haikupi matumaini kwenda level ya pili...at the end of the day inakuwa useless.

So kuwa makini sana unapo kuja kufanya mambo kam hii tanzania..most of wa wawekezaji wanakuja fanya JV(Join venture) na company zenye maeneo...kwani kuna about 50 - 100 exploration company kanda ya ziwa acha uko kusini mwa tanzania kwenye uranium.

Asubuhi njema
 
1. Kwanza chagua jina halafu nenda Brela kasajili jina. It's a one day process.

2. Baada ya kupata 'OK' ya jina. Nenda kwa mwanasheria akuandalie documents mbili muhimu. Hii ni The Memorandum of the Company na Articles of Association copy nne nne. This is a Two days Job.

3. Unarudi Brella na kujaza forms na ku-submit na hizo documents na unalipia - applicable fees. This is another two days job.

In total 5 working days zinatosha kusajili kampuni. Ukianza Jumatatu, unamaliza Ijumaa. Kama una mkono mrefu, unaweza kufanyiwa kwa Fast Track na ukamaliza mambo yote in a day or two.
 
1. Kwanza chagua jina halafu nenda Brela kasajili jina. Its a one day process.

Kwa nyongeza, hatua ya kwanza should be a "name search", kwahiyo ni lazima uende na barua uliyoiandika ukiomba kuangaliziwa jina. Kwa maana hiyo kwenye hiyo barua yako "utapropose" majina matatu ukiwa umeyapangilia kulingana na "priority order" yako.

Hao watu wa Brela wakishaipokea hiyo barua watakupa kama siku mbili ili waangalie kwenye database yao kama hayo majina (kufuatana na priority order yako) hayajatumika.Ukishajua ni jina lipi limekubaliwa ndipo sasa utatakiwa kuandaa Memorandum of Association na Articles of Associasion kwa kutumia jina lililokubaliwa.

Maelezo zaidi pata kwenye hii link.
 
Last edited:
Sasa hao BRELA wapo upande gani na jengo lipi hapa Dar es Salaam na Mikoani wana matawi? kuna Kigezo gani ukitaka Kampuni yako iwe LTD au Holdings,Enterprises etc. Samahani kwa swali la nyongeza mtatusidia wengi tu jamani lol!!!
 
Sasa hao BRELA wapo upande gani na jengo lipi hapa DSM na Mikoani wana matawi? kuna Kigezo gani ukitaka Kampuni yako iwe LTD au Holdings,Enterprises etc. Samahani kwa swali la nyongeza mtatusidia wengi tu jamani lol!!!

Mkuu umesoma hiyo link uliyopewa na Chibidu?
Wapo eneo la Mnazi Mmoja, mtaa wa Lumumba, jengo la Ushirika jijini Dar-es-salaam
 
Wataalam, asanteni sana. Hapa nimeelewa na nashukuru kwa link naona pia ina maelekezo niliyokuwa ninayahitaji. Nitawasiliana nikimaliza kusajili.
 
This is JF, Nami nilitaka fungua kampuni binafsi nadhani maelekezo haya yatanifaa sana. BIG THANKS...!
 
Kwa nyongeza, hatua ya kwanza should be a "name search", kwahiyo ni lazima uende na barua uliyoiandika ukiomba kuangaliziwa jina. Kwa maana hiyo kwenye hiyo barua yako "utapropose" majina matatu ukiwa umeyapangilia kulingana na "priority order" yako.

Hao watu wa Brela wakishaipokea hiyo barua watakupa kama siku mbili ili waangalie kwenye database yao kama hayo majina (kufuatana na priority order yako) hayajatumika.Ukishajua ni jina lipi limekubaliwa ndipo sasa utatakiwa kuandaa Memorandum of Association na Articles of Associasion kwa kutumia jina lililokubaliwa.

Maelezo zaidi pata kwenye hii link.
Yaani Mkuu nikushukuru sana kwa taarifa na link its very informative. Thanks.
 
Hizi biashara za kuonana na receptionist ndio zinaumiza wananchi!, haya mambo kama vipi yafanyike online tuu, kuna kila sababu ya kufanyia hizi issue online, sioni kwa nini lazima tuonane na watu. ndio maana rushwa haitokoma TZ. Tujifunze kuokoa muda.

B.
 
Kumbuka, baada ya kusajili kampuni (Incorporation) na kabla ya kuanza biashara utatakiawa kupata leseni ya biashara (business licence) na pia kujisajili kama mlipa kodi (TIN certificate).

Nakutakia mafanikio.

Je nikisha sajili hiyo kampuni natakiwa nilipe nini kwa TRA, na je consultancy firms nazo zinasajiliwa Brella??

Tafadhali wakuu nifahamisheni hapo.
 
Pasco kaizungumza hii ishu kama ni rahisi. Ebwana jiandae kuna watu wananuka rushwa pale. Mie aliremember, ilinichukua miezi 2 kukamilisha kuna danadana za kijinga saana.
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom