Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ila BRELA mjitafakari sana, msione sifa watu wakiwa wanatafta vishoka ili wawasaidie kusajili kampuni. Mi natoka mkoani nakaa week mnanizungusha tu. Milolongo kibao na mwisho wa siku naamua kuachana na usajili maana naona nazidi kufilisika tu.

Kingine kwanini BRELA msihamie Dodoma wakati serikali yote ishahamia Dodoma?

Niko moto sana na hii Agency.
 
Heshima kwenu wote,
Naomba kupata mtu anayeweza kunisajilia kampuni yangu BRELA na kupata certificate of incorporation kwa haraka.
Nina memorandum na vitambulisho vya taifa na TIN number tayari.
Mwenye kuweza fanya hii kazi aje PM akinieleza namna anavyoweza kuifanya na gharama zake.
Asante.
FIVE working days, I hand over the certificate to you! Pia I will assist you with legal management for six months free of charge!
 
FIVE working days, I hand over the certificate to you! Pia I will assist you with legal management for six months free of charge!
Can you plz release your mobile phone # here as am in the same recourse as the thread capitation.
 
Kwa nyaraka ulizonazo unaweza kuajisajili mwenyewe kupitia kwenye mtandao kama una Laptop Desktop, au Simu yenye uwezo mkubwa. Vinginevyo nenda pale BRELA mtaa wa Lumumba, wana kitengo kinachotoa huduma ya usajili. Ila jihadhari na vishoka, watakudaka hata kabla hujafika ofisi yenyewe. Kila la kheri.
 
Kama kichwa kinavyojieleza, ni company yenye mtaji usiozidi million 10. Natanguliza shukrani. Ahsanteni.
 
Afrolink-Tz Consult Ltd, Hello, nilikuwa nina swali kwa upande wakupata TIN ya biashara. Je Kama mtu unataka kufanya online business; vile vipengele vya hati ya pango na eneo la biashara unajazaje?

Note online business, I mean Kama unatumia Instagram, WhatsApp etc. Hauna physical shop.

Looking forward to hear from you.

-callmeGhost

Sent using Jamii Forums mobile app
 
callmeGhost,
Hello
Kupata TIN utafuata btararibu za kawaida tu. Suala la mahala unapokaa kufanya kazi zako ndiyo hapohapo eneo lako la biashara japo bidhaa zipo online. Hivyo basi utachukua mkataba kama umepanga nyumba/chumba utaenda nao TRA
 
Asante kwa elimu:
Maswali:
1) Asiye mtanzania awe na paspoti , vipi kuhusu TIN awe nayo?
2) Je, agent anaweza wasainia kwa niaba, wakurugenzi ktk consolidated form? Ikiwa wako mbali?
3) Je mfumo wa kuorodhesha shughuli za kampuni ktk memart uko kama wa zamani au unaorodhesha kwa vipengele kama ilivyo ktk ISICS REV4?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za mida wakuu.
Nina hoja naleta kwenu kwa msaada. Natarajia kuchimba gold hivi karibuni na nguvu za kusajili ili kupata leseni au kibali sina. Jee naweza watosa wachimbaji wakati nasubiria nguvu ipatikane ndio niende? Na jee haitakua shida pindi wakija kagua ingawa site ipo uchaka ni vigumu watu kupajua ni zaidi ya huyu mtaalamu wangu.
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom