Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Asante Mkuu thesym

Tatizo halipo upande wa BRELA bali lipo upande wa NIDA. Hivyo basi unachotakiwa kufanya ninkwenda ofisi za NIDA na kuelezea tatizo lako utasaidiwa. Maana yake ni kwamba kitambulisho chako hakijawa "activated"

Vlvl kwa kuongezea tu huwa inatikea hata ktk TIN. Iwapo haisomi huwa kuna mawili:

1. Inawezekana majina yako umetofautisha herufi baina ya majina uliyosajili ktk TIN vs NIDA. Hivyo kuonekana kama watu wawili tofauti. Hakikisha majina yawe yenye kufanana ie TIN vs NIDA names to be the same.

2. TIN haisomi. Inawezekana pia huku "update" TIN yako wkt wa zoezi la kuhuisha maelezo. Au haijawa activated pia. Hivyo rudi mahala husika na si kutupa lawama BRELA. BRELA wajibu wao ni kuunganisha link (database) ya majina na utaifa wk tu
 
BRELA wana matatizo sana..Mkurugenzi katumbuliwa bado matatizo yao hayaishi...Hii ya kutumia kitambulisho cha Taifa ni upuuzi sababu vitambulisho vya Taifa bado watu wengi hawajapata
Ni kweli Mkuu watu wengi hawajapata. Lkn BRELA wanatoa barua ya kukurahisishia kupata kitambulisho kwa muda mfupi baada ya kukamilisha kujaza fomu zote. Hivyo unachofanya, unapotaka kurudisha fomu ulizojaza ambatanisha na barua kutoka BRELA
IMG_20180914_093550.jpg
 
BRELA wanamatatizo, mwaka juzi nilataka kusajili kampuni wakanikatalia wakesema na miaka 17 nisubiri mpaka nifikishe 21, nikarudi manispaa wakanisajilia biashara tu
 
BRELA wanamatatizo, mwaka juzi nilataka kusajili kampuni wakanikatalia wakesema na miaka 17 nisubiri mpaka nifikishe 21, nikarudi manispaa wakanisajilia biashara tu
Mkuu umri huo wa miaka 17 si bado mtoto kwa mujibu wa sheria? Mm naona BRELA wapo sahihi. Hebu tuwaite wanasheria watolee ufafanuzi juu ya umri huu a miaka 17. Ingekuwa miaka 18 ningekua pamoja nawe kwa hili la BRELA
 
Mkuu umri huo wa miaka 17 si bado mtoto kwa mujibu wa sheria? Mm naona BRELA wapo sahihi. Hebu tuwaite wanasheria watolee ufafanuzi juu ya umri huu a miaka 17. Ingekuwa miaka 18 ningekua pamoja nawe kwa hili la BRELA
nishafanikiwa ila duuh utata mtupu
 
Taratibu za kisajili Kampuni, Tanzania.

Usajili wa kampuni (BRELA)na masuala mengine mengi kama vile Leseni ya biashara, hati miliki; hufanywa kwa mfumo wa wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS)
Hatua za lazima za kuingia kwenye mfumo wa ORS ni kama zifutazo;

(i) Kuwa na namba ya Utambulisho wa Utaifa inayotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
Namba ya Utambulisho wa Utaifa ndiyo kitambulisho pekee cha kuingia kwenye mfumo wa ORS. Wakurugenzi na Makatibu wa Kampuni pamoja na Namba ya Utambulisho wa Utaifa ni lazima pia wawe na Namba ya utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) na kama siyo watanzania wanapaswa kuwa na namba ya pasi ya kusafiria.

Kama ni mgeni (siyo Mtanzania) ambaye anatarajia kusajili Kampuni Tanzania anatakiwa awe na namba ya pasi ya kusafiria (Passport Number) au namba ya kitambulisho cha utaifa kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

(ii) Wakati unaandaa Malengo na Katiba ya Kampuni (Memorandum and Article of Association) hakikisha malengo unayojiwekea yameendana na shughuli unazozichagua kwenye mfumo wa ORS kwa mujibu wa ‘ISIC classification’ ambayo inapatikana kwenye mtandao na kwenye Tovuti ya BRELA www.brela.go.tz
Ili kuepuka usumbufu na kuchelewa hakikisha unakuwa na namba ya utambulisho wa Utaifa pamoja na namba ya utambulisho wa mlipa kodi kabla ya kuanza taratibu za usajili. Kwa kampuni zilizosajili zilizowasilisha maombi ya kusajiliwa kabla ya tarehe 1 Februari 2018, tafadhali zingatia yafuatayo:-

(i) Kuwa na Namba ya Utambulisho wa Utaifa (National Identification Number (NIN) inayotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

(ii) Wakurugenzi na Katibu wa kampuni kuwa na Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) na Namba ya Utambulisho wa Utaifa (NIN), kwa wasio Watanzania wawe na namba ya pasi ya kusafiria.

(iii) Ingia kwenye mfumo na uchague ‘Filing Annual Returns/ Accounts ingiza taarifa muhimu.

(iv) Kuhakiki taarifa za kampuni yako katika ofisi ya Msajili wa Makampuni ikiwa nyaraka kwenye jalada lako hazijasajiliwa au hujawasilisha Mizania (annual returns) ya miaka ya nyuma.
Note:Bila kuweka nyaraka zako kwenye mfumo, hutaweza kuwasilisha taarifa/mizania ya Mwaka, kubadilisha Makatibu wa kampuni, taarifa za benki na kadhalika.
 
Habarini za asubuhi ndugu zangu....

Poleni na pilikapilika za kutafuta chakula cha kila siku...

Mada

Nataka kujua je kuna uwezekano wa kusajili kampuni as "INTERNATIONAL NON GOVERNMENT ORGANIZATION"

Na kama inawezekana pale BRELA, process zake zimekaaje..

Asanteni:
 
Hii ni taasisi sio kampuni, unatakiwa uwe na muhtasari wa kikao cha wajumbe waliokaa na kukubali kuanzishwa kwa taasisi, CV's au Wasifu wa Mwenyekiti, Katibu na mweka hazina. Barua ya Afisa maendeleo wa mkoa, wilaya, halmashauri au Manispaa ambayo inakutambulisha, passport size mbili kwa Katibu, Mwenyekiti na mweka hazina.

Ada yake ni 115000 kama sijakosea hii ada ni kwa taasisi inayokusudia kufana kazi zake ndani ya tanzania
Pia unatakiwa ujaze form namba moja ya NGOs'
Usajili wake haufanyiki brela unafanyika wizarani huku Dodoma ofisi zao ziko udom wizara ya afya, jinsia na maendeleo ya jamii kama sijakosea ila ni wazar ya afya
 
Heshima kwenu wote,
Naomba kupata mtu anayeweza kunisajilia kampuni yangu BRELA na kupata certificate of incorporation kwa haraka.
Nina memorandum na vitambulisho vya taifa na TIN number tayari.
Mwenye kuweza fanya hii kazi aje PM akinieleza namna anavyoweza kuifanya na gharama zake.
Asante.
 
Back
Top Bottom