Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Je kufungua financial consulting ni kiasi gani na je kusajili jina ni kiasi gani je nikitaka nianze kukopesha nahitajika nitoe kiasi gani… ……
 
Msaada wana jamvi
Naomba kujuzwa juu ya masharti ,sheriA Na taratibu za kufungua cosmetics shop pamoja na mtaji minimum wa kuanza nao
Asalaam nawasilisha
Kufungua biashara
Unatakiwa kufuata taratibu za kufungua biashara, sasa hujasema unataka kufungua kama kampuni au mtu binafsi au kwa jina la biashara.

Kama binafsi kasajili TIN ya biashara TRA (nenda TRA na barua ya utambulisho wa wa eneo lako la biashara, Mkataba wa pango, utajaza fomu za maombi ya TIN, na makadirio ya kodi),
Pita TFDA upate mwongozo wa vipodozi vinavyoruhusiwa na visivyoruhusiwa. Utalipia na ada pale na kupata cheti pia.
Chukua TIN, cheti cha TFDA, Mkataba wa pango wa eneo la biashara na kuna fomu ya kujaza ya kuombea leseni ya biashara, utajaza na kupat leseni.

Gharama uanze na kiasi gani Mtajinpmj na hizi gharama ni ngumu kujua exactly kwa sbb hujaweka mtaji kiasi gani, hujasema unafungua kama kampuni au binafsi. Lkn kwa uzoefu wa biashara za vipodozi jitahidi kuwa na mtaji mkubwa kdg kutokana na vipodozi "vya maana" ni gharama. Mzigo wa mil 5 unaweza shangaa mzigo umejaa ktk boksi saizi ya kati
 
Kwanini Brela wanazingua kusajili Kampuni ? Kila siku wanasema system IPO down sijui INA matatizo, je ni Kweli hii kitu au ni hujuma wakati MTU umelipia kila kitu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini Brela wanazingua kusajili Kampuni ? Kila siku wanasema system IPO down sijui INA matatizo, je ni Kweli hii kitu au ni hujuma wakati MTU umelipia kila kitu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakushauri ingia ktk website yao www.brela.go.tz juu pale pna kipengele cha contacts, cheki utaona namba za simu kuwasilisha malalamiko. Wasilisha hapo kwa kumpigia cm ya mkononi mhusika moja kwa moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hata hizi non-profit associations nazo zinasajiliwa BRELA? Kama siyo, ni taasisi gani inasajili hizi associations?
NB: Non-profit associations ni taasisi/kampuni zisizo za kibiashara. Msaada tafadhali.
 
Hivi hata hizi non-profit associations nazo zinasajiliwa BRELA? Kama siyo, ni taasisi gani inasajili hizi associations?
NB: Non-profit associations ni taasisi/kampuni zisizo za kibiashara. Msaada tafadhali.
Zinasajiliwa BRELA pia ambazo zinakuwa ni limited kampuni zisizo na shea (non-profit associations)
Gharama zake angalia ktk fomu ya "fee structure" za BRELA ni 300k+ (cheki no 2)

Ukisajili hii then unaweza kusajili km NGO ktk ngazi ya utendaji wilaya, mkoa, taifa au kimataifa Wizara ya Maendeleo ya Jamii na watoto
Screenshot_2018-09-02-21-00-39-60.jpg
IMG_20180818_225120.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • IMG_20180818_225120.jpg
    IMG_20180818_225120.jpg
    57.9 KB · Views: 185
Wakuu nasajili kakampuni kangu kadogo BRELA. Nataka kwanza nipate jina la kampuni. Sasa nikiingiza namba ya kitambulisho changu wananambian person not found, nipo na mawazo hapa anayejua wanaingizaje namba anisaidie wadau
 
Nenda kwenye ofisi za NIDA wachukue alama za vidole. Inakuwa kama wana-activate hicho kitambulisho kwenye system. Bila kuchukua alama za vidole wakati wa kupewa kitambulisho chako hakitaweza kutambulika.

NB: Siku ya kupiga picha ulichukuliwa alama za vidole, hilo halihusiani na kuchukuliwa alama tena wakati wa kuchukua kitambulisho.
 
BRELA wana matatizo sana..Mkurugenzi katumbuliwa bado matatizo yao hayaishi...Hii ya kutumia kitambulisho cha Taifa ni upuuzi sababu vitambulisho vya Taifa bado watu wengi hawajapata
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom