Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Yaani nilitafuta sana msaada wa watu kama nyinyi Afrolink, nitawatafuta soon
 
Mkuu hizi hatua kumi rahisi ni Kwa ajili ya business name registration au companies registration? Na je naweza sajili kampuni online bila kufika BRELA? Msaada pls
Mwishoni mwa maelezo kuna kiunganishi kwenda kwenye hatua 10 za kufuata ili kusajili kampuni kupitia website ya brela.
Kwa sasa usajili wote unafanyikia kwenye website, brela hawapokei tena karatasi ngumu
 
Napenda kuwajuza wana JF kwa yoyote mwenye uhitaji wa kusajili company limited au business name au mwenye swali lolote kuhusu usajili wa brela unaweza kuniuliza hapa au kuni PM for more info.
Asante
 
Uzi huu umekuja wakati mwafaka wakati nikijipanga kwenda BRELA, ni vitu gani ninahitaji kuwa navyo pindi ninapotaka kufungua kampun(registration) hapa kwetu?
 
Uzi huu umekuja wakati mwafaka wakati nikijipanga kwenda BRELA, ni vitu gani ninahitaji kuwa navyo pindi ninapotaka kufungua kampun(registration) hapa kwetu?
Cha kwanza kabisa unatakiwa kuwa na kitambulisho cha taifa au namba ya kitambusho cha taifa.

Bila hicho huwezi kufungua akaunti ambayo itakuwezesha kufanya shughuli yoyote kwenye system kama business name registration nk.
 
Mbadala wa kitambulisho cha taifa??
 
Hatua zipi na nyaraka zipi zinatakiwa kusajili biashata km ya utalii..??
 
k
Cha kwanza kabisa unatakiwa kuwa na kitambulisho cha taifa au namba ya kitambusho cha taifa.

Bila hicho huwezi kufungua akaunti ambayo itakuwezesha kufanya shughuli yoyote kwenye system kama business name registration nk.
ama bado sijjapata kitambulisho nifanyeje?
 
Napenda kuwajuza wana JF kwa yoyote mwenye uhitaji wa kusajili company limited au business name au mwenye swali lolote kuhusu usajili wa brela unaweza kuniuliza hapa au kuni PM for more info.
Asante
Kufungua kampuni ambayo itakua inaoperate online tu brela mnahusika hapo?
 
msaada wakuu kwa mfano nikisajili jina la biashara vip kuhusu kodi lazima mahesabu yakaguliwe na auditor au TRA watanikadiria tu
 
msaada wakuu kwa mfano nikisajili jina la biashara vip kuhusu kodi lazima mahesabu yakaguliwe na auditor au TRA watanikadiria tu
Mkuu ipo hivi
1. Sheria ya kodi inakutaka kuandaa hesabu za mizania (audited financial statements) pasina kujali ni jina la biashara, mtu binafsi au kampuni kama na kama tu mauzo yako yanavuka milioni 20 kwa mwaka. Hivyo kama mauzo ya biashara yako yapo ktk kiwango nilichoainisha unalazimika kuandaa mahesabu na kukaguliwa baada ya hapo ndo utapeleka TRA ktk kulipa kodi na vlvl BRELA katika kulipa Annual Returns pia

2. Kwa kukuongezea tu kwa faida zaidi na kama mauzo yako yapo juu ya milioni 14 unalazimika kuwa na mashine ya kielektroniki ya risiti (EFD machine)

3. Na kama mauzo yako yapo kuanzia mil 100 jitahidi na usajili kabisa na VAT. Lkn kama unafanya biashara za kitaalam, haijalishi unauza kiasi gani unlazimika kusajili VAT pia. Hata kama ni mil 2 kwa mwaka lkn ikiwa tu biashara ya taaluma (hudima) kama vile Consultant, injinia nk
 
Msaada wana jamvi
Naomba kujuzwa juu ya masharti ,sheriA Na taratibu za kufungua cosmetics shop pamoja na mtaji minimum wa kuanza nao
Asalaam nawasilisha
 
Back
Top Bottom