Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Nimewauliza hilo wakajibu Kitambulisho cha Taifa ni lazima na kama bado kabisa itabidi usubiri tu. Ndio hali halisi
Aise, huko ni kudumaza maendeleo, bora wangeweka vitambulisho viwili au vitatu ukikosa hichi jnaleta hichi mfano passport au Leseni ya Gari.
 
Hongera kwa kazi nzuri ya kuelimisha jamii mimi nafanyaga hizi kazi ila kwa ufafanuzi uliotoa hapa nakupa hongera mno mtu akiifuatilia haya yote yanawezekana akiwa nyumbani kwake umetoa detail za kutosha mno.

Naomba kuongezea tu na kwamba kila kampuni inatakiwa kuanza kwa kuupdate information zake na ni vyema kufanya hivyo mapema na kama hamna hivyo vitambulisho basi mtafute ilie muanze na kufanya annual returns ambayo ni njia mojawapo ya kuupdate taarifa za kampuni.

Hongera na Ahsante mno.
 
lembu,
Mimi nilisajili mpaka hapo kwenye Namba 8 nikakwama. Ebu nieleweshe na Attach nini Maana hapo ndo nilipofikia nikakwama
 
Nashukuru sana mtoa post! kwa andiko hili, nitafanya kama ulivyoelekeza nitahakikisha nna taarifa zote ndio naanza kujaza.
 
Mimi nilisajili mpaka hapo kwenye Namba 8 nikakwama. Ebu nieleweshe na Attach nini Maana hapo ndo nilipofikia nikakwama
Hello mfuga kuku
unatakiwa kupakua Business Name Consolidated Form ambayo utatakiwa kuisain na kurudisha kwenye website kama pdf, Baada ya hapo utaendelea na malipo ya ada kupitia banki au mobile phone. Consolidated form unatakiwa kuisubiri angalau kwa dakika moja ili system iweze kukutayarishia
 
Mkuu hata kutoa elimu inahitaji authorization ya BRELA au hukupima ulichouliza! Hata hivyo BRELA hawana authorized agents kama ilivyo makampuni ya simu. Wao wanachotaka kampuni au biashara imesajiliwa kwa kufuata sheria na taratibu zao period.
Mawakala wa Usaji Wapo mkuu
 
Msaada mkuu...pale kweny representative statement natakiwa kujaza nini?
Hata mimi nimekwama kwenye hii hatua ukipata solution unijuze.Sipati ushirikiano mzuri na namba za Msaada za BRELA zilizopo kwenye mtandao.
 
Hata mimi nimekwama kwenye hii hatua ukipata solution unijuze.Sipati ushirikiano mzuri na namba za Msaada za BRELA zilizopo kwenye mtandao.
Polee mkuu ,yani walitakiwa kwanza watoe form yenye kueleze kila jinsi ya kujaza had kumalza zoez...ngoja tusubri majibu hapa
 
Wakuu,
Hivi huu usajili mpya wa Brela moja kwa moja mtandaoni,

Ndo mbadala wa kile kile tulichokua tunakifanya cha kwenda kwa afisa BIASHARA halmashaur kujisajili?

Au hiki ni kitu kipya?,
kwamba ukishajisajili humo mtandaoni ndo imeisha hiyo

au bado utalazimika tena kwenda kwa afisa biashara.

Ufafanuzi hapo wakuu
 
Hongera kwa kazi nzuri ya kuelimisha jamii mimi nafanyaga hizi kazi ila kwa ufafanuzi uliotoa hapa nakupa hongera mno mtu akiifuatilia haya yote yanawezekana akiwa nyumbani kwake umetoa detail za kutosha mno. Naomba kuongezea tu na kwamba kila kampuni inatakiwa kuanza kwa kuupdate information zake na ni vyema kufanya hivyo mapema na kama hamna hivyo vitambulisho basi mtafute ilie muanze na kufanya annual returns ambayo ni njia mojawapo ya kuupdate taarifa za kampuni. Hongera na Ahsante mno.
Mkuu,
Naomba ufafanuz tafadhar.

Kwa mfumo huu mpya,
Kwa mfano unaanzisha biashara mpya

Na ukafanikiwa kuisajili mtandaoni na kulipia hizi gharama (15,000 +5000) huko Brela kama hatua zlvoelekeza.

Ndo imeishia hapo?

Kwamba ule utaratibu wetu tulozoea wa kwenda kusajili halmashaur na kuchukua leseni ndo hauna tena maana au vipi?

Vipi kuhusu leseni Hardcopy naipata pataje chini ya huu mfumo?

Ufafanuz tafadhari
 
Naomba namba ya makao makuu NIDA,kuna jamaa yangu yuko sumbawanga anahitaji kupata namba tu ilikufungua kampuni ni mwezi sasa,juzi kapata namba ya simu ya msimamizi wa NIDA manispaa ya sumbawanga na kumpigia ili apewe namba ya usajiri nida ulizuka mgogoro mkubwa sana msimamizi akidai aambiwe kwanza namba yake imepatikanaje sivyo hatoi namba na jamaa yangu hakutaja alipoipata namba na kweli akamnyima namba hiyo ya NIDA,tumejaribu kutafuta NIDA makao makuu kwa na. 0687416666 inakata tu na simu za mezani (ttcl) hazipokelewi.


Namba ya ofisa wa NIDA aliyegoma kutoa na. ya usajiri wa NIDA ili tusajir kampuni na kuanza kulipa kodi serikalini kwa kwa sharti hadi atajiwe alikoipata namba yake ni Bw. KABANJA +255768205055

NIDA ONDOENI HUU URASMU MNAIKOSESHA MAPATO SERIKALI KWA KIBURI
 
Kusajili jina la biashara sio kupata leseni halmashauri... Ukishapata certificate of Reg, nenda halmashauri na Tin yako ujipatie leseni hardcopy.. Brela huendi.

Kuhusu hoja ya Bujibuji, nadhani sio dhambi endapo kunatokea watu wenye weledi, muda na uzoefu ktk mchakato huu wakajinafasi kuwasaidia wasioweza mchakato huu kwa namna moja au nyingine. Ukiona elimu aliyotoa mtoa post imekufaa na unaweza mwenyewe Go ahead.. Ila maisha ni kugawana vijikazi. Huwezi fanya hiyo wape watu wakusaidie najua malipo kidogo yapo.. Maana hiyo pia ni kazi.. Sio kila mtu anajua, na huo mchakato hauna sura ya mtu kukutapeli, madam ujue unadeal Vipi.

Kuhusu NIDA, serikali wameamua kutumia vitambulisho hivi maana taarifa za kila mtu zinakuwa easily verified by authorities.. Ukigusa mfumo wowote online kwa no ya id hiyo taarifa zako zinaonekana, hapa wameepusha mambo mengi sana ya utapeli, uhujumu uchumi nk nk. Wananchi tukubaliane na mpango huo, nenda kajiandikishe NIDA,
 
Hapo Jaza Director, Owner or Partner yaani inategemeana wewe ni nani katika hiyo kampuni. Na kama ni representative wa kazi hiyo

Hata mimi nimekwama kwenye hii hatua ukipata solution unijuze.Sipati ushirikiano mzuri na namba za Msaada za BRELA zilizopo kwenye mtandao.
 
Hapo Jaza Director, Owner or Partner yaani inategemeana wewe ni nani katika hiyo kampuni. Na kama ni representative wa kazi hiyo
Yan statement ya uwakilishi ndio unajaza Director,owner au partner?
 
Hivyo ndio inataka, Yaani wewe unaiwakilisha kampuni kama nani. Na sheria imeelekeza ni nani anaruhusiwa kuwakilisha kampuni. Ahsante
Asante mkuu wacha tuendelee.
.nikikwama nitarud mkuu usituchoke
 
Inachukua mda gani kupata registration business certificate ? Mimi nmefanya hatua zote, hadi nikalipa, na nikapewa receipt... Ila status ikaonyesha niedit anuani ya makazi in full, nikafanya... Tangu tareh 8 /5 sioni mwendelezo, zaidi ya status inayosema task... Corrections
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom