Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Inamaana baada ya kua aproved alaf sjafanya ORS ndan ya siku sita nitakua nmepoteza info zote za kule obrs?
OBRS haipo tena. Kama hujamaliza application ndani ya siku sita kila kitu kinafutwa itakubidi uanze upya, ndio maana nikashauri kwa kusisitiza uwe na taarifa zote kabla hujaanza kuomba kwa sababu ukikosa hata taarifa ndogo inaweza kukufanya urudie rudie mpaka uchoke
 
Anhaaa kumbe OBRS haipo tena..bas nina kibarua cha kuanza upya..ID ya uraia ndio ilinikwamisha kdgo..thanks...nikiwa na shida nita ku pm mkuu
 
Je nikitaka kusajili jina la biashara? mm nna biashara ambazo sijazisajili nimeshindwa kuuza supermarket wameniambia hadi nizisajili, hebu nisaidie steps au ndio hizo hizo hapo juu ktk post?
 
UTANGULIZI
Kuanzia tarehe 1 Februari 2018 #BRELA ilitangaza kuanza kutumika kwa mfumo wake wa kuwawezesha wamiliki wa makampuni na biashara kusajili na kuwasilisha returns BRELA. Pia BRELA ilishatangaza kwamba mnamo tarehe 25 Machi 2018 mfumo wake wa awali wa OBRS uliokuwa unaruhusu kusajili jina la biashara na kufanya clearance ya jina la kampuni kupitia website ungefungwa rasmi ili kuuruhusu mfumo mpya wa #ORS wenye uwezo wa kusajili majina ya biashara na makampuni kufanya kazi rasmi.

Hatua 10 za kufuata ili kusajili jina la biashara imeelezwa hapa chini, tafadhali fuatilia.

Kwa wale wanaohitaji kusajiliwa kampuni au jina la biashara chapu chapu tafadhali wasiliana nami kupitia kwenye ukurasa huu wa mawasiliano

HATUA 10 ZA USAJILI
Hatua #1: Taarifa za msajili, mmiliki au wamiliki wa biashara

  1. Kitambulisho cha Taifa kwa wenyeji na Passport kwa wageni
  2. Simu ya kiganjani
  3. Barua pepe yaani email
Hatua #2: Taarifa za biashara
  1. Aina ya biashara mtu binafsi, washirika au shirika
  2. Jina la biashara
Hatua #3: Ofisi ya biashara (Business Location)
  1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
  2. Kama halijapimwa tayarisha anuanii ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa.
  3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, namba ya kitalu na namba ya nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe (email)
Hatua #4: Shughuli za Biashara (Business Activities)
Hatua #5: Taarifa za Wamiliki (Business Owner’s Information) pamoja na Akaunti ya Benki kama ipo
  1. Aina ya mmiliki kama ni mtu au taasisi
  2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
  3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
  4. TIN
  5. Simu ya kiganjani
  6. Barua pepe yaani email
  7. Anuani ya makazi kwa kila mmiliki kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
Hatua #6: Taarifa za Akaunti ya Benki Zingine kama ipo (Business Bank Account Information)
  1. Aina ya mmiliki kama ni mtu au taasisi
  2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
  3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
  4. TIN
  5. Simu ya kiganjani
  6. Barua pepe yaani email
  7. Anuani ya makazi kwa kila mmiliki kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
Hatua #7: Taarifa za Wawakilishi (Person who can update ORS Information)
  1. Aina ya mmiliki kama ni mtu au taasisi
  2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
  3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
  4. TIN
  5. Simu ya kiganjani
  6. Barua pepe yaani email
  7. Anuani ya makazi kwa kila mmiliki kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
Hatua #8: Viambatanisho (Attachments in PDF)
Viambatanisho vinavyotakiwa kuambatanisha kwenye maombi (zote katika pdf) ni:-
  1. Consolidated form iliyosainiwa wamiliki wote wa biashara
  2. Viambatanisho vingine vinakuja - Mkataba wa washirika kama wamiliki ni zaidi ya mtu mmoja
Hatua #9: Ada za usajili na kufaili (Different Fees)
Aina za ada ni kama ilivyoonyeshwa hapa chini
  1. Kusajili biashara = TZS. 15,000
  2. Kuhifadhi nyaraka na = TZS. 5,000/mwaka
Hatua #10: Namna ya kulipa ada (Payment Methods)
Malipo ya ada yanafanyika kwa njia kuu tatu ambazo ni
  1. Kuweka Benki: Kwa njia ya kuweka Fedha kwenye Tawi la Benki /Wakala wa Benki
    Nenda kwenye Tawi lolote la Benki / Wakala wa Benki ya CRDB /NMB kwa kutumia Namba ya Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
  2. Kwa njia ya Simu ya Mkononi: Tumia mtandao wa simu wa AirTell Money / Tigopesa/ MPesa/ HalloPesa kwa kuweka namba ya Kampuni 888999 na Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
  3. Kwa njia ya Kuhamisha Fedha: Unaweza kuhamisha Fedha moja kwa moja kutoka katika Benki yoyote kwenda kwenye Akaunti zetu zilizoko katika Benki ya NMB/ CRDB kwa njia ya TISS /SWIFT kwa kujaza: Namba ya Akaunti na Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
Kumbuka: Utaratibu wa malipo aidha kwa simu au benki utapewa ukishafikia hatua husika ya malipo

Soma zaidi kuhusu jinsi ya kufanya malipo BRELA Kupitia Simu Yako

HITIMISHO NA USHAURI
Brela sasa hivi hawataki usajili kwa njia ya zamani, yaani kupeleka karatasi ngumu na kusubiri mlangoni kwa siku 6. Pia BRELA hawakubali mtu asiye na kitambulisho cha Taifa yaani #NIDA kusajili kampuni au jina la biashara.
Taarifa zilizotolewa hapo juu ni zile za lazima ambazo bila hizo huwezi kumalizia usajili na au usajili unaweza kukawia

Nashauri yafuatayo:
  1. Nashauri kama unataka kusajiliwa kampuni au jina la biashara kwa haraka wasiliana nasi kwa kutumia mawasiliano
  2. Kama huna kitambulisho cha Taifa na umeshaandikisha ili kupata kitambulisho cha Taifa, tembelea ofisi zozote za NIDA karibu na wewe ili wakupe angalau namba yako ya kitambulisho ili uweze kukitumia ukiambatanisha na Kibali cha BRELA ili Kupata Kitambulisho cha NIDA kwa haraka.
  3. Nashauri pia kama bado hujajiandikisha ni vyema ukawahi, hata kupitia kwenye eneo ambalo zoezi linaendelea ili uwahi kwa maana serikali imeanza kuzuia kupata huduma za public kama huna kitambulisho. ambatanisha pia Kibali cha BRELA ili Kupata Kitambulisho cha NIDA kwa haraka.
  4. Mwisho nashauri hizi taarifa zote uwe nazo mkononi kwa sababu huu mfumo wa usajili wa ORS unakupa siku sita (6 days) tu kukamilisha usajili kama baada ya hizo siku bado, taarifa zote zinafutika na itakubidi uanze upya from the scratch.
Kwa wale wanaohitaji kusajiliwa kampuni au jina la biashara chapu chapu tafadhali wasiliana nami kupitia kwenye ukurasa huu wa mawasiliano

Bofya hapa: Hatua 10 Rahisi za Kusajili Kampuni Kupitia Website ya BRELA
 
Kwa wale wanaohitaji kusajiliwa kampuni au jina la biashara chapu chapu tafadhali wasiliana nami kupitia kwenye ukurasa huu wa mawasiliano
Ahsante kwa hili bandiko, Nimehifadhi mawasiliano yako.
 
Attachments

  • kusajiri_Biashara.pdf
    485.6 KB · Views: 256
Sio nchi nzima waliopata vitambulisho vya taifa, kwa hao watu inakuwaje? vitambulisha vya taifa haviandikishwi kila siku je nikitaka kufungua kampuni 2019 ambako pengine zoez la kuandikisha vitambulisho vya taifa litakuwa limekoma hapo inakuwaje mkuu.
 
Wewe uko authorized Na Brela au ni kanjanja tu mjanja mjanja wa mjini?
Mkuu hata kutoa elimu inahitaji authorization ya BRELA au hukupima ulichouliza! Hata hivyo BRELA hawana authorized agents kama ilivyo makampuni ya simu. Wao wanachotaka kampuni au biashara imesajiliwa kwa kufuata sheria na taratibu zao period.
 
Sio nchi nzima waliopata vitambulisho vya taifa, kwa hao watu inakuwaje? vitambulisha vya taifa haviandikishwi kila siku je nikitaka kufungua kampuni 2019 ambako pengine zoez la kuandikisha vitambulisho vya taifa litakuwa limekoma hapo inakuwaje mkuu.
Nimewauliza hilo wakajibu Kitambulisho cha Taifa ni lazima na kama bado kabisa itabidi usubiri tu. Ndio hali halisi
 
Ni ID ya NIDA tu sasa hivi? Ina maana zile za kura hazifanyi kazi tena kwani nchi nzima wameshaandikisha nida? Au ipo namna nyingine pia?
 
Mkuu hata kutoa elimu inahitaji authorization ya BRELA au hukupima ulichouliza! Hata hivyo BRELA hawana authorized agents kama ilivyo makampuni ya simu. Wao wanachotaka kampuni au biashara imesajiliwa kwa kufuata sheria na taratibu zao period.
Tayari umesha Toa elimu sasa hapa chini ulikuwa unamaanisha nini????

Ukabadilisha na rangi kabisa.

Kwa wale wanaohitaji kusajiliwa kampuni au jina la biashara chapu chapu tafadhali wasiliana nami kupitia kwenye ukurasa huu wa mawasiliano
 
Mkuu hata kutoa elimu inahitaji authorization ya BRELA au hukupima ulichouliza! Hata hivyo BRELA hawana authorized agents kama ilivyo makampuni ya simu. Wao wanachotaka kampuni au biashara imesajiliwa kwa kufuata sheria na taratibu zao period.
Tayari umesha Toa elimu sasa hapa chini ulikuwa unamaanisha nini????

Ukabadilisha na rangi kabisa.

Kwa wale wanaohitaji kusajiliwa kampuni au jina la biashara chapu chapu tafadhali wasiliana nami kupitia kwenye ukurasa huu wa mawasiliano
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom