Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Karibu tukusajilie kampuni au jina la biashara online kwa njia mpya ya ORS.
Unatakiwa kuwa na
1. Kitambulisho cha uraia kitolewacho na NIDA
2. Uwe na TIN no itolewayo na TRA

Tutakuandalia Morandum &Articles of association kwa kuzingatia "ISIC CLASSIFICATION" na mengine yote kwa gharama nafuu na kwa haraka na usahihi kabisa kampuni yako itasajiliwa

Vilevile tunatoa huduma mbalimbali kama washauri wa biashara kama vile kufuatilia malipo ya "Annual Returns" za BRELA na uhakiki wa vielelezo vyote vya kampuni yako
Vilevile tunatoa huduma za usajili wa TIN no kuanzia za binafsi, matawi ya kampuni na kampuni, Annual Return of Income kwa TRA
Kwa maelezo, maswali na ushauri waweza kutucheki kwa
Email: consultafrolinktz@gmail.com
Hotline: 0755411455

Karibuni sana
 
Habari zenu..msaada jamani..naombeni kujua hatua za kusajili bidhaa..kupewa kibali cha TFDA na TBS..na je! Inagharimu kiasi gani katika usajili?na ofisi kwa Dar es salaam ziko sehemu gani? Na inachukua mda gani kusajiliwa?na yeyote mwenye kujua wapi nitapata mashine ndogo ya kutengenezea chalk? Na wapi nitapata malighafi za losheni kwa bei nzuri..AHSANTENI
 
Naomba nikujibu katika masuala ya usajili
1. Je umeshasajili jina la biashara yako au kampuni kwa upande wa BRELA?
2. Je umeshasajili TIN no kwa upande wa TRA?
(Tufanye umesajili vyote hivyo vya awali)
Hatua inayofuatia ni
3. Kusajili SIDO ambao wao watakuwa wanakutambulisha katika taasisi unazoomba leseni au kibali kama mjasiriamali wao hivyo kupata huduma kwa urahisi
4. Hii ina maana kupata kibali TBS, ina maana SIDO wataandika barua kwa TBS baada ya wewe kuomba kubali kupitia SIDO juu ya bidhaa yako unayozalisha. TBS watajiridhisha ubora wa bidhaa unayozalisha kwa kuchukua sample, kama ipo vema basi utapata cheti cha ubora. Huduma hii ni BURE kwa wajasiriamali wadogo
5. Ukija TFDA utaandika barua kama mlolongo wa hapo juu ambapo SIDO watakuombea kama mwanachama wao mjasiriamali. Baada ya hapo TFDA watafuata utaratibu wao n wakijiridhisha basi utapata cheti chao. Gharama hii sina uhakika nayo
6. Ofisi za TFDA zipo pale Mabibo External karibu na B. W. MKAPA EPZA Zone na ofisi za TBS zipo pale UBUNGO kati t stendi ya mabasi na kituo cha mafuta cha Oilcom

Mashine ndogo ya kutengeneza chaki nenda SIDO pale Vingunguti/Kiwalani small industries zone

Ukifika SIDO mule ndani hata hizo malighafi utazipata pia kwani kuna harakti nyingi sana za uzalishaji za wajasiriamali

Karibu
Maoni, ushauri na maswali waweza kutucheki ktk

Ahsante..ubarikiwe mno
 
Brela wako wapi?
 
Hallo watalaam wa Biashara mimi ninakampuni nilisajili mwaka jana mwezi wa nne April,2017.
Sina TIN namba. Jumla ya pesa niliyolipa ni 240,000/= mtaji ni mdogo. Nasikia eti hata kama sijafanya biashara natakiwa kulipia mwezi wa nne April, 2018. Kama ni kweli je nalipia kiasi gani ?

Nitashukuru kama mtanidaidia kwa hilo na nadhani itabido nije kupanua mawazo kuhusu kodi nk consultations
 
Hatua za kupata TIN NO ya kampuni.

Kwanza kabisa mkuu unatakiwa kumpata Mshauri wa kodi ambaye moja kati barua 3 utakazoandika kwe!nda TRA itaonyesha hy mshauri wa kodi ndiyo atasimamia masuala yako yote ya kodi na yeye huyu mshauri atasaini kwenye hiyo barua.

Pili, barua zako ya bodi na ya maombi utaambatanisha pamoja na zile fomu mbali mbali za TRA, MEMORANDUM na Cheti ambavyo vinatakiwa viwe "certified" na mwanasheria.

Mwisho, suala la utalipa kiasi gani cha awali haijalishi mtaji kiasi gani, lakini utafanyiwa "assessment" kwanza kwa kuulizwa maswali mbalimbali kuhusiana na biashara. Hapo kiuzoefu wengi ndo huwa wanaumia. Lakini waweza kwenda na mshauri wako wa kodi.

Ina maana yale mapato (income) yako utakayosema kwa mwaka mzima ndiyo utachajiwa kodi hapo. Kingine sio kila biashara lazima ilipe kodi kwani mauzo chini ya mil 4 hulipi kodi hivyo ondoa dhana hiyo
 
Back
Top Bottom