Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Afrolink-Tz Consult Ltd

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2018
Messages
298
Points
1,000

Afrolink-Tz Consult Ltd

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2018
298 1,000
kuna faida gan kujisajili kama kampuni ukilinganisha na kusajili biashara.......kampuni inakuwa na sifa gani hasa
Mkuu maswali yako ni mafupi mafupi lakini ni mapana sana. Nami ntajitahidi kuyajibu kwa upana wake

1. Utangulizi
Kampuni ni asasi au shirika linalohusika kufanya biashara/shughuli nyingi kihalali

2. Aina za kampuni
a) Kampuni binafsi
Ni kampuni yenye ukomo ambayo wamiliki wanawajibika kisheria kwa kiasi cha mtaji walichowekeza tu

b) Kampuni tanzu
Ni kampuni yenye kumiliki nusu ya mali zinazomilikiwa na kampuni nyingine

c) Kampuni ya umma
Hii ni kampuni inayomilikiwa na serikali au inaweza kumilikiwa na serikali pamoja watu binafsi

===>Sifa za kampuni
Sifa za kampuni zinategemea na aina ya kampuni kama nilivyoainisha hapo juu. Sifa hizo ni kama ifuatavyo:
1. Kampuni binafsi
A. Inaundwa na watu wenye uhusiano wa kijamaa kabla. Mf baba na mama, baba na mtoto nk
B. Idadi ya wanahisa waundao kampuni ni kuanzia 2 na mwisho 50
C. Ina ugumu katika kuhamisha hisa hivyo ni ngumu kusajiliwa katika masoko ya hisa

2. Kampuni ya umma
A. Inaundwa na serikali na vilevile makampuni au watu wengine
B. Haina idadi kamili ya wamiliki
C. Ni rahisi kuhamisha hisa hivyo ni rahisi kuisajili soko la hisa

3. Kampuni tanzu
A. Ina umiliki wa kampuni nyingine ambayo inaweza kuwa nje ya Tanzania

===> Faida za kusajili kampuni dhidi ya jina la biashara ni kama ifuatavyo:
1. Mtaji
Mtaji kwa kampuni mnachanga hivyo inategemea uwezo wenu wa kuanza na mtaji kiasi gani na kuongezea kwa kuvhanga zaidi ya mtu watu wawili LAKINI katika suala la jina la biashara mtaji huwa kutoka kwa mmiliki mmoja tu hivyo uongezekaji wa mtaji unakuwa mgumu

2. Hadhi ya kisheria
Kampuni ina hadi kisheria kama asasi inayojitegemea hivyo hata panapotokea jambo basi kampuni ndiyo huhusika kisheria LAKINI jina la biashara jambo lolote humgusa moja kwa moja mmiliki wa jina la biashara

3. Huduma za kifedha
Kupata msaada wa huduma za kifedha kama mikopo kuendesha shughuli/biashara/miradi ni rahisi kupitia kampuni kwa sababu inasimama kama asasi yenye kujitegemea LAKINI katika jina la biashara unakopa binafsi hivyo kuna ugumu au kuna kuwa na kiwango cha msaada wa kifedha

4. Gharama za uendeshaji
Kampuni ina gharama mbalimbali za uendeshaji. Hii inatokana na kuwa na mfumo kamili wa kiutendaji ambao utahitaji kuwa na watendaji wengi kadiri inavyozidi kukua LAKINI jina la biashara ina maana waweza kila jambo kusimamia wewe binafsi

5. Uwasilishaji wa mahesabu
Kampuni inawajibika kuwasilisha mahesabu yaliyokaguliwa na mkaguzi wa hesabu kwa taasisi mbali mbali kama vile TRA katika kulipa kodi nk LAKINI jina la biashara unakadiriwa katika gharama kama kodi nk

6. Uwezekano wa kuendelea kwa kampuni kuwepo katika shughuki zake ni mkubwa hata mmiliki/wamiliki wakifa kutokana na muundo na asili ya utendaji kazi wake LAKINI jina la biashara kuna uwezekano wa kufa kwa biashara baada ya mmiliki kufa kutokana na kila jambo kuwa la mmiliki tu

7. Tenda, kazi nk
Kampuni ina nafasi kubwa sana ya kupata mfano tenda au kazi inapoomba kama kampuni kuliko jina la biashara. Hii inatokana na masuala kama umiliki katika mtazamo wa kisheria nk

Hizi ni baadhi tu.
 

Afrolink-Tz Consult Ltd

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2018
Messages
298
Points
1,000

Afrolink-Tz Consult Ltd

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2018
298 1,000
Kwani njia isiyo ya mtandao, yaani kusubmit katiba brela haipo tena au ndo mpaka mtandandaoni tu?
Kwa sasa njia ni moja tu ya mtandao. Ambapo inabidi uwe na akaunt ya "ORS". Akaunti hii utafungua kwa kutakiwa kuwa na kitambulisho cha Taifa (Driving licence, passport, voting id havikubaliki)
Vilevile katiba yako uandae inayoendana na katiba ya mule ktk mtandao ie ISIC. Na mambo mengine
Karibu
 

Afrolink-Tz Consult Ltd

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2018
Messages
298
Points
1,000

Afrolink-Tz Consult Ltd

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2018
298 1,000
Nahitaji nina issue brela very urgent naomba mawasiliano ya mtu aliyeko pale anisaidie issue yangu
Ingia kwenye website yao, halafu nenda online registration, namba zao utazipata zote katika ukurasa.
Karibu
Business| Auditing| Tax| Logistics consultancy firm
 

lembu

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2009
Messages
3,681
Points
2,000

lembu

JF-Expert Member
Joined Dec 31, 2009
3,681 2,000
UTANGULIZI
Kuanzia tarehe 1 Februari 2018 #BRELA ilitangaza kuanza kutumika kwa mfumo wake wa kuwawezesha wamiliki wa makampuni kusajili na kuwasilisha returns BRELA. Pia BRELA ilishatangaza kwamba mnamo tarehe 25 Machi 2018 mfumo wake wa awali wa OBRS uliokuwa unaruhusu kusajili jina la biashara na kufanya clearance ya jina la kampuni kupitia website ungefungwa rasmi ili kuuruhusu mfumo mpya wa ORS wenye uwezo wa kusajili majina ya biashara na makampuni kufanya kazi rasmi.

Hatua 10 za kufuata ili kusajili kampuni imeelezwa hapa chini, tafadhali fuatilia.

Kwa wale wanaohitaji kusajiliwa kampuni au jina la biashara chapu chapu tafadhali wasiliana nami kupitia kwenye ukurasa huu wa mawasiliano

HATUA 10 ZA USAJILI
Hatua #1: Taarifa za msajili
Ili kutumia mfumo huu mpya wa ORS mteja (msajili) anayetaka kusajili jina la kampuni anatakiwa kuwa na taarifa za msajili (msajili anaweza kuwa ni mmoja wa wakurugenzi, Katibu au Wanachama/Wenye hisa wa Kampuni tarajiwa).

Taarifa zenyewe ni:-
 1. Kitambulisho cha Taifa kwa wenyeji na Passport kwa wageni
 2. Simu ya kiganjani
 3. Barua pepe yaani email
Hatua #2: Taarifa za kampuni
Taarifa za kampuni zinazotakiwa ni:-
 1. Aina ya kampuni kama ni ya hisa au isiyo na hisa, ya binafsi au ya uma nk
 2. Jina la kampuni
 3. Tarehe ya kufunga mahesabu - mfano 31 Desemba
 4. Kumbuka: TIN No., Namba ya usajili zitawekwa na mfumo automatically
Hatua #3: Ofisi za kampuni
Taarifa za ilipo au itakapokuwa ofisi za kampuni ambazo ni:-
 1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
 2. Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
 3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namaba ya kiwanja, kitalu na nyumba,
 4. Sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
Hatua #4: Shughuli za Kampuni
Hatua #5: Taarifa za wakurugenzi
Taarifa zinazotakiwa za Wakurugenzi ni:-
 1. Aina ya mkurugenzi kama ni mtu au taasisi
 2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
 3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
 4. TIN
 5. Simu ya kiganjani
 6. Barua pepe yaani email
 7. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
  1. Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
   1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
   2. Kama halijapimwa tayarisha anuanii ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
   3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namaba ya kiwanja, kitalu na nyumba,
 8. Simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
Hatua #6: Taarifa za katibu wa kampuni
Taarifa za katibu wa kampuni (company secretary) zinazotakiwa ni:-
 1. Aina ya mtu kama ni mtu asili au taasisi
 2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
 3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
 4. Simu
 5. Barua pepe - email
 6. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
  1. Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
   1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
   2. Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
   3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, kitalu na nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
 7. Simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email na (sanduku la posta kwa ajili ya memart)
Hatua #7: Taarifa za wanachama/wenye hisa
Taarifa za wanachama au wenye hisa zinazotakiwa ni:-
 1. Aina ya mtu kama ni mtu au taasisi
 2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
 3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
 4. Simu
 5. Barua pepe - email
 6. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
  1. Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
   1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
   2. Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
   3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya
Hatua #8: Viambatanisho (Attachments in PDF)
Viambatanisho vinavyotakiwa kuambatanisha kwenye maombi (zote katika pdf) ni:-
 1. Memorandum and articles of association iliyosainiwa na wanachama/wenye hisa pamoja na mwanasheria wa uma (Notary Public)
 2. Form 14b iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi na mwanasheria wa uma (Notary Public)
 3. Ethics and Integrity Forms iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi
 4. Company consolidated form iliyosainiwa wakurugenzi wote na katibu wa kampuni
Hatua #9: Ada za usajili na kufaili (Different Fees)
Aina za ada ni kama ilivyoonyeshwa hapa chini
 1. Kusajili kampuni
 2. Kuhifadhi nyaraka na
 3. Stamp Duty
Hatua #10: Namna ya kulipa ada (Payment Methods)
Malipo ya ada yanafanyika kwa njia kuu tatu ambazo ni
 1. Kuweka Benki: Kwa njia y kuweka Fedha kwenye Tawi la Benki /Wakala wa Benki
  Nenda kwenye Tawi lolote la Benki / Wakala wa Benki ya CRDB /NMB kwa kutumia Namba ya Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
 2. Kwa njia ya Simu ya Mkononi: Tumia mtandao wa simu wa AirTell Money / Tigopesa/ MPesa/ HalloPesa kwa kuweka namba ya Kampuni 888999 na Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
 3. Kwa njia ya Kuhamisha Fedha: Unaweza kuhamisha Fedha moja kwa moja kutoka katika Benki yoyote kwenda kwenye Akaunti zetu zilizoko katika Benki ya NMB/ CRDB kwa njia ya TISS /SWIFT kwa kujaza: Namba ya Akaunti na Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
Kumbuka: Utaratibu wa malipo aidha kwa simu au benki utapewa ukishafikia hatua husika ya malipo

Soma zaidi kuhusu jinsi ya kufanya malipo BRELA Kupitia Simu Yako

HITIMISHO NA USHAURI
Brela sasa hivi hawataki usajili kwa njia ya zamani, yaani kupeleka makaratasi ngumu na kusubiri mlangoni kwa siku 6. Pia BRELA hawakubali mtu asiye na kitambulisho cha Taifa yaani #NIDA kusajili kampuni au jina la biashara.
Taarifa zilizotolewa hapo juu ni zile za lazima ambazo bila hizo huwezi kumalizia usajili na au usajili unaweza kukawia

Nashauri yafuatayo:
 1. Nashauri kama unataka kusajiliwa kampuni au jina la biashara kwa haraka wasiliana nasi kwa kutumia mawasiliano
 2. Kama huna kitambulisho cha Taifa na umeshaandikisha ili kupata kitambulisho cha Taifa, tembelea ofisi zozote za NIDA karibu na wewe ili wakupe angalau namba yako ya kitambulisho ili uweze kukitumia ukiambatanisha na Kibali cha BRELA ili Kupata Kitambulisho cha NIDA kwa haraka.
 3. Nashauri pia kama bado hujajiandikisha ni vyema ukawahi, hata kupitia kwenye eneo ambalo zoezi linaendelea ili uwahi kwa maana serikali imeanza kuzuia kupata huduma za public kama huna kitambulisho. ambatanisha pia Kibali cha BRELA ili Kupata Kitambulisho cha NIDA kwa haraka.
 4. Mwisho nashauri hizi taarifa zote uwe nazo mkononi kwa sababu huu mfumo wa usajili wa ORS unakupa siku sita (6 days) tu kukamilisha usajili kama baada ya hizo siku bado, taarifa zote zinafutika na itakubidi uanze upya from the scratch.
Kwa wale wanaohitaji kusajiliwa kampuni au jina la biashara chapu chapu tafadhali wasiliana nami kupitia kwenye ukurasa huu wa mawasiliano

Bofya hapa: Hatua 10 Rahisi za Kusajili Jina la Biashara Kupitia Website ya BRELA
 

kcamp

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2014
Messages
5,651
Points
2,000

kcamp

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2014
5,651 2,000
Inamaana baada ya kua aproved alaf sjafanya ORS ndan ya siku sita nitakua nmepoteza info zote za kule obrs?
 

Forum statistics

Threads 1,389,869
Members 528,040
Posts 34,036,802
Top