Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Msaada wa haraka wadau, ninataka kuanza biashara, ila sina kitambulisho cha kura wala cha taifa ( vilipotea),
Je inawezekana kuanza biashara yaani kupata namba ya mlipakodi na leseni bila kuwa na jina la biashara? Maana ili kusajili jina la biashara vinatakiwa vitambulisho, na mim hivyo sina, msaada tafadhali!
Unaweza kuanza biashara kwa kutumia jina lako na ukapata TIN na leseni... Kama hauna ulazima sana basi tumia tu majina yako bila kusajili jina la biashara
 
1. Kwanza chagua jina halafu nenda Brela kasajili jina. It's a one day process.

2. Baada ya kupata 'OK' ya jina. Nenda kwa mwanasheria akuandalie documents mbili muhimu. Hii ni The Memorandum of the Company na Articles of Association copy nne nne. This is a Two days Job.

3. Unarudi Brella na kujaza forms na ku-submit na hizo documents na unalipia - applicable fees. This is another two days job.

In total 5 working days zinatosha kusajili kampuni. Ukianza Jumatatu, unamaliza Ijumaa. Kama una mkono mrefu, unaweza kufanyiwa kwa Fast Track na ukamaliza mambo yote in a day or two.
Kusajili ni mpaka Dar tu? kwani hakuna ofisi za kanda kama kati, nyanda za juu kusini, magharibi na ziwa? Tafadhali naomba kujuzwa!
 
Habari members
Nina shida na majibu ya haya maswali,naomba kujibiwa
nataka kufanya biashara flani ambayo inafanyika online au saa nyingine unamfuata mteja alipo unampa huduma hiyo anakulipa.sasa naomba kujua

1- naweza kufungua kampuni ya hii biashara? Bila kuwa na ofisi maalumu? Yaan ofisi ni mimi mwenyewe na msaidizi wangu

2- je hata kama mtaji wangu ni chini ya laki tano (500,000) tsh naweza kufungulia kampuni biashara hii?

3- je mambo ya kodi yanaendaje kulingana na biashara yangu ilivyo ndogo japo nategemea baada ya miaka kadhaa itakuwa na kumiliki ofisi pia

4- je gharama za kufanya utaratibu wote kabisa mpaka unakabidhiwa cheti cha kampuni yako jumla ni sh ngapi ili nijipange?

NB: Nataka kufungua kampuni katika stage hii kwa sababu kwa ninavopanga naona baadae naweza kuomba tenda nikiwa kama kampuni ,kwa hiyo naona niwe na kampuni yangu japo haina ofisi ni mimi na simu yangu tu!!

Nawasilisha
 
Naomba nikujibu maswali yako kama ifuatavyo
1. Kufngua kampuni
Limited company inafunguliwa kwa kuwa na Memorandum na Articles of Association. Ss katika Memorandum hapo utaona ofisi za kampuni zinasajiliwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini eneo la ofisi hata nyumbani kwako waweza kuweka ndipo ilipo ofisi ya kampuni yako. Mfano Unakaa Ilala, mtaa wa Lindi, barabara ya Shaurimoyo, plot no 1, block b nk.
2. Mtaji wa laki 5
Kampuni inaanza kusajiliwa kuanzia na kiasi cha chini cha mtaji wa sh elfu 20 hivyo hiyo laki 5 ni kubwa sana
3. Masuala ya kodi
Kodi inategemea na kiasi gani kwa mwaka kinapatikana kwa sababu si kila biashara inafuzu kulipa kodi. Mauzo yasiyozidi mil 4 kwa mwaka haulipi kodi. Rejea TRA kodi na ushuru mbalimbali 2017/2018, chapa ya Julai 2017 ukurasa wa 9, jedwali sehemu no 2.
4. Gharama za usajili
Gharama za usajili inategemea na thamani ya mtaji kwa upande wa malipo ya BRELA na vlvl kuna gharama za consultant. Kwa mujibu wa mtaji usemao kwa haraka haraka ni 177,200/=. Then gharama za consultant inategemea kwani hazipo fixed lakini kwetu ukija tutaongea. Mawasiliano ntaweka chini
Karibu
I-Business Consult ltd
Mobile:0659211222/0777777766
Email:iconsultbuzness@gmail.com
 
Da! Asante sana mkuu! Short and clear nimekuelewa!!! Ntakutafuta nipe mda niweke sawa mambo
 
Nimeona watu wakiorodhesha shughuli nyingi zitakazofanywa chini ya kampuni moja na wengine wanakuwa specific na aina fulani tu ya shughuli ningependa kujua labda kuna gharama tofauti kati ya gharama za kuwa na kampuni yenye shughuli nyingi ndani yake lakini sio zote zinafanyika na ile yenye shughuli moja au mbili? Na vipi kwenye suala zima la kulipia mapato TRA kwenye kampuni yenye shughuli nyingi na ile yenye shughuli labda moja tu?
Ni kweli nahitaji kufungua kampuni lakini before nahitaji kufahamu juu ya mambo hayo mawili.
Mkuu naomba kuchangia kama ifuatavyo
Katika usajili wa kampuni ambayo ni limited by shares kuna Memorandum of Association na Articles od Association (Memorandum and Articles of Association) . Ss katika hiyo Memorandum unaweza kuorodhesha biashara mbali mbali ambazo unafanya na unaweza kufanya baadae. Gharama za usajili kwa upande wa BRELA haijalishi umeandika biashara ngapi bali utachajiwa kutokana na mtaji 'capital' ya kampuni yako
Ukija upande wa TRA utalipa kodi kutokana na biashara au shughuli unayofanya. Maana yake kama una biashara moja basi hiyo biashara ndiyo itakayohusika kulipa kodi na kama una biashara zaidi ya moja kila biashara itafanyiwa ukaguzi na kukadiriwa kiasi stahiki
Lakini kumbuka ya kwamba limited coy huwa unatakiwa uandae mahesabu yaliyokaguliwa na kuhakikiwa na auditor na kukabidhi TRA
 
Ndugu wana JF naomba mwenye taarifa za taratibu za kusajili kampuni ya kutengeneza furniture hapa kwetu Tanzania, anijuze .
-shukrani.
 
Ndugu wana JF naomba mwenye taarifa za taratibu za kusajili kampuni ya kutengeneza furniture hapa kwetu Tanzania, anijuze .
-shukrani.
Mkuu
Kwanza unatakiwa kubuni jina ambalo halifanani na jina la kampuni nyingine. Waweza kujaribu kufanya official search( njia hii ni gharama ya sh 20,000-BRELA FEES).
Ukipata jina then unatakiwa kuandaa MEMORANDUM and ARTICLES OF ASSOCIATION (unaweza kuwaona wanasheria au business consultants kukuandalia). Baada ya hapo utapeleka BRELA. LAKINI MFUMO UMEBADILISHWA
ANGALIZO
Njia hii ilikuwa kabla ya Tangazo la tarehe 23.01.2018 ambapo usajili utafanyika online katika mfumo wa ORS. Hivyo nakushauri kumpata Business Consultant ambapo kuna gharama vilevile za kumlipa
Suala la biashara yako itakuwa imeainishwa katika MEMORANDUM. Na ktk njia ya ORS utachagua biashara utakayo kufanya pia

Karibu I-Business Consult
Mobile: 0659211222/0777777766
Email: iconsultbuzness@gmail.com
f7c86b83ac7a851b49ee479b6a426641.jpg
 
Back
Top Bottom