Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

ZINGATIA HAYA UNAPOTAKA KUSAJILI KAMPUNI
1. Jina.
Unapotafuta jina jitahidi jina liwe linatamkika kirahisi ili isikusumbue katika marketing lakini kikubwa ni maana ya jina. Kuna maneno mengine ni matusi kwa lugha nyingine, hivyo jitahidi sana kufanya utafiti wa kina wa jina hilo.
2. Mtaji:
Maamuzi ya mtaji kiasi gani kiandikishwe ni ni jambo la msingi sana. Wengi hupenda kuweka mtaji mdogo ili kupunguza gharama za usajili na kodi, vema, lakini hicho kisiwe kigezo mama cha kukuamulia mtaji uwe kiasi gani. Tambua kwamba mtaji unawakilisha ukomo wa kuwajibika kwa kampuni katika wajibu wake.
3. Wanahisa:
Wanahisa mnatakiwa kuwa watu mnaofahamiana vema, wenye mrengo unaofanana na mnaelewana. Tofauti na hilo itasababisha kuchelewa kwa maamuzi muda wote na kuhatarisha ustawi wa biashara.
4. Uandishi wa katiba:
Ni hatari kutegemea mtu yeyote asiye na utaalam wala ujuzi wa kuandika katiba akuandikie. Kibaya zaidi wengine huandika wao wenyewe hata kama hana utaalam na uzoefu huo. Hata kwa wanasheria, si kila mwanasheria anaweza kukuandikia katiba iliyo standard.
Kitu kibaya zaidi watu hudhani kwamba unaweza kuchukua katiba yoyote na kubadili majina tu kisha ukaendelea na usajili. Hawaangalii mpangilio wa maneno na malengo, hawazingatii kama katiba ina vipengele vya kuruhusu mambo Fulani Fulani kufanyiwa mabadiliko,
Hawazingatii ni namna gani founders wanalindwa na katiba, na mengine mengi. Hivyo unashauriwa kuwatumia wataalam wenye uzoefu kufanya kazi hiyo.
Kwa huduma za uhakika na weledi katika masuala hayo yote, waone essence consult company limited.
Pia tunatoa usaidizi katika kusajili NGO, Huduma za kihasibu, kuandika michanganuo ya biashara, na usaidizi kwa wale wanaotaka kuanzisha taasisi za mikopo n.k Wasiliana nasi kwa namba 0768597186 au email
doricelucas21@gmail.com
Mkuu in mtaji kiasi gani angarau unafaa kuanzisha Microcredit company
 
Mtaji wa chini ni Milioni Moja, ila sikushauri usitumie mtaji huu,anzia hata na Million ,japo unaweza aza na mtaji mdogo baadae ukaongeza ,lakini memorandum and articles ya awali haitabadilika ila uta file special resolution pamoja na form ya kuongeza mtaji,kwa hiyo kujua au kuthibisha kwamba mtaji umeongezeka itakuwa kwa majibu ya barua ya official search inayotoka kwa msajili
Sole propiator ama businessname inasajiliwa kwa hela ndogo,hausishi kuandaa memorandum and articles ambayo kama mtaalam atakuandalia itabidi umlipe, pia huwasilisha mahesabu ya kila mwaka TRA yanayoandaliwa na muhasibu Faida za limited ni kwamba unaweza fanya shughuli mbalimbali kwa company moja ilimradi objectives zimeainishwa kwenye memorandum,pia kuna baadhi ya biashara ambayo huwezi kufanya bila kuwa limited company,company inahusika kama yenyewe kwa sababu company is legal person hivyo hata kama ni kufilisi zinafilisiwa mali za company na si za mtu ambazo hazija orodheshwa kama ni za company,pia hata kama ni mahakamani company inaweza mtumia mwanasheria kuiwakilisha wakati kwenye sole propriatorship mwenye biashara ndiyo huhusika zaidi.

Zaidi ya wapo kuna wataalam wengine humu wataongozea
Habari mkuu Singo na wataalum wengine ninaomba kufahamu business arrangement nzuri kama ninataka kuanzisha kiwanda kidogo cha product 1 mkoa A na kiwanda kidogo kingine cha product 2 mkoa B.

Lakini pia ninataka kuanzisha Sales stores mkoa C, mkoa D na mkoa E. Hizi sales stores ninataja ziuze product zangu na related products za manufacturers wengine.

Je ni business arrangement gani inaweza kuleta ufanisi in terms of management, revenue,cost control, profitability na tax liability.
•Sole propieter or limited company?
•One business entity or a number of entities?

Ninatanguliza shukran
 
Habari mkuu Singo na wataalum wengine ninaomba kufahamu business arrangement nzuri kama ninataka kuanzisha kiwanda kidogo cha product 1 mkoa A na kiwanda kidogo kingine cha product 2 mkoa B.

Lakini pia ninataka kuanzisha Sales stores mkoa C, mkoa D na mkoa E. Hizi sales stores ninataja ziuze product zangu na related products za manufacturers wengine.

Je ni business arrangement gani inaweza kuleta ufanisi in terms of management, revenue,cost control, profitability na tax liability.
•Sole propieter or limited company?
•One business entity or a number of entities?

Ninatanguliza shukran
Itafaa usajili Limited company ambayo ita ainisha shghuli zote za company.Hapo utakuwa na Uhuru wa kufanya biashara popote,Ila utatakiwa kuwa na leseni ya biashara na branch TIN kwa kila mkoa utakokuwa na hayo maduka au huduma.

Sole proprietorship haitafaa kwa sababu eneo la ilipo biashara huandikwa kwenye Extract from registrar ambayo hutolewa pamoja na Certificate of registration,hivyo hutoweza kutumia hiyo business name kupatia leseni za biashara mikoa tofauti tofauti.

Ila limited company inaweza miliki majina ya biashara zaidi ya moja ambazo zinafanyika maeneo tofauti tofauti na biashara tofauti tofauti.
 
Gharama halisi n Tsh ngap ..?
Mtaji wa mil 1 ni 177,200
Mtaji zaidi ya mil 1- 5 ni 267,200
Mtaji zaidi ya mil 5 - 20 ni 357,200
Mtaji zaidi ya mil 20- 50 ni 387,200
Mtaji zaidi ya mil 50 ni 532,200
NB hizo ni gharama za usajili wa limited company ynye mtaji na shares na zinajumuisha registration fee,filling fee na stampduty
 
ahsante mkuu
Hv mtaji ukiongezeka itabidi ulakafanye tena usajiri..?
Utawajulisha kwa kutumia special resolution ,kisha utafanyiwa assessment na kulipia kadri ya assessment itakavyokuwa.

Memorandum haibadiliki ukiongeza mtaji.

Baada ya kuongeza mtaji majibu ya kwamba mtaji umeongezeka yatapatikana kwa kuomba barua ya official search.
 
Mkuu ni rahisi tu
Hatua ya kwanza ni kujisajiri kwa kufungua akaunti na Brela katika mfumo wa online ie. OBRS!
Baada ya kuwa na akaunti utaenda katika menu ambayo utachagua aina gani ya usajili utakao kama individual, partnership, company nk
Utapendekeza jina kipekee ambalo biashara/kampuni yako iitwe
Kwa Maelezo zaidi tembelea website ya brela
Kwa msaada usisite kutucheki au kuwasiliana katika barua pepe I consultbuzness@gmail.com
Karibu

Sent from my HUAWEI Y330-U11 using JamiiForums mobile app
Mkuu nimechasajili jina na limekuwa approves. Nafanyaje ili nipate certificate ya kuonyesha jina limesajiliwa.
 
Itafaa usajili Limited company ambayo ita ainisha shghuli zote za company.Hapo utakuwa na Uhuru wa kufanya biashara popote,Ila utatakiwa kuwa na leseni ya biashara na branch TIN kwa kila mkoa utakokuwa na hayo maduka au huduma.

Sole proprietorship haitafaa kwa sababu eneo la ilipo biashara huandikwa kwenye Extract from registrar ambayo hutolewa pamoja na Certificate of registration,hivyo hutoweza kutumia hiyo business name kupatia leseni za biashara mikoa tofauti tofauti.

Ila limited company inaweza miliki majina ya biashara zaidi ya moja ambazo zinafanyika maeneo tofauti tofauti na biashara tofauti tofauti.
Nimeelewa maana ya neno Limited
 
Habari wapendwa, ninaomba kwa mtu anayefanamu au anayeweza nisaidia kusajiri kampuni anielekeze tafadhali, nahitaji kufungua kampuni ya software ila sijajua utaratibu wa kusajiri ukoje, please mwenye mawazo mazuri tusaidiane.
 
1.Hapo ni kumuona Mwanasheria akuandalie Memarts(Memorandum and articles of association)...halafu gharama za usajili Brela zitategemea mtaji(capital) wa kampuni ni kiasi gani, pia kuna gharama za filing fees, stamp duty..gharama zote za Brela utajua baada ya kufanyiwa assessment na unalipia..na ku-file nyaraka zako.

Zikiwa successful basi kampuni itasajiliwa na tapewa hati ya usajili na utaweza kuanza kuendesha kampuni. Hii ni baada ya kujaza fomu za uadilifu(integrity) na kuweka muhuri wa kampuni yako kwenye fomu hiyo.

Hatua zote nilizoeleza hapo zinatanguliwa na stage ya name clearence..hatua hii imelenga kupata jina la kampuni na kuangalia kama halifanani na majina mengine yaliyokwisha sajiliwa. Nayo hufanyika Brela, physicaly au online.

2. Baada ya Brela unaenda TRA kwa ajili ya kuipatia kampuni utambulisho wa kulipa kodi ambako directors nao watahitajika kupata utambulisho wa kulipa Kodi...baada ya makadirio na kulipa utapewa Tax clearence ambayo itakuwezesha kupata Leseni ya biashara katika halmashauri uliyopo.

3. Kama biashara yako itahitaji leseni/compliance certificates za mamlaka nyinginezo za usimamizi basi utahitajika kufika huko na kupata leseni zao eg TCRA, OSHA,

4. Baada ya hapo basi utakuwa umekamilisha taratibu za usajili wa kampuni na post incorporation requirements. Kampuni litaanza kazi.

5. End.
 
Back
Top Bottom