Jinsi ya kurudisha makato ya mshahara toka TRA!

Mahorii

Member
Jan 26, 2014
71
69
Habarini ndugu na marafiki. Namatumaini wote ni wazima wa Afya. Poleni sana na majukumu na mapambano dhidi ya janga la Korona. Leo nilipokea simu toka kwa Rafiki yangu akilalamika biashara imekuwa ngumu sana, pia kujumlisha na ushuru wa TRA, mambo yamekuwa magumu.

Kutokana na mazungumzo naye, nimeamua kujikita kwa mwaka mzima 2021, kuelemisha watu kwenye maswala ya Tax, hususani jinsi au namna ya kupunguza ushuru. Nitajikita sana kwenye ushuru wa mtu na kampuni kwa ujumla. Pia nitakuwa naonesha mianya ambayo watu wanaweza kutumia kukwepa kodi, madhumuni ni kuweka chachu kwa taasisi usika kufanyia kazi hiyo miyanya.

Kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu, sheria ya usimamizi wa ushuru, 2015, sehemu ya 73, imempa ofisa wa TRA uwezo wa kurudishia makato yaliyo zidi wakati ukipokea mshahara wako. Hii inaweza kusababishwa na mabadiliko kwenye mshahara. Kwa mfano, Juma, mwalimu wa shule ya msingi, alikuwa analipwa Tshs 600,000 kwa mwezi(Gross pay) kuanzia January paka June. kama ikatokea, Juma kupunguzwa mshahara na kuanza kulipwa Tshs 400,000 kila mwezi kuanzia July paka December, hii inaweza kupelekea Juma kupata “tax refund”.

Pia kifungu, kinatoa mwogozo wa mhusika kulipwa makato yalio zidi Pamoja na “Interest”.



Formula: Unatakiwa kujua ni kiasi gani umelipwa kwa mwaka mzima. Unaweza kupata hizi number kutoka kwenye “Pay slip”. Hii ni Gross pay, ambayo inajumlisha basic pay na malipo ya ziada kama nyumba, simu..nk

Kwa mfano, Kama umefanya kazi miezi 12 na jumla ya mshahara wako ni GROS PAY Tshs 9,000,000/=
Kwa mwezi itakuwa ni Tshs 750,000/= (9,000,000/12)
= (750,000-520,000) =230,000
=230,000*20% + 22,500*
=Tshs 68,500/=
= 68500 * 12miezi = Tshs 822,000

Hii inamaanisha ulitakiwa kulipa Tshs 822,000 kama ushuru kwa mapato yako ya Tshs 9,000,000.

*Angalia attachment ya picha.

Hatua ya pili, nikujaribu kuangalia kama kuna makato ya ziada. Hapa utatakiwa kujua ni kiasi gani umelipa ushuru ndani ya hiyo miezi 12 au kwa mshahara wa Tshs 9,000,000/=. Utapata hizi number kutoka kwenye “Pay slip”.
Kwa mfano, baada ya kujumlisha ushuru toka kwenye pay slips za miezi 12 na kupata jumla ya Tshs 940,240/=

Kiasi kilicho zidi ni 940,240 - 822,000 =Tshs 118,240

Hichi ndio kiasi ambacho unaweza kurejeshewa kutoka TRA mwisho wa mwaka.

**Huu ni mfano rahisi. Kwa wale watu ambao huwa wanapokea mishahara Tanzania na nchi za nje, au watu wanao fanya investments kwenye shares, itakuwa ni complex kidogo. Ninaweza kuelezea kwa undani kama kutakuwa na maombi au ulazima.

Unaweza uliza swali lolote hapa au PM
 

Attachments

  • Untitled.png
    Untitled.png
    99.6 KB · Views: 7
Naomba uelezee jinsi gani naweza kurudisha pesa niliyotumia kununua EFD machine.
 
Tax returns na tax refund ni same thing??
Ni kitu kimoja. Unapo fanya tax returns, mwisho utapata tax refund au tax payable. Nadhani kwa nchi kama US na nchi za ulaya wanatumia sana neno kama "Tax refund" kwa sababu mara nyingi watu huwa wanapata tax refund/receivable na sio tax payable.
 
Naomba uelezee jinsi gani naweza kurudisha pesa niliyotumia kununua EFD machine.
Hi ndugu,
Unaweza kurudisha pesa yako yote uliyo tumia kununulia machine yako ya EFD kwa asilimia 100%. Pesa uliyotumia kununulia machine ni full deductable, kwahiyo unaweza kutumia gharama uliyo lipia machine kupunguza ushuru wa mapato. Pesa yako itakuwa inarudi kupitia "punguzo la kodi" na sio Pesa kama Pesa.

Kuweza kupata hii faida ya kurudisha hii gharama ya machine na vitu vingine ulivyo nunua, itakubidi uwe unatunza mahesabu.kama hauna system ya kutunza mahesabu yako itakuwa vigumu mno.
Unaweza kuuliza kama bado utakuwa na swali.
 
Back
Top Bottom