SoC03 Jinsi ya kupunguza/ kujiondolea stress haraka ili upate amani na furaha

Stories of Change - 2023 Competition

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
670
Na mimi huwa natumia hizi njia kama naona nna mawazo sana. Kwaiyo nawe zinaweza kukusaidia.

Stress huanzia pale unapokubali kuendeshwa na mawazo yanayokujia.

Bongo zetu ni mashine za mawazo, bila kujali ni mazuri au mabaya. Yenyewe inachapisha tu.

Sasa pale ubongo unapochapisha mawazo mabaya kutokana na uzoefu ulionao/ stori ulizosikia ndo mwanzo wa kuwa na wasiwasi, na mawazo mengi juu ya hicho kitu.

Muda mwingine hadi unakosa usingizi, hamu ya kula inaisha yote, hamu ya sex inapotea kabisa, hutaki ukaribu na watu unaona wanakuongezea stress tu, kiufupi unakua kitu usichotaka.

Stress zipo, ila kinachojalisha ni nini unafanya baada ya kuwa na stress. Hicho ndo kitaamua uendelee kuwa na stress au urudi katika hali ya kawaida.

Na ujue hakuna mwenye uzoefu na stress. kila siku ni mpya na ina mawazo tofauti.

kwaiyo stress itakupata tu, ila kinachojalisha ni nini unafanya baada ya kupata stress.

Pombe, sigara, bangi na ngono zinapunguza stress, lakini hazina matokeo ya muda mrefu. Yatakufanya uwe mtumwa tu wa ivo vitu.

Lakini haukuumbwa kuteseka na stress, fata hatua hizi kujipunguzia stress;

- Kuwa Mtu wa Shukrani.
Stress nyingi huwa zinatokana na kukumbuka vitu vya nyuma au kuwaza sana huko mbeleni itakuaje.

Mwingine anawaza madeni yatamuua, mwingine anajuta kwanini hakufanya kitu fulani huko nyuma. Na mengine mengi, ambayo yanakufanya hadi unakosa usingizi.

Hatua ya kwanza, hata kabla hujaomba, shukuru Mungu.
Jifunze kuwa na shukrani.

Tembea barabarani, mwambie Mungu asante leo nimeamka tena, sema asante nyingi moyoni kadri uwezavyo.

Na akilini mwako usiruhusu wazo jingine lolote zaidi ya nashukuru.

Wazo lingine likikujia, sema asante kwa kuwa nina uwezo wa kufikiri kisha urudi kusema asante.

Na uwashukuru watu ulionao karibu. Watu waliokusaidia kwa namna moja au nyingine. Ikiwezekana tenga siku ya kuwaambia watu asante.

Hata mtu akikukasirisha sema asante kwa kuwa amenionesha sura yake ya tofauti. Au asante kwa kuwa amenionesha jinsi alivyo nami nilivyo.

…Mana mtu unayeongea naye mmefanana/ mnaendana kwa namna moja au nyingine ndo mana mnaongea.

Ukifanikisha hili utajiondolea mawazo kwa asilimia kubwa sana. Utapata unafuu sana.
Kwa kuwa wazo pekee unaloliruhusu kichwani mwako ni wazo la shukrani.

Na siku zote shukrani huwa zina hisia nzuri.

- Rudi Mwanzo.
Kurudi mwanzo namaanisha, rudi kwenye malengo yako. Rudi kwenye kujua ni kitu gani unataka.

Wengi huwa tunaenda tu, bila kujua ni kitu gani hasa tunataka maishani. Yani hatuna mwelekeo. Hiki huwa kinasababisha sana stress.

Ndo mana tunashikwa na stress mbalimbali zisizotuhusu. Jitahidi uwe na mwelekeo.

Jiulize, ni kitu gani hasa unataka? Ni hatua gani hasa unatamani ufike? Ni kitu gani hasa unataka ufanye na maisha yako?

Ukishajibu hayo, utagundua unachokiwaza hakikupeleki huko unakotaka kwenda. Aitha yanakuogopesha au yanakurudisha nyuma.

Sasa ni muda wa kubadili mtazamo na jinsi unavyofikiri. Ni kitu kidogo sana unatakiwa ubadilishe. Mtazamo.

Mfano, una mawazo juu ya madeni uliyonayo, na yanakuumiza kweli.
Lakini unachokitaka ni kuwa huru na kujitegemea mwenyewe.

Unachotakiwa kubadilisha ni mawazo, kutoka, haya madeni yananiumiza kwenda, najitegemea na nipo huru mwenyewe.

Yani waza kile unachohitaji tu, wazo jingine likija libadilishe kuweka wazo la kile unachotaka. Na uamini unaweza kipata.

Hata kama sio kweli kwa sasa, lakini kumbuka kuna nguvu kubwa zaidi yako itakayo kusaidia. Kwanini usiiruhusu ikusaidie?

Hiyo ndo maana ya imani. Hiyo ndo imani tunayofundishwa tuwe nayo.

Faida ya wazo kama hilo ni kwamba utapunguza kuwaza jinsi unavyoteseka, au utakavyokufa. Badala yake mawazo yako yanahamia kwenye kutafuta njia za kuwa huru na kujitegemea. Utajikuta unatafuta njia ya kumaliza matatizo yako.

Tofauti na kwa sasa ambapo unajikuta unafanya vitu vinavyokuongezea stress tu. Au unashangaa vitu vingine vinaibuka tu na vinakuongezea stress.

Japo ni kitu kidogo umebadilisha lakini kina nguvu sana.

Pia ukibadili hilo wazo hivyo utagundua unaacha kufikiria kitu hakiwezekani. Na utakua unatafuta mbadala wa kitu.
Usisahau kushukuru.

- Jikataze Kulalamika.
Jizuie kadri uwezavyo usilalamike. Kulalamika maana yake ni unyonge.
Unyonge wa kimawazo. Ni utumwa. Mwanaume usilalamike.

Jiwekee kwamba hutolalamikia kitu chochote na badala yake utakua unatafuta utatuzi.

Na kama hakuna utatuzi, hautolalamika, bali utawaachia wengine wenye uwezo nalo kulitatua.

Na kuna vitu vingine sio vya kulalamikia, basi tu tumezoeshana kulalamikiana. Mfano, mtu hajapokea simu, alafu baadae akapokea.

Kwani kuna haja ya kulalamika kwamba hapokei simu, wakati sasaivi ameshapokea? Sawa saile alikua hapokei, lakini sasa amepokea kwanini ukumbushie mambo yaliyopita badala ya kwenda moja kwa moja kwenye pointi? Au umezoea tu kulalamika ili mradi ulalamike!

Ni stress za kujitengenezea hizo. Jitahidi uruke baadhi ya vitu tulivyozoeshana kwenye jamii.

Mfano, mtu amebarikiwa kupata mlo, na familia yake inakula, inasaza, ina pa kuishi na haiendi hospitali hovyo. Lakini bado analalamika maisha magumu!

Badala ya kushukuru kwa baraka zote hizo alizojaliwa anajiongezea stress kwa kutaka mwenyewe.

Mfano 2, umeona mtu amekosea kidogo, tumeshazoea kumsema/ kumlalamikia kwanza kabla ya kutafuta suluhisho.

Achana na hiyo ya kwanza nenda moja kwa moja kwenye suluhisho. Kwani utapungukiwa kitu? Au mguu wako utakatika usipomlalamikia mtu?

Haijaandikwa popote kwamba kwenye maisha yako lazima ulalamike. Au lazima ugombane na watu. Hivyo vitu ni tumeamua tu kujizoesha.

Mbadala mzuri wa kulalamika ni kushukuru, kufanya kile unachotaka au kuachana na kitu kama kipo nje ya uwezo wako.

Na hapa watu wengi ndo hupata stress, wanalalamikia vitu wanavyoweza kubadilisha lakini hawabadilishi.

Wengine wanalalamikia vitu vilivyo nje ya uwezo wako kabisa. Utafkiri wasipolalamika vidole vyao vitakatika.

Utagundua hivi vitu vitatu vyote vinaingiliana. Ukijizoesha vyote, hakika utakua na mtazamo wa tofauti ambao utakupunguzia sana mawazo.

- Acha Kuhangaika na Yasiyokuhusu.
Inatokana kwamba mtu hajui kile alichoumbiwa, kile Mungu amemtuma afanye hapa duniani. Kwaiyo anakua hajui ni upeo gani anao, na ni nguvu gani anazo.

Mfano, mtu anahangaika na biashara ya kuuza vitu mbalimbali, lakini ukimuweka kwenye kompyuta ni mtaalamu sana. Na hajasomea hapo.

Ana upeo kwenye kitu kingine lakini anafanya vitu vingine.

Pia ukiingilia mambo usiyoweza kubadilisha au mambo anayotakiwa afanye mtu mwingine lazima uwe na stress.

Kaa chini ujitathmini upya. Jiulize, ni kitu gani kipo nje ya upeo wangu lakini naking’ang’ania tu? Ni maamuzi gani hayanihusu lakini nayalazimisha? Kwanini siangalii maisha yangu naangalia ya wengine tu?

Kisha ubadilishe na kuanza taratibu kufanya yale yanayokuhusu.

Pia usikubali kupewa na kuwekea kichwani mzingo usio wako. Mzigo wako ulionao unakutosha.

Na usiruhusu mawazo ya mtu yakuathiri. Yapokee yaone ni kama maoni tu.

Nikutakie Siku Njema Isiyo Na Stress.

Share Na Wengine Wapate Kujifunza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom