Jinsi ya kupika Ugali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya kupika Ugali

Discussion in 'JF Chef' started by MaxShimba, Nov 7, 2009.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  This is how to make it,
  [​IMG]

  Ugali = Cornmeal Mush*

  Serves 8

  Ingredients:

  1 quart water
  1 tea spoon salt
  1 cup white cereal (e.g. farina)
  Instructions:

  In a 2-quart saucepan:
  Boil rapidly 1 quart WATER or CHICKEN BROTH.
  Add: 1 tsp. SALT and
  1 cup ANY FINE WHITE CEREAL.

  Swirl the cereal into the boiling water and cook according to package directions to a thick heavy mush.
  Keep warm over hot water (in a double boiler) until ready to serve. Serving:

  Put in a big glass or plastic bowl then cover with a big plate. Turn upside down so that 'ugali' which is now bowl shaped gets in the plate. Take a smaller dish and press on the top of 'ugali' to form a hole. Pour coconut cream red kidney beans or tapioca leaves, or duckling into the hole and serve. Usually every one eats together. In case some one wants to eat separately, serve a portion of 'ugali' in their plate and pour any of the above mentioned soups onto
  it.

  Do you like it?
   
 2. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Pamoja na maisha hayo moshi mkali,moto mkali, lakini watu bado wanatabasamu na furaha kwa kwenda mbele. Ni maisha matamu sana.
   
 3. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  This is how we eat it.

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=eGTmYmcA0C8&feature=related[/ame]
   
 4. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kabisa Mkuu.
   
 5. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  te te te picha nzuri sana...raha tupu
   
 6. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
 7. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2009
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Mmhh!
   
 8. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #8
  Nov 9, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Yereeeee! huyo ni mama ndubwi akilisonga NGUNA, NGUNGA, BONDO, au SIMA....SEMBE! mwanangu siku ikipita bila kula hili dude hata sishibi! tehteh! Kuna ugali wa mtama, muhogo, mchele, na hata wa viazi. Ila umekosea hapo kwenye kula, dude hiyo inaliwa kwenye mkeka baba, mnauzunguka mkiwa mmekunja miguu, unamega tonge na kuweka shimo la kuchotea mchuzi kkatikati. Nguna inanoga sana kwa mrenda! pembeni kikombe kikuubwa cha mtindi! daha nimemmisi sana Bibi yangu Mpenzi, akipika mtu mwengine tofauti na bibi utajua tuuu!.....kisha utaskia madogo wanaongea chini chini "huu ugali siyo mkono wa bibi...!", mara oooh "na hii mboga mbona imechacha!" wakati ngoma iko kwenye chungu tena imetoka motoni sasa hv hata kuimega mziki, NGOMA YA MOTO KAMA UNAKULA PASI!....kumbe visa tu kumuudhi aliyepika, hasa kama ni shemeji.....teh teh! Yeeeeeeeeeere.

  NAIPENDA SANA TANZANIA
   
 9. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  Mkuu itabidi tupate picha. Maana umeeleza kifasaha vilivyo.
   
 10. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #10
  Nov 9, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 11. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #11
  Nov 9, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0

  mkuu ngoja niorganize sherehe ya "asili yetu" kisha tufanye mapishi ya ugali wa mtama kwa samaki, ugali wa dona kwa mrenda, ugali wa sembe kwa nguru wa kuchoma, ugali wa muhogo kwa furu! picha nitazimwaga hapa za kutosha
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Nov 9, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Dah nguna bana mwisho, kweli hata mie nikiikosa nguna mwili una vibrate. my bro ndo alinifundisha kusonga ugali. kuna wa kuchemsha maji peke yake yakichemka unachota km kikombe kimoja kutokana na kiasi unachotaka kusonga halafu moja kwa moja unaweka unga na kuanza kusonga dizaini nyingine unakoroga uji kwanza ukichemka ndo unatenga uji kidogo pembeni halafu unaweka unga uaendelea songesha. kuna ugali wa muhogo huu wazeiya ni mtamu kupindukia unakuwa mlaini halafu unavutika kwa mbali. ktk kuuandaa kuna time inabidi uutoe kwenye moto usongee chini km dk 5 hivi unaurudisha tena kwenye moto halafu unaendelea kusongesha. kuna wa ulezi huu wakati tupo wadogo tukiuita ugali wa ulea haha baba huu ukila noma yake inakuja unapokwenda toilet lzm upige mayowe kitu hakitoki kigumuuu
   
 13. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #13
  Nov 9, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  Mkuu huu wa Muhogo ukiula na bamia na nyanya chungu na dagaa kwa mbaali basi inakuwa kaaazi kweli kweli.
   
 14. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #14
  Nov 9, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  Mkuu ule wa Muhogo jaribu kula kwa Kambale wakavu na Bamia au Kisamvu cha Nazi, ni hatari kubwa mkuu. Mkuu kama upo karibu na Samaki wa Vibua, basi usisahau hao.

  God bless Dar Es Salaam.
   
 15. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #15
  Nov 9, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 16. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #16
  Nov 9, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Yaani wewe 1080P umenitamanisha ugali mweeee!!!
   
 17. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #17
  Nov 9, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Wewe sasa unanitoa udenda. lol

  Yaani we acha tu, na hako ka pilipili mbuzi ndio kabisaa.
   
 18. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #18
  Nov 10, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  mi nipatie tu ugali wa muhogo, samaki wa kukaanga, mchicha wa nazi na kombe la mtindi baridikwa pembeni, halafu baada ya hapo namalizia na embe dodo moja, hapo nimefika...
   
 19. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #19
  Nov 10, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Kwa wale waliowahi ishi morogoro, kuna wale samaki wanaitwa NGURUKA, wanatoka kwenye bwawa moja hivi huko maeneo ya Nguruka kigoma, ni aina ya PEREGE lkn wanakaangwa na mafuta ya mawese halafu wanawekwa chumvi kwa wingi kuwa preserve, basi wakazi wa mji kasoro bahari unachofanya ni kupiga ugali wakati umemtuma kijana gengeni kuleta hao nguruka wakija ni kupasha moto tu na kulumangia na UGALI, tehe hapo lazima ujing'ate
   
 20. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #20
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hahahah
  yaani mmenikumbusha ugali oops
  pale kwa mamaangu mzazi -- tunakula ugali na mlenda( nsoga) aaah unashuka kama nini unashushia na Togwa jamani

  kule tabora -Ugali na Mswalu akina nyie mpo

  Ugali na Kisamvu ,matembele ,kimanshia sijui nimepatia spelling
  [​IMG]
   
Loading...