Jinsi ya kupika mboga ya majani ya maboga kwa urahisi na kwa muda mfupi

Delightie

Senior Member
Feb 7, 2014
138
196
Habari wapendwa,ni matumaini yangu mu wazima wa afya njema.Leo nataka niwaelekeze kupika mboga ya majani ya maboga kiurahisi na matamu sana,japo najua kila MTU ana style yake ya kuyapika.

MaHITAJI:
1.Majani ya maboga fungu hata 2 kutegemeana na ukubwa wa familia.
2.Hoho.
3.Kitunguu maji
4.Karoti
5.Mafuta ya kupikia
6.Karanga za kusaga(kipome) kwa wenzangu wa nyanda za juu kusini.
7.Chumvi

JINSI YA KUPIKA:
1. Chambua,osha vizuri halafu katakata mboga zako.

2. Chukua sufuria weka mboga yako,weka na mafuta ya kupika kiasi ukitakacho.

3. Andaa kitunguu,hoho,karoti pia weka vyote kwa pamoja juu ya mboga.

4. Weka chumvi na maji kiasi yatakayo tosha kuivisha mboga na karanga utazoweka baadae,ila yasizidi mboga,maana mboga ya majani INA tabia ya kunywea au kusinyaa ikichemka.

5. Bandika jikoni,baada ya dk 8 angalia kama viungo ulivoweka vimesinyaa.

6. Geuza mboga yako iache iive kama dk 5 tena.

7. Baada ya hapo weka karanga zako kulingana na wewe unavopenda(kama Mimi napenda karanga nyingi kwenye hii mboga).unapoweka unakoroga mpka zichanganyike na mboga vizuri.

8. Iache mboga iendelee kuchemka kama dk 5 usiifunike,maana karanga INA tabia ya kushika chini ya sufuria,koroga ili zisishike chini.

9. Hakikisha harufu ya karanga ile mbichi haisikiki,mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa.

INAPENDEZA in UGALI,WALI HATA NDIZI MSHALE AU MZUZU ZILE MBICHI,UKIWA NA PARACHICHI PEMBENI.
 
Yani upike kwa mafuta na karanga vyote kwa pamoja?

Mimi nilizani kiafya ilipaswa kutumia kimojawapo badala ya vyote viwili Yani mafuta ya kupikia na karanga kwenye mboga moja.

Hiyo kazi afya haifai hata kama ukila mdomoni ni tamu sana!
 
Yani upike kwa mafuta na karanga vyote kwa pamoja?

Mimi nilizani kiafya ilipaswa kutumia kimojawapo badala ya vyote viwili Yani mafuta ya kupikia na karanga kwenye mboga moja.

Hiyo kazi afya haifai hata kama ukila mdomoni ni tamu sana!
Mafuta hulainisha mboga ndo maana yanawekwa mwanzoni na sio karanga
 
Hata wale wanaopika chakula kwa nazi na mafuta kwa pamoja ni common mistakes

Haifai kiafya!
Mimi eti napenda maharage niunge na nyanya na kitunguu roast hasa ninaweka na masala au vinginehalafu niweke nazi.
Ule mchanganyiko wake na rangi kama njano njano ndo napenda inanoga hasa
 
Wale wadada wa iringa kujeni huku msome, haraka ya nini ukiwa jikoni? Ule utaratibu wa maji nusu kikombe, mnatia mboga, viungo vyote juu, unafunika baada ya dk 5 kitu inageuzwa imewiva sijui huwa mnawahi wapi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom