Jinsi ya kupika Chapati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya kupika Chapati

Discussion in 'JF Chef' started by X-PASTER, May 18, 2012.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Chapati


  Vipimo


  • Unga wa ngano mweupe ................... 1 Kilo
  • Samli .............................................. 150gm
  • Chumvi ............................................3 vya chai
  • Maji ya moto yasichemke lakini ........... Kiasi
  • Mafuta Ya Zaituni (olive oil) ................ 4 vijiko vya supu
  • Samli tena ....................................... 200 gms
  • Iliki iliyosagwa ...................................1 kijiko cha chai


  Namna Ya Kutayarisha Na Kupika


  1. Tia unga kwenye sinia au bakuli kubwa lilo na nafasi, changanya na chumvi, mafuta ya zaituni, samli 150g, iliki, mimina maji ya moto kwa kipimo cha kikombe kila unapovuruga unga.
  2. Unga uwe mwepesi unapoganda kuwa donge moja kubwa. Uwache kwa muda wa dakika 20 – 30 ukiwa umeufinika ili unga ulainike.
  3. Katakata madonge makubwa yenye ukubwa wa chungwa ili uweze kutoa kila donge chapati mbili. Ukimaliza hapa weka madonge kwa muda wa dakika 15 ukiwa umefinika bila ya kuingia upepo ndani.
  4. Sukuma donge ukiwa umelimwagia unga mkavu juu, liwe mviringo. Unaweza kutumia kifimbo hata chupa kusukumia madonge ikiwa huna kifimbo juu ya meza au kwenye kibao maalumu cha chapati.
  5. Sukuma donge moja mpaka liwe duwara jembamba.
  6. Paka samli kama kijiko kimoja cha kulia, ukihakikisha umepaka duwara lote.
  7. Kunja lile duwara kama mfano wa kamba, huku unazungusha kama kamba ili iwe ndefu kidogo.
  8. Zungusha ile kamba iwe mviringo. Funika na kitambaa kisafi cha jikoni ambacho kimajimaji kidogo.
  9. Endelea namna hii mpaka umalize madonge yote.
  10. Sukuma chapati iwe mviringo kama nchi 7 hivi
  11. Weka chuma cha kuchomea chapati jikoni moto mdogomdogo.


  Pika chapati kwenye frying pan, moto uwe wa kiasi. Ikiiva upande mmoja na kuanza kufura, geuza upande wa pili. Tumia kitambaa kisafi cha jikoni kupress na kuzungusha zungusha ile chapati. Ikiiva upande wa pili, mimina kijiko kimoja cha chakula cha samli na ugeuze chapati tena, zungusha zungusha kisha mimina nusu kijiko cha kulia cha samli na ugeuze upande wa pili kidogo. Toa chapati uweke kwenye sahani. Ikunje kunje kidogo kisha uifingue vizuri.


  Zipange kwenye sahani huku unazifinika, hapa tayari kuliwa kwa mchuzi au mboga yoyote.
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  thanks kwa somo..
  kitu gani kinafanya chapati kuwa ngumu?
   
 3. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  mara nyingi ni ukandaji na kiwango cha maji,unga wa chapati unalainika kwa kukandwa vizuri sio kuweka maji mengi
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Hapa yamekosekana maharage tu

  [​IMG]
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  photo msisahau
   
 7. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  darasa zuri
   
 8. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Ha ha haa......jamaa kafikia KEMPISKI lakinia anakula VYAPATI huku FERI

  [​IMG]
   
 9. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #9
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
 10. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  chapati kwa njegere za nazi, na nyama ya kukaanga au nyama ya kopo.
   
 11. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #11
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Mama, hujaacha tu kula njegere za nazi?
   
 12. Paloma

  Paloma JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2012
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 5,341
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  jamaniii napenda chapatiiiii ziwe za kusukumaa.....au kumimina......wallah zinashuka vizuri mauongoni....ladha yake murua mdomoni....cant wait chai time! Thanks to mpishi kwa kunitengenezea appetite:A S 465:
   
 13. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  tena nikishakula sinawi mikono, hope hujasahau, lol! mzima wewe??
   
 14. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #14
  Sep 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Nisahau tena??? Si ili uwe unanusa harufu yake mda wote...Mie mzima sijui wewe.
   
 15. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #15
  Sep 4, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  mzima sana tu! MUNGU NI MWEMA!
   
 16. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #16
  Sep 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Haya mama...nafurahi kusikia hivyo. Mie napita tu. Wasalimi twins.
   
 17. Lilian Masilago

  Lilian Masilago Verified User

  #17
  Sep 4, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 246
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo la chapati zinakula mafuta mengi sana....
   
 18. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #18
  Sep 4, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  pamoko kaka!
   
 19. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #19
  Sep 4, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Jaribu chapati za nazi, mafuta vijiko 2 tu kwa chapati nzima mpaka kuliwa.
   
 20. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #20
  Sep 4, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Nilikuwa sijaliona hili jukwaa, nitakuwa mdau mkubwa hapa, si mnanikaribisha?
   
Loading...