Jinsi ya kupika chapati laini

Doncy monco

Member
Joined
Jul 26, 2019
Messages
36
Points
125

Doncy monco

Member
Joined Jul 26, 2019
36 125
MAANDALIZI

1.Kwanza hakikisha unakanda unga vizuri

2.Lazima unga uukande mpaka uwe laini sana

3.Baada ya kukata madonge ya idadi ya chapati unazo zitaka

4.Wakati wa kusukuma tumia unga kuhakikisha unapata duara kubwa kiasi

5.Yeyusha samli au blue band changanya na mafuta kupaka katika duara lako

6.Kunja unavyopenda ila kumbuka jinsi unavyo ikunja ndio inatengeneza muonekano mzuri wa chapati

7.Baada ya kuziweka mafuta ni vizuri uziache kiasi cha dakika 10 mpaka 15 kabla ya kuzipika

8.Sukuma chapati jitahidi upate duara zuri lenye shape ya kuvutia

9.Unapo sukuma chapati isiwe nyembamba wala nene sana iwe na upana wa kiasi

10.Chapati ikiwa nyembamba sana unapo ichoma huwa ina kakamaa na ikiwa nene sana huwa haiivi vizuri inaweza kuwa mbichi

JINSI YA KUPIKA

1.Moto hapa ndio kwenye mambo yote ukikosea chapati nayo inaweza kuwa mbaya

2.Moto ukiwa mdogo hupelekea chapati kunyonya mafuta

3.Moto ukiwa mwingi chapati huungua
If the heat is high the chapati will be burnt

4.Weka moto wa wastani ili uivishe chapati yako taratibu

5.Weka chuma jikoni pakaa mafuta kijiko kimoja

6.Weka chapati yako jikoni

7.Iache kidogo sana yaani ikisha kubadilika kutoka ubichi tu geuza upande wa pili

8.Acha iive mpaka ianze kufanya rangi za kuiva

9.Usiache mpaka ikaungua

10.Izungushe zungushe kwenye chuma ili sehemu zote zipate ile rangi ya kuiva hasa nchani mwa chapati

11.Ikunje sehemu mbili sawa

12.Weka mafuta kijiko kimoja

13.Penyeza kijiko kati kati ya chapati

14.Fanya kama unaigandamiza huku ukiisugua na china

15.Ongeza mafuta kidogo izungushe chapati hadi ups chapati yako itakua tayarii kwa kuliwa.
 
Washawasha

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
11,032
Points
2,000

Washawasha

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
11,032 2,000
sijawahi kupika chapati ikawa laini nakwama wapi?
Huwa naweka unga kwenye bakuli
Natia pinch ya sukari
Natia mafuta ya moto,nachanganyachanganya mpaka yale madonge yapotee
Natia maji ya moto,nakanda linakuwa donge kubwa halafu nalifunika,baada ya nusu saa nakata madonge na kumalizia hizo process lkn chapati haiwi LAINI, msaada tafadhali nakwama wapi?
Nalog offHu
 
Executor

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2014
Messages
652
Points
500

Executor

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2014
652 500
sijawahi kupika chapati ikawa laini nakwama wapi?
Huwa naweka unga kwenye bakuli
Natia pinch ya sukari
Natia mafuta ya moto,nachanganyachanganya mpaka yale madonge yapotee
Natia maji ya moto,nakanda linakuwa donge kubwa halafu nalifunika,baada ya nusu saa nakata madonge na kumalizia hizo process lkn chapati haiwi LAINI, msaada tafadhali nakwama wapi?
Nalog offHu
Haha chapati inakuwa ngumu km mkate wa zamani
 
joanah

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
11,067
Points
2,000

joanah

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
11,067 2,000
Ktk vitu vigumu kupiga basi ni hiki.
Ni kweli,kupika chapati,mandazi na vitu vya ngano ni mtihani mgumu sana

Juzi jumamosi nilisema nijaribu kupikia chapati nyumbani nikakandia maziwa,blueband nimeweka lakini chapati zilivyotokea sasa!!!nikaamini kupika chapati is not my thing
 
troublemaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Messages
10,268
Points
2,000

troublemaker

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2015
10,268 2,000

๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€Hukuzipiga picha nione.

Ila me za kumimina kiukweli huwa hazinisumbui. Yaani nazipatia hata kuzigeuza nafanyaga kwa kuzirusha tu.
 
joanah

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
11,067
Points
2,000

joanah

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
11,067 2,000
๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€Hukuzipiga picha nione.

Ila me za kumimina kiukweli huwa hazinisumbui. Yaani nazipatia hata kuzigeuza nafanyaga kwa kuzirusha tu.
Nilipanga zikitokea vizuri nizipige picha nipost kwa status kule WhatsApp lakini kilichotokea ni aibu tupu ๐Ÿ˜

Hizo za kumimina sijajaribu kuzipika lakini nilishakula mara kadhaa hazikunivutia
 
troublemaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Messages
10,268
Points
2,000

troublemaker

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2015
10,268 2,000
Nilipanga zikitokea vizuri nizipige picha nipost kwa status kule WhatsApp lakini kilichotokea ni aibu tupu ๐Ÿ˜

Hizo za kumimina sijajaribu kuzipika lakini nilishakula mara kadhaa hazikunivutia
๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€ Si ajabu hata kuzisukumu tu zilitoka zina mapembe.
Nacheka maana umenikumbusha niliwahi pikiwa chapati hizo kau kau halafu + zina mapembe. Hazieleweki nyingine pembe tatu, nyingine imekaa trapezium
 
joanah

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
11,067
Points
2,000

joanah

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
11,067 2,000
๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€ Si ajabu hata kuzisukumu tu zilitoka zina mapembe.
Nacheka maana umenikumbusha niliwahi pikiwa chapati hizo kau kau halafu + zina mapembe. Hazieleweki nyingine pembe tatu, nyingine imekaa trapezium
Nilisukuma vizuri zilikuwa round bila kona kona
Tatizo ni ule ugumu asa sijui nilikosea wapi akati nilikua naweka katika hotpot
 
mkabasia

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2014
Messages
1,929
Points
1,500

mkabasia

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2014
1,929 1,500
Nilisukuma vizuri zilikuwa round bila kona kona
Tatizo ni ule ugumu asa sijui nilikosea wapi akati nilikua naweka katika hotpot
Labda hukukanda vizuri,au unga ulikua mgumu.Pia kama moto ulikua mdogo sana zikakauka.Sababu nyingine yaweza kua ulivokanda unga hukuacha kidogo ziumuke.
 
Sakayo

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Messages
48,024
Points
2,000

Sakayo

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2015
48,024 2,000
Ni kweli,kupika chapati,mandazi na vitu vya ngano ni mtihani mgumu sana

Juzi jumamosi nilisema nijaribu kupikia chapati nyumbani nikakandia maziwa,blueband nimeweka lakini chapati zilivyotokea sasa!!!nikaamini kupika chapati is not my thing
Kanda unga uwe laini, wakati wa kupaka mafuta ili ukunje tumia KIMBO, kisha ziache kwa dk 20 mpaka 30. Ndo uanze kusukuma dear!
 
Sakayo

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Messages
48,024
Points
2,000

Sakayo

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2015
48,024 2,000
Si ajabu hata kuzisukumu tu zilitoka zina mapembe.
Nacheka maana umenikumbusha niliwahi pikiwa chapati hizo kau kau halafu + zina mapembe. Hazieleweki nyingine pembe tatu, nyingine imekaa trapezium

Mimi nimeanza zipika nikiwa std 5.. saivi napika nauza
 
Forum statistics

Threads 1,344,262
Members 515,354
Posts 32,813,361
Top