Jinsi ya Kupiga Simu na Kutuma SMS nchini Canada na USA Bure

Tanzania Tech

JF-Expert Member
Dec 8, 2016
340
500
Habari wana JF, Karibuni tena tujifunze kidogo kuhusu mambo mbalimbali ya teknolojia, najua kuwa wote mmeamka salama, kama kuna aliyeamka na tatizo usijali hayo yote ni sehemu ya maisha.

Kwa siku ya leo ningependa kushare na nyie njia rahisi ambayo unaweza kupata namba ya USA bure kabisa, njia hii itakusaidia kupiga simu USA na Canada bure, kitu cha msingi unatakiwa kuwa na internet kwenye simu yako. Njia hii imenisaidia sana kupiga simu kwenye sehemu mbalimbali kama Google na sehemu kama hizo pale nilipokuwa na matatizo kama ya Google Adsense na mengine kama hayo. Njia hii pia inaweza kukusaidia kupata namba ya simu ambayo unaweza kuitumia kama namba nyingine za simu namba ambayo pia unaweza kuitumia kusajili WhatsApp au mitandao mingine inayo hitaji namba za simu.

Kifupi ni kuwa namba hii inaweza kukusaidia kwenye mambo mengi sana unachotakiwa ni kufuata maelezo hapo chini, sababu za kuweka video hii ni rahisi kwa mtu kufuatilia kwa vitendo kuliko kuandika maelezo marefu.


Kujua zaidi kuhusu link zilizotejwa tafadhali bofya video husika utapelekwa youtube kisha soma kwenye sehemu ya description utaona link zote. Kama kuna mahali hujaelewa unaweza kuandika hapo chini tutasaidiana kuelewa. I HOPE THIS IS GOING TO HELP YOU ONE WAY OR OTHER
 

Statarea

JF-Expert Member
Dec 11, 2018
895
1,000
Huko youtube unataka viewers? weka kila kitu hapa ili usaidie watu wengi tunaotaka kuwasiliana na mange kimambi na nyani ngabu.
 

Tanzania Tech

JF-Expert Member
Dec 8, 2016
340
500
Huko youtube unataka viewers? weka kila kitu hapa ili usaidie watu wengi tunaotaka kuwasiliana na mange kimambi na nyani ngabu.
its not about view, ila kama unahisi ni views unaweza kuachana nayo, may be inaweza kusaidia wengine.
 

Tanzania Tech

JF-Expert Member
Dec 8, 2016
340
500
Maelezo meeeengi, nikajua umeweka hizo njia hapa.....
Ni ngumu kuweka maelezo yote hapo maana itakuwa ni gazeti na sio kila mtu anapenda kusoma, kwa tathimini niliona wengi hupenda kujifunza kwa vitendo kuliko maandishi inakua ni rahisi hata kwa mgeni wa mambo haya.
 

Tanzania Tech

JF-Expert Member
Dec 8, 2016
340
500
Najua hii itakuja kusaidia mtu kwa namna moja ama nyingine, sipendi kushare kitu kisicho na faida kwa jamii hasa jamii forums, hii imenisaidia mimi sana na imesaidia kampuni yetu kwa ujumla, kama unaona hii haina faida kwako achana nayo kwa sasa utaitafuta baadae ukiwa na shida nayo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom