Jinsi ya kupata wazo la biashara (special kwa graduates)

Hunyu

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
4,775
4,316
Ndugu zangu Jf napenda kumshukuru Mungu kwa siku nyingine tena ambayo ametuwezesha kuiona. Mungu azidi kukulinda na kukubariki popote ulipo na akuvushe katika kila gumu ulilonalo.

Moja kwa moja kwenye Mada, nimetafakari nikaona niwasaidie wadogo zangu ambao wamemaliza vyuo na wako mtaani hawana issue au wanawaza watapata wapi ajira. Ni kwamba ajira kwa sasa ni ngumu sana ingawa zipo nyingi tu ila kuzipata ndio issue. Hazipatikani either kwasababu zinatolewa kwa kujuana au hizo kazi hazipati watu wenye sifa sitahiki lakini pia kuzigundua (locate) ni issue nyingine kwasababu pengine zinatangwaza ndani ya taasisi husika tu bila kuhusisha watu was nje. Anyway hill sio lengo LA Uzi, ngoja niande kwenye lengo LA Uzi.

Nataka nikusaidie wewe ambaye unawaza utapata wapi issue ya kufanya au utapata wapi ajira.

Moja.
Ni lazima utambue kuwa, wewe jinsi ulivyoumbwa unakipaji ndani yako ambacho ni tofauti ni MTU mwingine yeyote hapa duniani. Kama hujui kama unakipaji unaweza kutumia njia ya kukaa chini ufikiri ni jambo gani ukilifanya hulifanya kwa ufanisi zaidi, watu hukuelewa na kukuappreciate sana au uko comfortable sana kulifanya. Hapa naomba tuweke pembeni kabisa suala LA elimu kwasababu Mimi elimu naichukulia kama sehemu ya kukupatia uwezo mkubwa wa kufikiri na kuweza kupractice talent yako.

Ukishakigundua anza kukupractice ili kikufae kwa maisha ya kila siku. Kama unaweza imba imba, kucheza, kuandika, kuchekesha, kupika..chochote Fanya ili mradi moyo uwe na amani.


Mbili:
Badili kile unachokipenda kuwa fursa ya BIASHARA. Hapo juu nimeongelea kuhusu kuangalia ni kitu gani unakipenda katika maisha yako na ukikifanya unakifanya kwa ufanisi.

Sasa kitu hicho unatakiwa ni kukitumia kipaji chako kama fursa ya BIASHARA. Tumezoea kuona wanamziki wakiendeleza vipaji vyao baada ya shule au akihisi kama anauwezo was kuimba basi anaamua kukomaa hao hapo. Vivyo hivyo na wewe unaweza kuiendeleza talent yako ya ususi ikawa fursa ya kukupatia kipato. Mfano, wakati uko chuo watu walikuwa wanakufuata sana wakikuomba uwasuke na ukiwasuka wanaapreciate sana, basi hiyo ni fursa unaweza kuitumia. Tengeneza vipeperushi hata hamsini, kagawe kwenye sehemu yanye mkusanyiko mkubwa na maofisin kwamba unasuka na pengine unaosha na nywele Bure kama bonus kwa wateja. Waambie wakupigie au waje sehemu flani utawahudumia. Nakuambia ukifanya hivyo kwa moyo hutalalamika kuwa hamna ajira kwasababu kwa mwanzo huo baada ya muda utapata mtaji wa kufungua salon yako nzuri. Huo ni mfano mmoja wa jinsi ya kutumia talent yako.

Tatu:
Angalia changamoto zilizopo mtaani kwenu au katika duka LA mangi wa mtaani kwenu. Mfano, katika duka LA mangi bidhaa zote zinapatokana lakini mangi kaizoelea BIASHARA kwasababu yuko peke yake mtaani kwahiyo hana motisha kwa wateja wake. Cha kufanya, fungua biashara kama ya Mangi, tengeneza mkakati wa kuchukua wateja asilimia 60-70 ya wateja wote wa mangi hapo mtaani. Njia ya kwanza ni kutumia watoto. Hakikisha kila mtoto anayekuja kupata huduma kwako unampatia Big G moja ya Bure. Au hata mzazi akinunua bidhaa Fulani Fulani mpatie na pipi au Big G kwa ajili ya mtoto wake. Nakuhakikishia, baada ya miezi miwili utakuwa unakimbiza kuliko mangi kwasababu, mtaani wanaofanya manunuzi Mara nyingi ni watoto ambao huagizwa mahitaji ya nyumbani na watakuwa wanakimbilia kwako kwasababu wanauhakika wa kupata Ben ten za Bure.

NNE:
Acha kujifungia ndani na kuangalia TV kisa huna kazi au huna cha kufanya. Waswahili wanamsemo wao unasema mtembea Bure si sawa na mkaa Bure. Kwasababu, kama umetoka kwamfano mwenge mpaka ubungo kwa lengo LA kwamba unatembeatu kujifunza na usitake kupanda daladala ili huko njiani upate kuangalia fursa na wengine wanafanya nini, nakuhakikishia huko njiani utaona tu kitu ambacho kitakupa changamoto kuwa kama huyu anafanya hivi kumbe na Mimi nnaweza Fanya hivo. Maana yangu ni kwamba jinsi unavyotembea ndio mawazo yako yanafanya kazi kuhusu nini ufanye: Angalizo, ukitaka kufanya hii kitu be serious kwamba natoka kwenda kutafta fursa:

Ushuhuda wangu, kuna wakati nikiwa nimemaliza form four nikawa nawaza nitafanya nini, kichwani likanijia wazo nitafte kibanda cha kukodi ili nianzishe salon ya kunyoa. Wakati natembea mjini kuna sehemu nikaona kuna kibanda cha kampuni ya coca cola. Kichwani nikaona kile nikikipata kitanifaa kwa matumizi. Ikabidi niulizie yule mtu wa pembeni, mbona hiki kibanda hakifanyi kazi na nikikihitaji nakipataje? Yule mtu akaniambia ukikihitaji mtafte meneja wa coca cola ndio atakusadia. Sikulaza damu, nikauliza ofisi za coca cola ziko wapi ili nionane na meneja nimuombe hicho kibanda. Ni kweli nikafanikiwa kuziona ofisi, ila kumuona meneja ikawa mziki, nikawa napigwa tarehe njoo kesho njoo kesho kutwa hadi week tatu zikafika. Kumbuka kila siku naenda kumuulizia naambiwa njoo kesho. Wakati naendelea kumtafta meneja, kichwani likanijia wazo kuwa nikionana na meneja nimwambie vitu viwili, suala LA kibanda lakini nimuombe kazi. Kweli baada ya wiki tatu nilifanikiwa kuonana nae tena akiwa high high, dogo unasemaje, nikamsogolea nikamweleza shida zangu. Kuhusu kibanda akaniambia kina mtu hawezi kunipatia, kuhusu kazi akaniambia Hamna ila ikipatikana atanijulisha, akaniambia Nipe namba yako. Nikamwachia namba nikarudi mnyonge sana siku zikaenda huku napambana kupata kibanda. Kumbuka nafanya yote haya sina hata shilingi mfukoni.

Kilichotokea baada ya mwezi mmoja siku moja jioni sa kumi na moja nikapigiwa simu na namba nisioifahamu. Baada ya kupokea akaniuliza we ni Fulani, nikasema ndio, akaniambia Mimi ni meneja wa mkoa wa coca cola, kesho asubuhi uje uanze kazi. Huo ndio ulikuwa muujiza, sikulala siku hiyo nawaza kesho ifike nikaanze kazi.
So usijifungie ndani.

Hitimisho:
Kila mtu anadestiny yake, usiangalie mazingira na jinsi mambo yalivyo ukakata tamaa kwamba sitapata ajira, no. Amka anza na hapo ulipo, fursa ndio hiyo na ndio milango mingine itafunguka.

Asanteni na usiku mwema!
 
Dah...uzi mtamu lakn naona wana wanapita pembeni...wanakimbilia jukwaa la siasa kumtukana Maghufuli na jukwaa la celebrity kumshangilia diamond na wasafi festival pamoja na demu wake mpya
 
Duuhh " bonge si-la thread ".... watu wa Kg wamezoea ku-discuss kuhusu makalio na siasa tu .. masuala ya msingi " kama haya " huwezi kuwakuta waki-ya discuss " hata utakapo wakuta " basi huwa ni wachache " ...

No Wonder CCM inavyo endelea kuitawala hii nchi kwa takribani ya nusu karne sasa "
 
Umeanza vizuri ulipofika kwenye habari za iccm ndio umevuruga aseee
Duuhh " bonge si-la thread ".... watu wa Kg wamezoea ku-discuss kuhusu makalio na siasa tu .. masuala ya msingi " kama haya " huwezi kuwakuta waki-ya discuss " hata utakapo wakuta " basi huwa ni wachache " ...

No Wonder CCM inavyo endelea kuitawala hii nchi kwa takribani ya nusu karne sasa "
 
Dah...uzi mtamu lakn naona wana wanapita pembeni...wanakimbilia jukwaa la siasa kumtukana Maghufuli na jukwaa la celebrity kumshangilia diamond na wasafi festival pamoja na demu wake mpya
Ni kawaida mkuu, watanzania tunapenda porojo kuliko mambo ya msingi.
 
Mfano mimi katika familia hakuna anaeamin nje ya kuajiriwa

Alaf mim ndo sipendi kuajiriwa mpak basi .sina mtaj ila nina mtaj wa akil japo sio nyingi za kuitwa jiniaz

Naamin siku moja allah atafungua njia zake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom