Jinsi ya kupata PML ya kitalu cha Copper huko Ruangwa

Bitabo

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,902
687
Wakuu jamvini naombeni msaada wenu.

Nataka kupata Mining Licence (wenyewe wanaiita PML) ya kitalu cha Copper huko Ruangwa, Lindi.
Naomba mwenye kujua utaratibu anisaidie njue pa kuanzia na kumalizia na kama kuna kitu natakiwa kuandaa ili kufanikiwa. Mimi ni Mtanzania.
Nawashukuru in advance
 
Mkuu ntakusaidia ninachokijua.
Leseni za utafiti madiini zinapatikana wizarani dar es salaam.
Leseni za uchimbaji zinapatikana ofisi za madini za kanda.
UNACHOTAKIWA KUFANYA.
kama tayari una uhakika kwamba eneo unalotaka kuchimba lina madini, na sasa moja kwa moja unataka lesseni ya uchimbaji, nenda ofisi ya madini ya kanda (kwa bahati mbaya sijui ofisi ya kanda ya kusini iko wapi).Kabla ya kwenda, hakiisha kwamba eneo unalotaka kuchimba tayari ni lako, yaani kama ni shamba la mtu, wasiliana na mwenye shamba kwanza na serikali za mitaa uhakikishe unamilikishwa eneo hilo kihalali.Baada ya hapo, uwe na angalau miliioni moja kwa ajili ya gharama za leseni. ukiwa na m1.5, ni bora zaidi.

NI HAYO TU MKUU NAKUTAKIA MAFANIKIO, UKIPATATA MADINI UNIKUMBUKE.

mimi nashughulika zaidi na utafiti wa vito na dhahabu.Pia nauza gold metal detectors.Hivi huko kusini hakuna sehemu yenye madini ya vito?
 
Mkuu nakushukuru sana kwa ushauri wako. Nitakupa mrejesho pale nitakapofikia.
Tunduru kuna gemstones nyingi from Diamond. Saphire na nyingi wala sizijui. Ungefika huko ungepata picha maana watu wa malaysia. China na thailand wako wengi huko
 
Kama hujui mambo bora umshauri mtu aende kwenye ofisi ya madini iliyokaribu naye atapewa utaratibu.
1.kama ameshafanya utafiti(exploration)ktk eneo husika kwa kuchukua mawe nakupeleka maabara kama vile SEAMIC kule Kunduchi dar au SGS na STAMICO dom akapata matokeo mazuri yaani % nzuri ya copper kama vile 20% nakuendelea
2.the next step ni kwenda na GPS device kuchukua cordinates za eneo husika na kujaza fomu za maombi ya PML nakulipa sh.50000/ kwa ajili ya ada ya maombi kwa leseni moja.
3.maandalizi ya kupatiwa kitalu yatafanywa na afisa madini kwa kuingiza cordinates hizo kwenye system nakuona kama hakuna maombi au leseni nyingine.sheria ya madini ya 2010 inataka aliyeomba kwanza afikiriwe kwanza.
4.kama eneo liko huru basi mwombaji atapewa barua ya offer ambapo atatakiwa kulipia 50000/ ya kuandaa leseni.na atatakiwa kulipa kiasi cha shilingi 80000/kwa kila hekta moja ya mraba...kama eneo lina hekta kumi za mraba basi atalila laki 8 za ada ya leseni(annual rent)
5.sheria imeweka mazingira mazuri ya kuelewana na mwenye shamba aidha kushirikiana kuchimba au kuuza kabisa eneo.kwa hiyo makubaliano hayo yatafikiwa na kushuhudiwa na viongozi pia ikiwezekana wa kijiji au kitongoji husika.huwa kuna surface rights na mineral rights..surface rights zinamfanya mwenye shamba kuweza kufanya shughuli za kilimo na ujenzi..ila mineral rights ni za raisi.
6.kwa mkt wa kijiji au kitongoji au mkurugenzi wa halmashauri hana nafasi ktk utoaji wa leseni..na hili limekuwa tatizo hata ktk viongozi wa TAMISEMI kutoza Ushuru wa zaidi ya 0.3% kama service levy(ushuru wa huduma) kwa wachimbaji..kifupi sheria Inataka ulipaji wa fidia mzuri au makubaliano yenye maslahi bora kwa mmiliki wa shamba..
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom