Jinsi ya kupata marafiki na kuwafanya wafanye unachotaka

shadownet

Senior Member
Aug 4, 2015
133
1,000
Nadhani hapa wengi wetu kila moja anamjua mtu Fulani ambae hata akienda kwenye sehemu ambayo hajulikani yeye haimchukui dakika hata zaidi ya 5 kuwa marafiki na watu asiowajua kwa kiasi ambacho huo urafiki unaweza kuonekana wa miaka kumbe ni wa dakika 5 tu, Katika uzi huu tutajifunza ni namna gani tunaweza kupata marafiki ambao wanaweza pia kufanya vitu tunavyotaka wao watufanyie kwa ufanisi zaidi.

UKITAKA KUZOELEKA HARAKA, JENGA MAZOEA YA KUTABASAMU

Kama unataka uwe unapendwa na watu kwa haraka zaidi basi cha kufanya waonyeshe watu kwamba una furaha, Kuna huyu mnyama anaitwa Mbwa, Huyu mnyama ni mnyama ambaye ametokea kupendwa sana kuliko wanyama wengine na hii ni kwa sababu kila ukimkaribia anaonyesha kwamba amejawa na furaha huku akizungusha mkia wake kama feni.

Usitabasamu kwa ajili umemuona mtu Fulani, Jenga mazoea ya kutabasamu kila mara. To be honest mnaweza kudhani ni utani lakini kuna siku nlikutana na kingwendu alie nifanya nimuone kama mshkaji ndani ya dakika tu na nakumbuka alifanyia masihara nimnunulie coca na kama asingekuwa anatania mimi nlikua tayari kumpa anachotaka,Sasa unajua kwanini ilitikea hii? Jibu ni rahisi maana kingwendu kila mda uso wake una tabasamu, Sasa ndugu yangu unaemuona mtu kwenye mwendokasi ndo unatabasamu lazima na yeye ashtuke mana kabla ya hapo aidha ulikuwa umenuna au upo kawaida tu na atahisi unataka kumtumia kufikisha malengo yako. Jaribu kutabasamu kila muda hata unapoongea, Nadhani hii sifa hata mtu wetu wa nguvu Millard Ayo anayo ndio mana ni mshkaji wa kila mtanzania. Kununa nuna ni ishara tosha kwamba haupo kwenye mood ya kuongeleshwa, so hata ukimfata mtu nae anakukwepa design flani hivi.

ACHA KUKOSOA TOA USHAURI

Kuwabishia / kuwapinga watu na kuongelea makosa yao hakuwafanyi wakupende au wajirekebishe kwa hiari yao bali kunawafanya waongeze kiburi ili wajione wao ndio wapo bora kitu ambacho kinaharibu urafiki, Binadamu ni viumbe vinavyo ingia katika urafiki kwa hisia na sio kwa sababu Fulani. Mtu unaemkosoa ni vigumu apokee ushauri wako maana anaona kabisa unamshambulia kitu kinachomfanya apate hisia za kujilinda kwa kukubishia zaidi, Na hata akikubaki basi kakubali kishingo upande. Njia nzuri sio kukosoa bali kutoa ushauri, Kwa mfano ukiwaona wanafunzi wa sekondari wanvuta bangi viwanja vya mpira usiwakaripie kwa hasira kuwa waache kuvuta bangi , Wape ushauri kwa kuanza kujenga mazingira mazuri kama kuwahadithia hostoria ya Ronaldo . Messi na ndipo una powaambia kwamba wakitaka waje kuwa kama hawa siku moja wasivute hizo bangi, Hii njia angalau itakuwa nzuri kuliko ya kuwakaripia. Usiwakosoe watu maana hata sisi tungekuwa katika hali zao basi kwa njia moja ama nyingine tungeyatenda mambo ambayo tumewakosoa,

Leo hii wewe ni bosi ambae kila kosa unakosoa kosoa tu na unalalamika kwamba hupendwi na wafanyakazi wako, Pungiza ukosoaji ongeza ushauri.


UKITAKA UFANYIWE JAMBO NA MTU, JALI WATU KUTOKA MOYONI MARA KWA MARA.


Unawezaje kumfanya mtu mtu akufanyie kitu Fulani? Jibu ni kwamba inabidi uhakikishe kwamba wanataka kukufanyia hicho kitu unachotaka ufanyiwe, Kila mtu hii dunia anataka kujaliwa na watu, Kila mtu anataka asifiwe na asikie kwamba anafanya vitu vyake vizuri. Hata hapa jamii forums wale watu wanaoonyesha kujali jitihada za watu wanaoandaa post na kuwapongeza , Believe me or not hao watu wanakuaga marafiki na wanaoandaa posts. Ili umfanye mtu afanye unachotaka msifie na umjali mara kwa mara, Ukimtisha tisha na kumkosoa kosoa hatafanya kitu kwa hiari yake na utendaji wa kazi yake unaweza kuwa mbaya na ikitokea yupo juu yako basi sahau kabisa yeye akufanyie kitu unachotaka. Jaribu kumweka kila mtu juu yako hata kama wewe ni boss, Waheshimu na wajali kutoka moyoni mwako.

Kumyonyesha mtu unamjali mfanye huyo mtu ajiskie raha anapofanya kazi na wewe au unapokuwa nay eye. Jaribu kutumia haya maneno mara kwa mara “Ahsante”, Nisamehe” na pia wewe ujifunze kuwasifia kutoka moyoni. Usijifanyishe kujali maana muda ndio kufichua kila kitu na mwisho wa siku utaonekeana mnafki mkubwa nah ii habari ikisambaa basi hata marafiki zako wengine watakuona mnafki.
KAMA UNATAKA UZOELEKE HARAKA, KUWA INTERESTED NA WATU WENGINE.


Waweza kutengeneza marafiki kwa muda mfupi kwa kuwa interested nao kuliko kuwafanya wao wawe interested na wewe, Kila mtu anapenda kuwa na mtu msikuvu ambaye anampa hamasa ya kuingea zaidi vitu vilivyomo ndani ya akili na moyo wake, Kama unataka uanze kuzoeleka fasta usiongee sana bali kuwa msikivu,Siri ya kuwa interesting kwa watu ni wewe kuwa interested nao, Kumsikia mtu ni kumpa mtu huyo attention yako yote, Usiwakatishe ama kuwa bize na vitu vingine wanapoongea, Kitu kingine unapoongea usijiongelee wewe mwenyewe tu maana utakinai fasta, Just imagine kila mtu unamwambia unamiliki kitu Fulani, unajua kuimba, una g.f/b.f mkali?!! Utakinai, Jaribu kumwongelea mlengwa pia na vitu ambavyo yupo interested navyo, Kwahiyo janani kama mnataka muwwe watu mnaotaka marafiki basi jaribuni kuwa wasikivu na piawapeni hamasa ya kuongea walengwa, Tumia maneno haya kuonyesha uskikivu” Eheeee”, “Kweli?”, “Endelea”.


ONGELEA VITU AMBAVYO NI MUHIMU KWAO NA USISAHAU MAJINA YAO


Kila mtu anapenda kuongea na mtu anayejua jambo ambalo yeye hupenda, Fatilia vitu gani watu wanavipenda then anza kuviongea, Kwa mfano kama mtu anapenda mambo ya dini ni vizuri kuongea nae mambo ya dini kwa asilimia kubwa katika maongezi yenu, Waongelee watu kuhusu wao na vitu wanavyovipenda hapo ndipo mtatpopiga story bila kuchokana, Watendee watu kama vile unayopenda kutendewa.

Kukumbuka jina lamtu ni namna nyingine ya kufanya upendeke haraka, Mimi mwenyewe nkikutana na mtu njiani aniambie “Niaje kaka” Ntamchukulia simple, Ila mtu nkutane nae anisalimie kwa jina langu ntakuwa nae so interested mana inaonyesha ni jinsi gani tu kaacha kukariri vitu vingine ili akariri jina langu, Pia kuna vitu kama tarehe za vitu muhimu kama birth days ni vitu ambavyo ukimkumbusha mtu miaka nenda rudi atakujali sana.


UNAPOKOSEA KIRI KOSA ,JIKOSOE NA UOMBE MSAMAHA HARAKA


Hakuna mtu ambae hafanyagi makosa hii dunia, Hakuna binadamu aliyekamilika, Popote unapomkosea mtu basi jua kuna njia ya haraka ya kukandamiza huzuni / hasira za uliemkosea ambayo ni kukiri kosa Haraka iwezekanavyo na kumuambia hutarudia, Usiishie kusema tu “Samahani” kiri kosa na namna uivyolitenda na mwishowe useme samahani.

Kitu kingine jikosoe mwenyewe kabla huakosolewa na lundo la watu, Jikosoe kwamba kosa ulilotenda ni kwajili ya uzembe wako, kir kosa na uombe msamaha, Hii njia itakufanya ujikosoe mwenyewe na kukwepa kwa kiwamngo kikubwa ukosoaji wa watu wengi

MY OTHER POSTS

Funzo: Mapenzi imara yatakayodumu muda mrefu
Jifunze kupendwa ndani ya dakika chache
Jifunze mbinu za kujitegemea kiuchumi na kuwa tajiri
Jinsi ya kupata marafiki na kuwafanya wafanye unachotaka
 

Man Thom

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
717
1,000
Upuuz mtupu
Nadhani tukiwa na utaratibu wa kuvumiliana, kuheshimu mawazo ya watu wengine kwa kuyachukulia uzito..Tanzania itakuwa sehemu nzuri na salama ya kuishi..na si ajabu tutapiga hatua kimaendeleo! Wakati mwingine kama jambo linakukera ni bora kukaa kimya kuliko kufanya kama ulilofanya ambalo kimantiki halina maana yeyote mkuu! Tuheshimu wengine..period
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom