Jinsi ya kupata driving licence mpya kwa haraka!

Nina Diploma ya Motor Vehicle Engineering from Belgium, nilikuwa chuo kimoja na King of all social network.
Apart from Engineering, driving is an art. You might be a good engineer yet very poor driver.
 
Watanzania bana,
Wachangiaji wengi hapa badala ya kulaani driving licence autholity kwa upokeaji wa rushwa ili kupindisha taratibu za utoaji leseni badala yake wanampiga madongo investigative journalist kana kwamba yeye ndiyo mwenye makosa. Hii inapelekea kuamini kuwa inawezekana wengi wao wana leseni ambazo wamezipata kwa njia hiyo au wanakubaliana na utaratibu huu wa rushwa.

Watu hawa hawa kila siku wanapiga kelele kuhusu ufisadi nchini lakini wanasahau kuwa ufisadi chimbuko lake ni rushwa hizi 'ndogondogo' ambazo madhara yake ni makubwa kwa jamii.

Tupende tusipende, upatikanaji wa leseni bila utaratibu uliowekwa kisheria ni moja ya kichocheo cha ajali barabarani. Na kama umepata leseni kwa njia hiyo na hujasababisha ajali, hii haina maana kuwa wote waliofanya hivyo wako makini kama wewe.

Kwa mawazo na fikra kama hizi siyo ajabu tatizo la rushwa nchini linakuwa ni ndoto za alinacha kuliondoa.
 
anaway hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya ajali na Fake Driving License!
Ajali utokea kwa sababu madereva wengi wanakiuka sheria na taratibu za barabarani

Yaani ulivyojichanganya kwenye hizo sentensi mbili unajua mwenyewe.

Hivi ni kwa nini watu wanatakiwa kufanya driving lessons?

Siyo kuzijua sheria na taratibu za barabarani?
 
Kwa utaratibu uliopo sasa hivi wa kutoa leseni, ukitoa RUSHWA hilo linakuwa ni tatizo lako mwenyewe!
kuna baadhi ya watanzania ambao wameshajenga tabia fulani kuwa bila "Middle man (mtu wa kati)" hawawezi kufanikisha mambo yao. wengi wao ndio wanaojipendekeza na vijiela vyao hata bila kuombwa rushwa!
Binafsi nilipata yangu hivi karibuni nililipa pesa halali na kufuata taratibu na bado nikapata ndani ya wakati,
cha ajabu nilikutana na baadhi ya watu wananishauri nitoe rushwa nishugulikiwa haraka, nikawambia sitoi.
Tusilaumu mamlaka usika, tujilaumu sisi tulioweka vijiela vyetu mbele kutafuta favour ambayo kimsingi inapaswa kuwa Haki yako! Kila mtanzania akisema NO kwa Rushwa-inakwisha tu!
Mind set change is very important!
Sehemu nyingi sana nimefanikisha mambo yangu kwa wakati na bila rushwa, lakini wengine wakienda kwa shughuli kama hizohizo, lazima walalamike kuwa wametokwa pesa isivo halali..WHY?? hii ni sawa na mwanamke anayejilengesha akishatongozwa analaumu wanaume waliomtongoza wakati alitengeneza mazingira yeye mwenyewe!
Watanzania tuache uzushi, na kulaumulaumu tu!

Watanzania bana,
Wachangiaji wengi hapa badala ya kulaani driving licence autholity kwa upokeaji wa rushwa ili kupindisha taratibu za utoaji leseni badala yake wanampiga madongo investigative journalist kana kwamba yeye ndiyo mwenye makosa. Hii inapelekea kuamini kuwa inawezekana wengi wao wana leseni ambazo wamezipata kwa njia hiyo au wanakubaliana na utaratibu huu wa rushwa.

Watu hawa hawa kila siku wanapiga kelele kuhusu ufisadi nchini lakini wanasahau kuwa ufisadi chimbuko lake ni rushwa hizi 'ndogondogo' ambazo madhara yake ni makubwa kwa jamii.

Tupende tusipende, upatikanaji wa leseni bila utaratibu uliowekwa kisheria ni moja ya kichocheo cha ajali barabarani. Na kama umepata leseni kwa njia hiyo na hujasababisha ajali, hii haina maana kuwa wote waliofanya hivyo wako makini kama wewe.

Kwa mawazo na fikra kama hizi siyo ajabu tatizo la rushwa nchini linakuwa ni ndoto za alinacha kuliondoa.
 
Ndio leseni zetu hazikubaliki sehemu yoyote duniani maana wanajua zimenunuliwa sio za qualification:madgrin::madgrin:
 
andaa sh 150000 nenda myfair muone mlinzi wa kampuni fulani"alwayz yuko bz"atakujazia form na kukupitisha kila sehem kisha anachukua no ya cm after three working dayz anakupigia ufuate leseni yako.fanya udadisi utakachoona tujadili nini kifanyike.nawakilisha.
 
Do you beleive the accidents are coused by these iilligal procedures?, or incompetence of the drivers? I have so many examples of drivers who attended driving classes, passed police tests, acquired licence, and yet they dont perform good driving. I dont accept curruptions in providing driving licence, but believe that having legal licence does not mean good driver.
Wahenga walisema usiige tembo kupyupyupyu utapasuka msamba.
 
andaa sh 150000 nenda myfair muone mlinzi wa kampuni fulani"alwayz yuko bz"atakujazia form na kukupitisha kila sehem kisha anachukua no ya cm after three working dayz anakupigia ufuate leseni yako.fanya udadisi utakachoona tujadili nini kifanyike.nawakilisha.
Huyo jamaa anafahamika kwa tabia yake ya kusababisha wateja kutofuata utaratibu wa foleni.
Wajihi wake ni: sio mfupi wala sio mrefu, ana mwili umeshiba kidogo, jina lake kwa leo nalihifadhi ila ipo siku akiingia kwenye anga la kimataifa nitamlipua hapa hapa na picha yake.
 
Kwa utaratibu uliopo sasa hivi wa kutoa leseni, ukitoa RUSHWA hilo linakuwa ni tatizo lako mwenyewe!
kuna baadhi ya watanzania ambao wameshajenga tabia fulani kuwa bila "Middle man (mtu wa kati)" hawawezi kufanikisha mambo yao. wengi wao ndio wanaojipendekeza na vijiela vyao hata bila kuombwa rushwa!
Binafsi nilipata yangu hivi karibuni nililipa pesa halali na kufuata taratibu na bado nikapata ndani ya wakati,
cha ajabu nilikutana na baadhi ya watu wananishauri nitoe rushwa nishugulikiwa haraka, nikawambia sitoi.
Tusilaumu mamlaka usika, tujilaumu sisi tulioweka vijiela vyetu mbele kutafuta favour ambayo kimsingi inapaswa kuwa Haki yako! Kila mtanzania akisema NO kwa Rushwa-inakwisha tu!
Mind set change is very important!
Sehemu nyingi sana nimefanikisha mambo yangu kwa wakati na bila rushwa, lakini wengine wakienda kwa shughuli kama hizohizo, lazima walalamike kuwa wametokwa pesa isivo halali..WHY?? hii ni sawa na mwanamke anayejilengesha akishatongozwa analaumu wanaume waliomtongoza wakati alitengeneza mazingira yeye mwenyewe!
Watanzania tuache uzushi, na kulaumulaumu tu!
Mkuu Mjanga mimi pia nilipata leseni yangu mpya bila usumbufu wowote, ni taratibu za kiofisi za kawaida tu ndizo nilizozikuta pale Myfair plaza.

Nilitakiwa kwanza kuwa na TIN yangu kabla ya kujaza fomu maalumu iliyopo pale.

Baada ya hapo utaonyesha fomu yako na leseni yako ya zamani kwa afisa wa TRA husika kwenye kaunta namba 1,2,3,4,au 5 ambapo utachukuliwa picha yako, alama za vidole na kuweka sahihi yako.

Utaenda dirisha lingine ambapo utakuta askari wa barabarani hapo utaonesha leseni yako tena na kupatiwa karatasi maalumu ambayo itaonesha ni kiasi gani unatakiwa kulipia benki.

Baada ya kulipia 40,000/= utatakiwa kusubiri kwa siku mbili tu, leseni yako inakuwa ipo tayari in akusubiri kaunta namba 6 bila usumbufu wowote.

Sasa huo mlolongo wa matukio yanayohusianishwa na rushwa ninaouona hapa sijui unatoka wapi. Labda cha kufanyiwa kazi ni yule mlinzi aliyetajwa hapa, kwa kweli kuna kitu cha kufanyiwa kazi pale.
 
Back
Top Bottom