Jinsi ya kupangalia chumba cha kulala kiwe na mvuto zaidi




Nyumba ni urembo, nyumba ni mapambo, ili nyumba iweze kuvutia inahitaji mazingira yenye hadhi ambayo yanaweza kumvutia mtu kwa muonekano wake wa nje na ndani pia inaweza kumvutia mtu kutokana na rangi za chumba.

Watu wengi huweka mazingira safi jikoni, sebuleni na kusahau kuwa chumba cha kulala pia kinatakiwa kuwa safi muda wote kwani ni sehemu ambayo inatumiwa kwa mapumziko.

Ili kuweze kupumzika vizuri baada ya mizunguko ya kutwa nzima ni vizuri chumba kikawa katika muonekano mzuri ambapo sambamba na hilo uwepo mpangilio mzuri wa nguo na fenicha.

Chumba cha kulala hakitakiwi kuwa na vitu vingi, kinahitaki kuwa na hewa ya kutosha ili kumuwezesha mtumiaji kuweza kupata hewa safi pia inamsaidia mtumiaji kuweza kufanya usafi sehemu zote kutokana kuwepo kwa nafasi ya kutosha.

Epuka kujaza vitu vingi chumbani kama computer, meza viti, kapu la nguo chafu, kwani vitu hivyo vinaweza kuwekwa sehemu nyingine ya nyumba na chumba kubaki mahali pa kupumzika tu.

View attachment 632369 View attachment 632370
Unampangilio mzuri wewe ngoja nije pm uniaabarishe
 
33b101081ec70e6038d59acda8442973.jpg


Plan kama hii inafaa kwa vijana tunaoanza maisha ila maBachelor tu.
Ata ukiwa na familia ndogo inafaa sana. Familia ya mtoto mmoja
 
Ku maintain status hakikisha upende kununua vitu quality, usijaze vitu vingi halafu vibovu... Basics za muhimu sebuleni kwa kijana wa kisasa ni Carpet, Sofa seats, TV & Deck, Pazia, Coffee table, Theatre system (si lazima but ni muhimu kwa entertainment) na Meza kwa ajili ya TV.

Hakikisha unaponunua/andaa vitu vi blend; blend in the sense kua unapokua/nunua vitu hivyo vya electronics hakikisha vinaendana rangi Vizuri, then unaangalia rangi ya ukuta wa hio sebule, unanunua pazia quality nzuri na rangi zilizopoa na za kiume kama coffee, beige, grey (kwa ufupi colours dark - usidhubutu sujui pink, yellow n.k). Mara nyingi coffe table nzuri za kisasa ni zile za kioo zenye stool zake, na hizi siku hizi zimeshuka sana bei sana i believe ukijipanga u can afford - miguu ya coffee table rangi ifanane na ya meza ya Tv.

Carpet nunua mwishoni, cause ni a guy mara nyingi nyie nafasi ya usafi ni finyu, nakushari dark colours; inaweza kua ya maua au michoro yenye rangi zote kama za pazia, sofa, meza n.k - ikiwa rangi moja walau iendane na pazia.. Carpet ikiwa dark colour itakusaidia coz ni nyumba ya vyumba viwili inamana lazima utapita sana hapo.

Kuepusha kuweka vitu kama glasses, sahani, jugs sehemu yoyote ya sebule ni vizuri ukachonga kimeza kidogo cha kuweka kona moja (hakikisha mgeni wako akiketi anakipa mgongo au ubavu) - hapo waweza funika na vitamba (zipo plastics but zinaonekana kama kitambaa) special kwa meza na water resistant. Hicho kitambaa cha plastic cha meza kiwe kinaendana walau na pazia. Hio meza waweza tumia kwa ajili ya kuweka all vyombo related things...

Good luk katika maandalizi... La ziada hizi mvua sisikudanganye fan muhimu.....
Dah! Ninakuelewa sema sisi wa single room changamoto kidogo. Chumba utasema kimepigwa bomu. Hata hivyo, ni tabia zetu zinachangia. Hatujui kuweka makazi smart.

Asante kwa mada nzuri
 
Mje na topic ya kupangilia vyombo kabatini na mpangilio wa jikoni. Wanawake mnatutesa na tabia yenu ya kupenda vyombo vingi.
 
Kitanda kinawekwa katikati ili ukitaka kuamka kwenye kitanda iwe rahisi na sio kukibana kwenye ukuta ikiwa mke au mme akiamka hamna shida yyote na chumba kiwe simple na safi na sio makorokoro .
 
Back
Top Bottom