Jinsi ya kupaka marashi (perfume): Siri 8 za kufanya harufu ya marashi idumu kwa muda mrefu

GokuOne

Senior Member
Jan 19, 2022
197
250
Moja kwa mbili kwenye mada:

100-1009274_transparent-background-perfume-png-png-download.png

1. USIPULIZE KWENYE NGOZI NA KUISUGUA:
Kwa nini?

*Kwa kusugua kwenye ngozi baada ya kupaka kutayafanya marashi yako yapotee (evaporate) kwa haraka zaidi kabla hayajatulia kwenye ngozi na kujichanganya na mafuta asilia ya ngozi (skin oils).

*Kuyatawanya kwa kusugua kwenye ngozi kutasababisha msuguana ambao utaharibu au hata kubadilisha harufu ya marashi. (Bado mupo!!)

2.PULIZA KWENYE SEHEMU ZENYE MAPIGO YA MOYO
Kivipi?

*Ni maeneo ya kwenye ngozi ambapo mishipa ya damu ipo juu zaidi: kama vile ndani ya viganja, kwenye viwiko (elbows), chini ya kitovu, nyuma ya masikio na nyuma ya magoti. Maeneo haya hutoa joto la asili ambalo husambaza harufu kwa uzuri zaidi. Hivyo basi puliza katika maeneo haya na uturi utabaki siku nzima.

3.UHIFADHI NI KIGEZO MUHIMU PIA
Kivipi?

*Usithubutu NARUDIA TENA kwa herufi ndogo usithubutu kuhifadhi kwenye sehemu zenye joto au zipigwe moja kwa moja na mwanga wa jua.

*Yahifadhi kwenye maeneo yenye hali ya ubariidi mbali na mwanga wa jua.

4.PULIZA HEWANI, KISHA INGIA KWENYE WINGU LA MARASHI
Heh heh 😲😮?

*Fanya kama unapiga hatua, ingia kwenye wingu la marashi kisha toka.
*Inasaidia kufanya harufu ikae kwenye mwili wote badala ya kujikita kwenye sehemu moja ya mwili.

5.KUWA HURU KUPULIZA KWENYE NGUO
Hii iko swafi.

*Hakikisha haileti madoa kwenye nguo.
*Puliza hewani kisha pepea nguo zako ili marashi yako yajinyonye kwenye nguo.
*Pia waweza kupulizia kwenye lining ya nguo zako.

6.JIPULIZIE BAADA YA KUOGA
Hii iko wazi kabisa kama pango

*Fanya hivi kwa sababu tundu za ngozi huwa wazi baada ya kuoga na joto litokalo litaisawazisha vyema harufu nzuri kwenye mwili wako.

7.IFANYE NGOZI IWE NA UNYEVUNYEVU
😮😮❓

*Ngozi kavu sana haihifadhi marashi hivyo jaribu kupaka lotion nyepesi au mafuta ya Vaseline, kufanya kunawezesha mafuta ya marashi kitu cha kujishikiza na hivyo kudumu kwa muda kwa mtu aliyejipulizia.

8.PAKAA MCHANGANYIKO WA AINA FULANI TU KWENYE NYWELE ZAKO
❓❓


*Kwa wapenzi wa kuoga marashi kwenye nywele inashauriwa kutojipulizia marashi yenye asili ya alcohol (alcohol based) maana yataharibu nywele na kuzifanya zikatikekatike ILA yenye asili ya maji hayana shida.

NAWASILISHA KWENU WANAJF

AMENO
 

Vicenza

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
806
1,000
Safi sana,nimeipenda hii namba

4.PULIZA HEWANI, KISHA INGIA KWENYE WINGU LA MARASHI
 

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
11,131
2,000
Yote haya ni kazi bure kama perfume ni feki yaani sio original formula. Perfume original au ya kiwango cha juu hutengenezwa kwa mimea asili na mauwa ambayo mafuta yake huvunwa na kuchanganywa na kemikali maalumu za kuituliza harufu nzuri ibalie inapopulizwa.

Perfume ya kiwango cha juu huwa mrija wake haugusi sakafu ya chupa. Yaani ukiona umenunua perfume halafu kale kamrija kamekwenda hadi kugusa chupa kwa chini na kamepinda kabisa jua hayo maji maji ni Synthetic material sio original plants and flower harvested scent.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

ki2c

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
3,579
2,000
Yote haya ni kazi bure kama perfume ni feki yaani sio original formula. Perfume original au ya kiwango cha juu hutengenezwa kwa mimea asili na mauwa ambayo mafuta yake huvunwa na kuchanganywa na kemikali maalumu za kuituliza harufu nzuri ibalie inapopulizwa.

Perfume ya kiwango cha juu huwa mrija wake haugusi sakafu ya chupa. Yaani ukiona umenunua perfume halafu kale kamrija kamekwenda hadi kugusa chupa kwa chini na kamepinda kabisa jua hayo maji maji ni Synthetic material sio original plants and flower harvested scent.

Sent using Jamii Forums mobile app
Fafanua kwa picha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom