Jinsi ya Kuongeza Mvuto wa Chumba cha Kulala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya Kuongeza Mvuto wa Chumba cha Kulala

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Michael Amon, Mar 30, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Chumba cha kulala ni mahali ambapo unapatumia wakati ukiwa umechoka na unahitaji utulivu na pumziko.


  Ni mahali ambapo unahitaji kuondoa ‘stress’ zote na kutuliza mwili na akili, vilevile ni mahali ambapo kwa wewe uliyeolewa unapata faragha ya kutosha kuwa na mume wako.


  Kutokana na umuhimu wa chumba cha kulala basi ni vyema kikawa na mvuto utakaokufanya ujisikie vyema kuwa ndani yake namuonekano wake uchangie katika kukuondolea uchovu na stress.


  Haipendezi kuona chumba kikiwa kimejaa makaratasi, magazeti na vitabu kila mahali bila mpangilio mzuri.


  Weka vitabu na makaratasi yote mahali pamoja na kama unaweza kupata kabati na ukaviweka humo ili chumba kionekane nadhifu na sio kiwe kama maktaba.


  Nguo ziwe zimepangwa vizuri kabatini au sandukuni na zile chafu zikae mahali pake kwenye kapu la nguo chafu. Usiache nguo zinaning’inia kila mahali kwenye milango, madirisha, besele n.k maana inafanya chumba kiwe kimejaa na kuondoa mvuto.


  Chumba cha kulala sio stoo hivyo haipendezi kuhifadhi vitu vya zamani chumbani kama viatu visivyovaliwa, nguo za watoto zisizovaliwa, miavuli, makoti ya mvua, toys za watoto n.k kama kuna ulazima wa kuhifadhi vitu hivi chumbani basi tafuta sanduku la bati na uviweke na kuhifadhi juu ya kabati au mvunguni ili kuondoa mlundikano wa vitu chumbani.


  Kipambe chumba chako kwa maua na mapazia ya kuvutia. usipambe tu sebule na jikoni na kusahau chumba cha kulala.


  Chumba kinaongezeka mvuto pale unapokipamba kwa maua na vessel nzuri, fremu za picha, mapazia mazuri na pia kapeti zuri la kuvutia. Unaweza weka picha yenu mkiwa honeymoon kwenye fremu na kuiweka mezani au ukutani na ikawa pambo zuri sana la chumbani kwenu.


  Wekeza kenye mashuka mazuri na yenye kuvutia. Mashuka mazuri yanakufanya ujisikie vizuri unapokuwa chumbani na vilevile unapokuwa umelala.


  Hakikisha unayafanyia usafi mara kwa mara na kuyabadilisha badilisha sio kila siku mashuka hayo hayo (kauka nikuvae). Wewe pia ni pambo mojawapo la chumba, hakikisha unakuwa na nguo nzuri za kulalia zenye kuvutia na kukufanya ujisikie vizuri na mwenye kuvutia.


  Hasa kwa wale walioolewa ni vyema kuzingatia hili na kuepuka kuvaa ma-tsheti ya zamani na madela kila siku unapoenda kulala au unapokuwa umejipumzisha chumbani.


  E-mail: meezy@youngmaster.co.tz
   
 2. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu umetoa darasa zuri sana kwa wote, wanawake na wanaume. Ni vema tukalielewa hili mwa mapana na marefu yake.
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,262
  Trophy Points: 280
  Sio tu chumbani sio stoo, bali sio museum! Asante kwa kutukumbusha.
  Unafanya kazi za internal decor mkuu? Ungetufahamisha huenda huduma ikahitajika.
   
 4. SALOK

  SALOK JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 2,684
  Likes Received: 880
  Trophy Points: 280
  OK, umetoa somo zuri! shukrani za dhati kwako mkuu! endelea kutukumbusha na mengine yenye faida kama hili.
   
 5. S

  SI unit JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 1,938
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  This is a "super" class! Jf is more than a Social University. Thanks YM, keep it up!
   
 6. Eversmilin Gal

  Eversmilin Gal JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 783
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu asante
   
 7. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,135
  Likes Received: 6,629
  Trophy Points: 280
  tafuta ile picha ya mtoto wa makamba uone chumba cha kulala kinakuwaje. unatuuliza ss wa kwa mtogole hayo tutayajuaje.
   
 8. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Mh. Mabwepande na kwa mfuga Mbwa na room ya hivyo sina hakika. Hii Srade itakua na matumizi .
  Bt Masaki, Obey, Mbezi, na kufananako na huko hii Srade inamatumizi .
  Vinginevyo ina mpangilio mtamu! Nimeipenda .
   
 9. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  lazima leo shem akute chumba kimebadilika...
   
 10. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #10
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Nafurahi sana mkuu kwa kuliona hilo.
   
 11. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #11
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Hapana sifanyi kazi za internal decorarion. Ila nina huo ujuzi cuz my mom and my dad walikuwa wakifanya kazi hiyo for fun ingawa walikuwa na kazi nyingine nzuri za kufanya. So most of the time nilikuwa nao nikijifunza
   
 12. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  :..na kwa majikedume,na madumejike...
   
 13. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #13
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kushukuru mkuu.
   
 14. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #14
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Thanks to you too.
   
 15. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #15
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Au sio?
   
 16. Deejay nasmile

  Deejay nasmile JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,916
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Mi nalalaga ubungo stand.
   
 17. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #17
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Acha masihara mkuu. Mie niko serious ujue.
   
 18. sister

  sister JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,029
  Likes Received: 3,940
  Trophy Points: 280
  na watu tuache kujenga vyumba vidogo utadhani duka, yani mtu sebule kubwa lakini chumba cha kulala kinatosha kitanda tu na ikizidi kabati, chumba kina msongamano wa vitu kama duka. somo zuri i like it mana chumbani ndo ugonjwa wangu.
   
 19. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #19
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Thank you kwa ushauri wako. msg yako imewafikia walengwa.
   
 20. A

  Anne deo JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2012
  Joined: Jul 10, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Thnx,umenisaidia mno.be blecd
   
Loading...