Jinsi ya kuongea unaposhinda Uchaguzi, au unaposhindwa. Chama Tawala na Wapinzani wanapaswa kujifunza

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,442
55,014
Mwanasiasa anaposhinda uchaguzi anatakiwa azungumze kwa namna itakayoteremsha joto la uchaguzi. Hii ni hotuba aliyoitoa Bill Clinton wa Marekani baada ya kushinda uchaguzi.

Nilitaka niweke hotuba ya Obama lakini nadhani ile ina vionjo vya kihistoria.



Aliyeshindwa uchaguzi naye anatakiwa atambue ushindi wa mwenzake, awafute machozi mashabiki wake, na aahidi kushirikiana na walioshinda uchaguzi.

Hotuba aliyotoa John Mccain mwaka 2008 inakubalika kama moja ya nzuri iliyotolewa na mgombea aliyeshindwa uchaguzi.

 
Mambo mengine kufanywa hasa na Watawala wa Afrika ni ngumu sana ,ni Msamiati kwao na hawawezi kuelewa kabisa wao wana waza kutawala tu Mkuu.
 
Kamanda umeambiwa kampeni zimeisha na Watanzania wameshinda. Siasa zinahamia bungeni. Mikutano na maandamano Sasa Basi, tuijenge nchi.
 
Kamanda umeambiwa kampeni zimeisha na Watanzania wameshinda. Siasa zinahamia bungeni. Mikutano na maandamano Sasa Basi, tuijenge nchi.

Kuna namna ya kuwaambia wananchi kuwa Uchaguzi umekwisha. Hotuba nilizozileta ni mifano mizuri ya jinsi ya kuhitimisha zoezi la Uchaguzi.
Na pia kuna namna nzuri ya kuhamishia siasa BUNGENI baada ya Uchaguzi.
 
Ina apply ukishinda kihalali
Na ukishindwa kihalali...

Tanzania tuna mifano ya watu wawili ambao waliwahi kuongea ukweli wakachukiwa
Ingawa ukweli mtupu..

Kitwana Kondo
Iddi Simba..

Hawa baada ya kusambaza pesa hadi wanashinda kuteuliwa na chama na kushinda
Uchaguzi walipofuatwa na waliojifanya waliwasaidia kushinda waliwaeleza ukweli mchungu..

'mimi na nyinyi tumeshamalizana..niliwapa hela mkanipa kura ..msinisumbue..
--- Iddi Simba..

'hamkunichagua nyinyi..pesa yangu ndo imenichagua'
- Kitwana Kondo
 
..sikiliza kwanza hizo hotuba.

..mada yangu inahusu walioshinda na walioshindwa.

..na inawahusu wagombea wa nafasi zote.
Tatizo hawezi kusikiliza kwa sababu ana kazi ya kupitia nyuzi nyingi na kuchafua hali ya hewa. Hii mada siyo level yake huyu.
 
Mshindi feki hana kauli nzuri tangu zama zile.

Ni vile wananchi nao wajinga wakiwa wengi wanaweza mchagua Raisi.

Aliwahi kuwaambia Raia asiye na Mia Tano apige mbizi ,kuhusiana na kivuko cha Kigamboni, akiwa waziri wa miundo mbinu kipindi kile.

Sasa mtu mwenye kauli za hovyo hovyo hawezi toa hotuba itakayowavutia wanazuoni.
 
Wapi nitampata raia mwenzangu Mwana wa Lissu?
Kuna kesi yangu ya shamba nahitaji usaidizi.
 
Ina apply ukishinda kihalali
Na ukishindwa kihalali...

Tanzania tuna mifano ya watu wawili ambao waliwahi kuongea ukweli wakachukiwa
Ingawa ukweli mtupu..

Kitwana Kondo
Iddi Simba..

Hawa baada ya kusambaza pesa hadi wanashinda kuteuliwa na chama na kushinda
Uchaguzi walipofuatwa na waliojifanya waliwasaidia kushinda waliwaeleza ukweli mchungu..

'mimi na nyinyi tumeshamalizana..niliwapa hela mkanipa kura ..msinisumbue..
--- Iddi Simba..

'hamkunichagua nyinyi..pesa yangu ndo imenichagua'
- Kitwana Kondo
Hiyo ya Kitwana Kondo ilikuwa mbaya sana kwa sababu watu wa Kigamboni walimtema Masudi aliyewapigania sana kwenye suala la Kivuko. Nakumbuka alikataa kurudisha shilingi yake kwenye bajeti ya wizara ya ujenzi mpaka Mustafa Nyang'anyi alipomhakikishia upatikanaji wa kivuko cha uhakika. Alikataa hata alipowekwa mtu kati kwenye kikao cha chama. Watu wake wakamsaliti baada ya Kitwana Kondo kuwapa kanga na pilau!

Amandla...
 
Back
Top Bottom