Jinsi Ya Kumwacha Mpenzi Wako Kwa Amani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi Ya Kumwacha Mpenzi Wako Kwa Amani

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Superman, Feb 26, 2012.

 1. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145

  [​IMG]

  Ziko njia mbili tu ambazo uhusiano baina ya wapenzi wawili utaandika historia. Ama uhusiano utadumu hadi kifo kiwatenganishe ama utavunjika. Hata hivyo uzoefu unaonyesha kuwa kwa walio wengi hawajaweza kuwa kwenye uhusiano wa kudumu, wanakuwa wamepitia katika mahusiano mengine na hivyo kupitia awamu Fulani Fulani za kuvunja mahusiano.Na kuna namna mbili ambazo uhusiano utavunjika. Ama kwa amani ama kwa ugomvi.

  [​IMG]

  Kumaliza mahusiano si kitu rahisi sana hata kama ni hakika umemchoka mwenzi wako na hata kama uhusiano wenu si mzuri kiasi kwamba uko tayari kuwa huru. Kwa hiyo basi, kuvunja mahusiano ya kimapenzi ni jambo ambalo haliwezi kuepukika. Hata hivyo kumaliza mahusiano kwa amani ni vizuri na inapendeza kuliko kuumaliza kwa ugomvi na jazba. Kumbuka "The Golden Rule": Kwamba ungekuwa ni wewe ungependa uachwe vipi? Kama upo katika mahusiano yasiyo na tija na unafikiri kwamba imefika wakati unahitaji uhusiano wenu uvunjike, basi dondoo zifuatazo zitakusaidia kumaliza mahusiano na mpenzi wako kwa amani. Kitu kimoja kikubwa cha kuzingatia ni kuweka Jazba pembeni:

  [​IMG]

  1. Kuwa Na Uhakika Na Unachotaka Kufanya: Kama huna uhakika juu ya hisia zako kwa mwenzi wako unapotaka kuvunja uhusiano bora usifanye hivyo maana utafanya moyo wako usiwe na maamuzi dhabiti aka "Maamuzi magumu". Kama una hisia naye pia itamfanya achanganyikiwe na ajisikie kuwa bado anayo nafasi ya kuwa na wewe ama anaweza akaamua na yeye kukukomoa na kukuacha kabisa wakati kumbe bado una hisia za mapenzi na yeye . Hata hivyo kama una uhakika kwamba ni kweli hauutaki uhusiano uliopo basi kuwa tayari kukata kabisa mahusiano yenu la sivyo kuwa tayari kukiona cha moto . . . maana utakuwa unachezea hisia zako.

  [​IMG]

  2. Fikiria Sababu za Kuvunja Uhusiano: Uhusiano unapovunjika mara nyingi ndugu, jamaa na marafiki wanapenda kujua sababu. Unapojua sababu zinazopelekea wewe kuvunja mahusiano itakusaidia kutoa majibu ya uaminifu pale unapoulizwa. Pia itakusaidia kumaliza mahusiano katika namna njema. Hata kama mwenzi wako hataamini au ataamini juu ya kuvunjika kwa uhusiano wenu, kuwa honest au mkweli ni muhimu. Mweleze unahitaji kusonga mbele na maisha yako bila yeye na mjibu maswali yote kwa uaminifu. (Fikiria huko nyuma kama uliwahi kuachwa bila sababu ulivyojisikia)

  [​IMG]

  3. Maliza Mahusiano Wewe Binafsi: Kama umekuwa na mpenzi wako kwa muda mrefu au kuipindi chochote ambacho uliwekeza muda na nguvu zako za kujenga mapenzi, basi ni busara mahusiano hayo yakamalizwa na mwenyewe binafsi. Usitumie njia yoyote ile zaidi ya wewe mwenyewe, usitumie SMS, usitumie IM "Chat", usitumie simu au email au barua au mtu yeyote kufikisha ujumbe. Ukitaka kumaliza mahusiano kwa amani, tafuta muda wa kukaa na mwenzi wako in person au face to face ili kuumaliza uhusiano huo katika hali njema.

  [​IMG]

  4. Chagua Mahali Panapofaa. Mahali pazuri panapofaa ni pale ambapo wewe unayetaka kumwacha mwenzako ungekuwa wewe unaachwa ungependa iwe mahali gani ili uelezwe? Be on his/her shoes. Public Places si mahali pazuri sana kwani mwenzi wako anaweza kujisikia kadhalilishwa. Kama ukiweza chagua mahali patakapomfanya mwenzi wako awe confortable na kurelax kama yuko nyumbani kwake.

  [​IMG]

  Angalizo: Kama una uhakika kuwa mwenzi wako anaweza kuleta ukorofi, basi chagua Public Place kama kwenye restaurant ambapo wapo watu wengine. Hii itasaidia kuondoa uwezekano wa kuleta vurugu. Public Place patakufanya ujiamini. Pale mambo yatakapochachamaa unaweza kuondoka tu bila tishio la ugomvi kwa kuwa kuna watu. Ukiona hali si shwari ni vema uanze kuondoka wewe kuliko yeye kuondoka kwanza.

  [​IMG]

  5. Msikilize Mwenzi Wako: Hata kama umeshaamua huwezi kubadili mawazo juu ya kuvunja mahusiano yenu haina maana kuwa usimsikilize mwenzi wako. Kumsikiliza mwenzi wako kutamfanya mwenzi wako atoe yote aliyokuwa nayo moyoni kitu ambacho kwa uhakika kitasaidia kumaliza mahusiano kwa amani. Pia unaweza kujifunza baadhi ya mambo ambayo yatakusaidia katika mahusiano yako yanayofuata.

  [​IMG]

  6. Kuwa Mpole Na Dhibiti Hisia Zako: Moja ya sababu kubwa ya mahusiano kuvunjika ni pamoja na wahusika wote kutokuwa na furaha na amani na mwenzi wako. Wakati wa kuvunja mahusiano hayo pia yanaweza kujitokeza hasa pale mtakapoanza kulaumiana na kuonyeshana vidole ni nani mwenye makosa. Hakikikisha unadhibiti hasira hisia zako na hasira hata kama anachoongelea mwenzio kitakutia hasira. Ukifanya hivyo utafanikisha kuwa na mazungumzo ya amani.

  [​IMG]

  7. Kuwa Mtulivu na Makini: Unahitaji kuumaliza uhusiano na kuondoka mahali mlipo. Hata hivyo ni busara kuwa mtaratibu na mpole. Kama kuvunjika kwa uhusiano wenu kutakuja kama Suprize kwa mwenzio, basi bila ya shaka atahitaji muda wa kuyameza unayomwambia, kuyatafakari ili aende sambamba na wewe katika mazungumzo yenu. Inaweza ikawa si habari njema kwa mwenzi wako kwa hiyo utulivu wako na upole katika maongezi yenu kutamfanya apunguze maumivu.

  [​IMG]

  8. Mkimaliza Maongezi Ondoka Haraka: Iko hivi: Kwa kiasi kikubwa anayeachwa anaweza kuwa alikuwa hajui kuwa ataachwa kwa hiyo hatakuwa na furaha kwa yeye kuachwa. Anaweza akakulaani sana na kukuita majina yote mabaya anayoyajua na hivyo kukufanya na wewe uwe na hasira. Tulia. Jizuie. Kwa kuwa umeshaongea na pia umemsikiliza kistaarabu, huna haja ya kuendekeza ugomvi au malumbano. Ondoka. Hakuna faida utakayoipata kwa kuendelea kutoa maelezo yoyote ya ziada. Kama ni mwelewa na mmemaliza maongezi kwa amani basi mwage na nenda zako.

  [​IMG]

  Je, ni nini uzoefu wako kuhusu kuacha au kuachwa katika mahusiano mbalimbali uliyopitia? Na je, kuna lolote la kujifunza?


  Nawakilisha Na Nitarudi Kuna Mdada wa JF kaomba lift:

  [​IMG]
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  asante kwa muongozo mzuri.

  Ila kama umependa, kuachwa ni kuachwa tu hata upelekwe trafangasi skwea.

  Kuna mtu aliachwa akapewa kitu fulani akakikataa vile vile.
   
 3. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kuachwa ni shughuli pevu. Hata hivyo mwongozo huu ni wa kuachana kwa amani. Umewahi kuacha au kuachwa? tupe uzoefu wako Kongosho.
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  sikumbuki hata idadi ya nlioacha na kuniacha.
  Ila kuna mmoja alikuwa mwanafunzi wa chuo.

  Dah, binti alikuwa mapepe huyo, nlivyomstukia nilimpiga chini mbaya.
  Badae nilijilaumu maana ilikuwa kipindi cha mitihani, kidogo adisko.
  Nilimfuata chuoni nimejaa hasira, nikampa live hapo hapo, huyo nikadandia usafiri na kuondoka.

  Ila poa tulishasahau ya kale, angalau tunasalimiana siku hizi.

  Sikutumia busara, ningeweza subiri.
   
 5. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  aisee, yaani kumpiga mtu kibuti unahitaji maelezo yote haya? mbona ni issue simpo tu..
   
 6. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Du Mkuu, nimecheka sana. Alikufanya nini hata ukampiga chni? Au mambo ya halua halua?
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,903
  Trophy Points: 280

  Kama kulikuwa na mapenzi ya kweli kwa wahusika wote basi kuachana kwa amani ni nadra sana.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Tunazungumzia kumpiga mtu kibuti kwa amani. Wengine ni vigumu kuwaacha.

  Tupe uzoefu wako basi uliwahi kupigwa kibuti au kupiga kibuti namna gani?
   
 9. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Nimekusoma Kiongozi wangu.

  Huwa inakuwa ngumu kwa sababu wengi hawajui ABC zake. Vipi uzoefu wako niaje Mkuu?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. +255

  +255 JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,909
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Hy namba 3, ndo imenikuta jana jioni..Alinipigia simu nimkute sehemu nikaenda akanieleza sababu za kutaka kuachana na mimi bahati nzuri sababu zake niliziona ka zina maana kidogo, pamoja na kuwa nae karibu miaka 4.Ila hii issue nilihisi itakuja kutokea tatizo nilikuwa sijui ni lini?!
   
 11. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  goodnite,sitaki kutia neno hapa,ila kama kuna mtu atamwona Lizzy basi amwambie namsalimia,
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,903
  Trophy Points: 280
  Inawezekana Mkuu kuachana kwa "amani" lakini inahitaji wahusika wawe wastaarabu wa hali ya juu, kitu ambacho ni nadra sana hasa kama mapenzi yalikuwa yamekolea.
   
 13. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  hakuna kuremba... just tell him/her "it's over between us" na kila mtu anachukua time yake right there and then...
   
 14. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mkuu ushapigwa chini nini? Tueleze vizuri.
   
 15. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Duuh! Miaka 4 ni mingi sana. Ilikuwaje Mkuu?
   
 16. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe Mkuu.

  Zali lako na kuacha au kuachwa huko nyuma lilikuwaje?
   
 17. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #17
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Unamwambia wapi?
  Lini?
  Kwa sababu zipi?
  nk

  Will all end up katika mwongozo huu. Mwishoni ni amani au no amani depends on how both handle the break up
   
 18. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #18
  Feb 26, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wewe Superman acha hizo! Siamini katika kuacha au kuachwa kwa amani. Kuacha ni kuacha tu! Na kuachwa vivyo hivyo! Hilo suala la kuachwa kwa amani lilinitokea zaidi ya mara moja lakini na mtu huyo huyo! Yaani kabla sijapona maumivu ya kuniacha anarudi kuomba msamaha na mie kwa vile nakuwa bado nampenda sana naona yanini kuendelea kuumia bora nimsamehe niwe na amani.
  Hakuna nafuu yoyote katika kuacha au kuachwa kwa amani. Maumivu kwa upande mmoja yapo pale pale.
  Tena bora pawe na shari, hiyo ya amani inakuja kuwaumiza wote wawili maana muachaji wakati mwingine hujiona na makosa au hujisikia vibaya kumuumiza aliyemuacha kama hakukuwa na sababu ya msingi bali ni tamaa tu.

  Usiku mwema. Kuna mkaka wa JF ana beep!
   
 19. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #19
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mkuu MwaJ, kwanza pole sana kwa hilo bandage lako nadhani ni PoP, mara nyingi nakuona nalo bado tu hujapona. Halafu huo ni Mguu au Mkono? Duh! Duniani kuna mambo.

  Tukije katika issue yako; huyo mwenzi wako hakuwa ameweka maamuzi sahihi. So No. 1 inahusika:

  1. Kuwa Na Uhakika Na Unachotaka Kufanya: Kama huna uhakika juu ya hisia zako kwa mwenzi wako unapotaka kuvunja uhusiano bora usifanye hivyo maana utafanya moyo wako usiwe na maamuzi dhabiti aka "Maamuzi magumu". Kama una hisia naye pia itamfanya achanganyikiwe na ajisikie kuwa bado anayo nafasi ya kuwa na wewe ama anaweza akaamua na yeye kukukomoa na kukuacha kabisa wakati kumbe bado una hisia za mapenzi na yeye . Hata hivyo kama una uhakika kwamba ni kweli hauutaki uhusiano uliopo basi kuwa tayari kukata kabisa mahusiano yenu la sivyo kuwa tayari kukiona cha moto . . . maana utakuwa unachezea hisia zako.

  Na bado katika kukuacha anweza akawa alitumia moja kati ya njia hizo. ama?

  Halafu hebu tuambie ilikuwaje? Achana na Maanko wa JF saa hizi. Utaachwa shauri yako.
   
 20. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #20
  Feb 26, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Superman achana na POP langu, tarehe ya kwenda kulifungua haijafika bado.

  Hadith ndefu sana. Nikiifungua atanishtukia maana ni member wa JF.
   
Loading...