Jinsi ya kumuondoa CAG madarakani

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,034
114,447
Ibara ya 144(2) ya Katiba, CAG anaweza kuondolewa madarakani kwa sababu tu ya kukosa uwezo wa kufanya majukumu yake(kwa ugonjwa ama sababu nyingine) au kwa utofu wa nidhamu au kwa kukiuka sheria za maadili za viongozi. Na hataondolewa isipokuwa kwa mujibu wa Ibara ya 144(4)

Rais akitaka kumuondoa CAG ataunda Tume ya Kijaji, Special Tribunal, na itakuwa na mwenyekiti na wajumbe wengine wasiopungua wawili. Mwenyekiti na wajumbe wasiopungua wawili watakuwa ni watu ambao ni majaji au waliowahi kuwa majaji wa Mahakama Kuu au mahakama ya rufani katika nchi yeyote kati ya nchi za Jumuia ya Madola.

Special Tribunal itafanyia ufukunyuzi na kuwasilisha taarifa kwa Rais ikimshauri kumwondoa au kutokumwondoa CAG

Kwa hiyo badala ya kumkwamisha Mzee wa watu ni bora mkamuondoa kwa taratibu hizo nilizoziainisha hapo juu ambazo ni kwa mujibu wa katiba.
Bajeti ya Ofisi ya CAG inasikitisha sana........................................inatia hasira
 
Serikali inayojiita makini na inayopigania maslahi ya umma....kwa muda huu na hapa walipoifikisha nchi yetu.....wangetakiwa waanze kuifanyia kazi ripoti ya CAG mara moja na sio kumkwamisha.....
 
so CAG atashindwa kkutimiza majukumu yake kwa 50% au, vipi mkuu sisi wa audit firms mtatu outsource kama miaka ya nyuma au mnapiga kila kitu wenyewe mwaka huu, maana msipo out source huku kuna ma auditor wastaafu tulikuwa tuki wasub contract watakosa pa kula
 
so CAG atashindwa kkutimiza majukumu yake kwa 50% au, vipi mkuu sisi wa audit firms mtatu outsource kama miaka ya nyuma au mnapiga kila kitu wenyewe mwaka huu, maana msipo out source huku kuna ma auditor wastaafu tulikuwa tuki wasub contract watakosa pa kula
mkuu tutakamua wenyewe,18b ni ndogo sana,ofice expenses humohumo,tutapata wapi za ku-outsource?
 
Kama kweli anavyosema anataka kupambana na ufisadi kwa nini asiiwezeshe ofisi ya CAG kwa bajeti ya kukidhi shughuli zake 100%? Huwezi kumtengua miguu CAG kisha ukategemea kufichua ufisadi hata kidogo. Mkuu anadhani atapambana na ufisadi kwa kutegemea ripoti za majungu anazoletewa kwa SMS?
Miezi sita hii imeonyesha sura halisi ya awamu ya tano kuwa ni usanii wa kiwango cha lami.
 
wanataka kumuondoa kwasababu sio mzalendo kwenye hicho kitu...in other words: ANATUMIKA.
Huenda ukawa sahihi lakini hujasema anatumikaje na ni nani anamtumia? Au hamkufurahishwa na lugumi scandal iliyoondoka na waziri japo imepoozwa kwa sasa? Au kuna mahali mlishapiga za kutosha ila hamtaki awaumbue?
 
kama bajeti haitotekelezeka hapo ndo CAG anatakiwa kuonyesha uzalendo wake kwa kujiuzuru. kinyume na hapo na yy ni mpigaji kama wengine. kwanza ofisi yake ni moja kati ya ofisi za serikal inayohusishwa na rushwa.
 
Back
Top Bottom