Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,534
Jinsi ya kumsaidia mtoto aliyefiwa na mzazi/mlezi/mtu wake wa karibu.(Imetoka kwenye kitabu "35 Ways to Help a Grieving Child")
Vifo hutokea kila siku kwenye jamii na watu huomboleza vifo hivyo kwa njia tofauti. Inapotokea marehemu ameacha mtoto au ndugu wa karibu mwenye umri mdogo simanzi nyingi huwajaa waombolezaji kwa kumhurumia mtoto yule na maisha yake yajayo. Lakini kinachosahaulika ni hisia za mtoto yule kuhusu kifo cha mpendwa wake. Tunaweza tukadhani kuwa mtoto yule haumii kwakuwa ni mdogo na haelewi kilichotokea lakini mara nyingi dhana zetu si kweli kwani watoto wana maumivu makubwa yanayochangiwa na kushindwa kwao kuelezea machungu yao kiufasaha.
Zifuatazo ni baadhi ya njia zinazoweza kutumika kumsaidia mtoto aliyefiwa ama kupotelewa na mtu wake wa karibu.
1. Jibu maswali yote anayouliza, hata yale magumu.
Watoto hujifunza kwa kuuliza maswali. Wanapouliza swali ni dhahiri kuwa wana shauku ya kuhusu kitu wasichokielewa. Mfanye ajue kuwa ni sawa kuuliza swali lolote. Mpe majibu ya ukweli lakini angalia lugha unayotumia. Tumia lugha itakayompa picha halisi ya kilichotokea Mfano; Kusema "baba ameenda Mbinguni au baba ameondoka" huweza kuleta taswira kuwa atarejea au anahitaji kutafutwa na badala yake "baba amefariki au amekufa" hupaswa kutumika.
2. Mpe nafasi ya kuchagua na kushiriki katika msiba.
Watoto hupenda kupewa nafasi ya kuchagua na hujiona wenye thamani. Mtoto asitengwe katika kufanya maamuzi bali ashirikishwe katika shughuli nzima ya kupanga mazishi ili aweze kujihisi kama sehemu ya shughuli hiyo ya kumuaga mpendwa wake. Watoto wa familia moja huweza kuwa na machaguo tofauti ya njia za kushiriki katika msiba hivyo ni vizuri mtoto akasikilizwa na kukubaliwa kushiriki kwa njia imfaayo Mfano; Mtoto A anaweza kutaka kuongea kitu mbele ya watu wote kwenye msiba wa mzazi wake na mtoto B anaweza kutaka kuaga mwili wa marehemu na kusema maneno yake hapo.
3. Muongelee na kumkumbuka mtu aliyefariki.
Kumuongelea mtu aliyefariki katika maongezi ya kawaida humpa mtoto ruhusa ya kuzisema hisia zake bila woga na kuona sio mwiko kumuongelea mtu aliyefariki.Hii pia humpa mtoto muda wa kufurahia kumbukumbu zote nzuri alizokuwa nazo na mtu wake wa karibu na kujua kuwa mtu anaweza kufariki lakini upendo wake ukaishi milele.
Watoto pia hupenda kuhifadhi vitu vitakavyowakumbusha kuhusu watu wao wa karibu hivyo ni vema waruhusiwe kuwa navyo na kuvitumia badala ya kuondoa kila kumbukumbu ya marehemu.
4. Heshimu tofauti katika namna za kuomboleza.
Watoto huomboleza tofauti na watu wazima na kila mtoto katika familia anaweza kuwa na namna yake ya kuomboleza. Wengine hupenda kuelezea machungu yao wakati wengine hupendelea kuwa peke yao. Wengine hupendelea kuwa busy na mambo yao ya shule au michezo wakati wengine hupenda kuacha kufanya chochote na kukaa tu nyumbani. Kutambua na kuheshimu uhuru huu wa kuomboleza kwa watoto ni muhimu katika kuhakikisha kupona kwa machungu yaliyosababishwa na msiba. Msikilize mtoto kwa makini na angalia mwenendo wake ili kutambua tofauti hizi.
5. Sikiliza bila kuhukumu.
Moja kati ya vitu vinavyoweza kumsaidia mtoto ni kumsikiliza bila kumhukumu,kumshauri au kukimbilia kumrekebisha. Unaweza kudhani unamsaidia mtoto kwa kutumia maneno kama "najua unavyojisikia" au "sahau na usonge mbele" lakini maneno haya hupokewa na mtoto kama ukinzani kwa hisia zake au jaribio la kufanya kile anachohisi kisiwe na maana. Cha kufanya ni kutumia maneno yanayoendana na yao na kuuliza maswali yatakayopelekea mtoto kujieleza zaidi Mfano; Mtoto anaweza kusema "Namkumbuka sana baba yangu",unaweza kumwambia "Unajisikiaje ukimkumbuka?" hii hupelekea kuhisi kuwa kile wanachohisi ni sahihi na kuona wako mikono salama.
6. Andaa Shughuli ya Kumbukumbu.
Shughuli ya kumbukumbu kila mwaka humsaidia mtoto kukomaza bond iliyopo kati yake na mtu wake wa karibu aliyefariki. Kabla ya shughuli hiyo wataarifu watoto kuhusu nini kitafanyika na kama watahitaji kushiriki. Na kama wasingependa kushiriki waruhusu watoe mawazo yao ya nini kifanyike kama mbadala. Wanaweza kuchagua kufanya kitu kitakachowafanya wajisikie karibu na mpendwa wao. Mfano; Kama mama alipenda kuwapeleka watoto kijijini kwa bibi yao mara moja kwa mwaka, watoto wanaweza kupendelea kuendelea kwenda kila mwaka kama Kumbukumbu kwa mama yao.