Jinsi ya kumkosanisha Rais Samia na Watanzania na kumfanya achukiwe: Tozo za Serikali, Katiba Mpya, Uonevu wa Polisi, Mambo ya Muungano

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Unapokuwa kiongozi, hasa wa siasa, unapaswa kuwa makini sana hasa na viongozi ambao watajifanya ni rafiki zako kumbe wanatafuta tu namna ya kukuchonganisha na wananchi. Na hili namwambia wazi Raisi Samia ajihahdari sana. Sifikiri kwamba viongozi wote, na hasa wateule wake, wapo pamoja naye siku zote kama ambavyo wanamfanya aamini.

Wapo viongozi ambao watamwambia Raisi Samia sisi tuko nyuma yako twende tu mama - lakini anapaswa kuwaambia wazi huko nyuma yangu mnafanya nini, njooni tuwe bega kwa bega ili nione mnachofanya.

Kuna mambo ya msingi manne ambayo Raisi Samia anapaswa kuwa nayo makini sana. Haya ni mambo ambayo yatamfanya aungwe mkono au kuchukiwa na wananchi kwa ujumla. Haya mambo ni;
  1. Suala la tozo/kodi za serikali
  2. Suala la Katiba mpya
  3. Suala la uonevu wa Polisi (pamoja na haki za binadamu)
  4. Mambo ya Muungano
Katika haya manne, nakuambia wazi Raisi Ramia, tread with care, la sivyo yanaweza kukuharibia sana rekodi yako ya uongozi wa Tanzania. Usiwe mwepesi kupokea ushauri wa wateule wako juu ya mambo haya manne, wasikilize, na kama ikibidi kupata ushauri ni vema upate ushauri nje ya watu wanaokuzunguka, wasio na maslahi ya moja kwa moja katika uamuzi wako juu ya hayo mambo. Na pia, lolote utakaloamua weka Tanzania na Watanzania first without separating the two. A seemingly good thing for Tanzania might not be a good thing for Tanzanians, and vice versa.

Acha matamko ya harakaharaka juu ya mambo haya, tafakari kwa makini kabla hujaongea lolote kuyahusu. Na sio lazima uende na masimamo wa chama chako katika haya mambo manne. Wapo wanaokuzunguka watakaotaka kukukaanga kwa mafuta yako mwenyewe kupitia haya mambo manne kwa kutumia moto wa chama chako - be warned.
 
Washamvuruga tayari.

Mimi kama MwanaCCM niliona haya yanakuja na kibaya zaidi nimeona yanakuja mengi sana. Sababu ya yeye kufanyiwa hivi zinaweza kuwa...

1. Aonekane ni Rais aliyeshindwa hasa kwa kuzingatia gender yake.

2. Waliomzunguka wana agenda yao ya siri.

3. Watangulizi kujaribu kulinda rekodi zao.
 
Hahahha... Naona sasa hivi kuna kampeni imeanzishwa ionekane Samia hahusiki na madudu yeyote katika selikali yake ila kuna watu wamemzunguka ndio wanamkosesha!
 
Hahahha... Naona sasa hivi kuna kampeni imeanzishwa ionekane Samia hahusiki na madudu yeyote katika selikali yake ila kuna watu wamemzunguka ndio wanamkosesha!
Hapana, hawezi kukwepa kuhusika. Yeye ndio raisi, na hivyo itakuwa ni mwendawazimu tu ambaye atashawishiwa kwamba Raisi Samia hahusiki na maamuzi ya serikali. Mwenye ultimate decision ya maamuzi yeyote ya serikali ni yeye, na hasa ukizingatia yeye ni Raisi wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM.
 
Hapo namba 3 Polisi wanaucheza mwingi sana yaani wanatusaidia kuisagia kunguni CCM na Serikali yake.
 
Hahahha... Naona sasa hivi kuna kampeni imeanzishwa ionekane Samia hahusiki na madudu yeyote katika selikali yake ila kuna watu wamemzunguka ndio wanamkosesha!
Mmojawapo ni wewe. Si ni juzi tu ulikuwa unaunga mkono tozo bibie?
 
Namba 2 na namb 3 ni upuuzi mtupu. Najua namb 2 inataka kutumiwa na upinzani kama kichaka cha kupiga hela kupitia vikao vya bunge la katiba na ukizingatia kuwa sasa hivi wapinzan wako hoi mifukoni kutokana na kupoteza viti vingi vya ubunge, huku ile ruzuku ya wabunge wa viti maalum ikiliwa na mwenyekiti akishirikiana na wajanja wachache ndan ya chama.

Namb 3 hii ishazoeleka kwa wapinzani kuvunja sheria au kujaribu kuhatarisha amani, afu wakidhibitiwa na vyombo vya dola wanakuja huku mitandaoni kulia lia japo hii mbinu chakavu haijawahi kuwasaidia kushika nchi kwan wananchi wa leo sio wa miaka ya 80 ambapo mtu alikuwa akifatilia habari mbali mbali kupitia kweny TV yake, halafu asubuhi anakuja kusema kuwa ameoteshwa kuwa kuna jambo linatokea, au litakuja kutokea sehem fulani. Watanzania wa dunia ya leo wanafatilia kila kitu na kujua ukweli uko wapi, isipokuwa wale ambao wamemkabidhi mwenyekiti akili zao atembee nazo mfukoni ndio wanaonasa katika mtego huo.

Kwahiyo kuchukiwa na baadhi ya wachumia tumbo wa upinzani hakutampunguzia madaraka yake, wala kumnyong'onyesha kwa namna yoyote ile... Mama endelea kutumia miguu yote ili maadui zako wasijue unapigia mguu gani.
 
Hahahha... Naona sasa hivi kuna kampeni imeanzishwa ionekane Samia hahusiki na madudu yeyote katika selikali yake ila kuna watu wamemzunguka ndio wanamkosesha!
Tena wa Kwanza kuwatazama wawe Wana Sgang.
 
Unapokuwa kiongozi, hasa wa siasa, unapaswa kuwa makini sana hasa na viongozi ambao watajifanya ni rafiki zako kumbe wanatafuta tu namna ya kukuchonganisha na wananchi...
Umesema kweli tupu...

Sijui ni kwanini tu Rais Samia Suluhu Hassani na baadhi ya wanaomsaidia hawajifunzi toka kwa Mwendazake...

Mwendazake John Pombe Magufuli hakuwa mtu wa kufa jana wala kesho...

Lakini kwa sababu ya "ujinga" na "upumbavu" wake aliamua yeye mwenyewe kujiharakishia kifo chake kwa kukubali kuzungukwa na mahayawani ambao mwisho wake haohao wakamuua...

Na aliuwawa kwa sababu moja tu kubwa, kukubali kufuata ushauri wa kukandamiza haki za watu wa Mungu aliopewa dhamana ya kuwaongoza kwa niaba ya Mungu mwenyewe.

Ni Bahati mbaya kuwa, huyu mama anaelekea na kufuata mkondo huo huo. HAKIKA ANAPASWA KUAMKA MAPEMA, VINGINEVYO HATA YEYE ATAKUFA KABLA YA WAKATI.
 
Huyu mama katuonyesha rangi yake halisi

Magufuli mwamba wa Africa atakumbukwa na wanyonge wengi amini nawambia na Sasa Ni zama za mabeberu wa matumbo
 
Sanasana watu ndo watamuonea huruma tu.

Wanajua Watanzania wengine vichwa maji
 
Back
Top Bottom