Jinsi ya kukumbuka eneo uliloegesha gari lako kwa kutumia simu yako

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,118
️Unawezaje kukumbuka sehemu uliyo-pack gari au kifaa chako kwa kutumia Google Assistant

Hakuna kitu kibaya kama kusahau sehemu uliyo-pack gari/kifaa chako lakini kwa bahati nzuri kama una iPhone, iPad au Android smartphone unaweza kukumbuka kwa urahisi

️Tuanze kuangalia Google Assistant kwa Android

Kitu cha kwanza unachotakiwa kukifanya ni kuhakikisha Google Assistant ina-acess location yako kwenye simu yako

Unatakiwa ku-enable location/ weka location ON

Settings >> location >> use location >> switch on
Baada ya hapo, unatakiwa kufungua Google Assistant kwenye simu yako [ Make sure uko sehemu ya Parking/sehemu unapoacha gari/kifaa chako ]

Kuna namna mbili za kufungua Google Assistant kwa Android smartphone

️sema "Okay, Google” au “Hey, Google.”
️Kwa wanaotumia Android 10 na kuendelea unaweza ku-swipe either chini kwenye kona ya kulia au kushoto

️Baada ya Google Assistant kufungua na kusikiliza unatakiwa kusema yafuatayo

“I parked here.”

“Remember where I parked"

Hapo Google Assistant itakumbuka sehemu uliyo-pack na kuweka
Kwenye Google Maps

Baadae ukirudi kutaka kujua sehemu uliyo-pack, fungua Google Assistant kisha sema moja kati ya hizi command

“Where’s my car?”

“Where did I park?”

“Find my car’s location"

Google Maps itafunguka na kukuonyesha sehemu uliyo-pack, nenda kachukue gari yako

Kwa iPhone na iPad
️Google Assistant kwa iPhone au iPad

Kabla ya kuanza kutumia Google Assistant Hakikisha "Location services" iko ON [location services is enabled ]

Settings >> privacy >> Location services [ put it ON ]

Baada ya hapo fungua App ya Google Assistant
Baada ya kufungua app unaweza kusema “Okay, Google" au bofya kwenye "Microphone" icon

Ikiwa Google Assistant inasikiliza, sema moja kati ya hizi command

“I parked here.”

“Remember where I parked.”

Google Assistant itasave parking location kwenye Google Maps.
Baada ya kazi zako kama ukitaka kujua sehemu uliyo-pack gari,

Fungua Google Assistant app kisha sema moja kati ya hizi command

“Where’s my car?”

“Where did I park?”

“Find my car’s location

Map itafunguka na kuonyesha sehemu uliyopack gari

Asanteni

Uzi under @
 
Asante, nimefanikiwa kuondoka na gari ya mchuchu kila siku namwambia niazime gari nioshe mjini hataki. Ila tukienda mahali akipaki ananipa funguo nikae nao kwenye pochi.

Nimemwambia naenda msalani kisha nikaenda kufanya majaribio waalah imekubali.

Nusu saa ijayo namuachia manyoya....😅

Yeeyooooh
 
️Unawezaje kukumbuka sehemu uliyo-pack gari au kifaa chako kwa kutumia Google Assistant

Hakuna kitu kibaya kama kusahau sehemu uliyo-pack gari/kifaa chako lakini kwa bahati nzuri kama una iPhone, iPad au Android smartphone unaweza kukumbuka kwa urahisi..
Watanzania mmeanza kuwa matajiri, yaani mnasahau hata ni wapi mlipopaki magari yenu!?
 
Very useful

Mnaoshangaa kua unawezaje kusahau ulipopaki it happens sometimes....kwa sie wenye vichwa vizito.

Nilishawahi peleka mtu airport wakati narudi nikawa nimejichanganya sijui gari nimeacha kwenye lane ipi aisee nikaenda kufata gari identical na yangu....aibuuu af mtu anaweza hisi kibaka

Again kwa sehemu kama kariakoo naweza kupaki nikaweka alama zangu kabisaaaaa kua nimepaki karibu na landmark flani ila nikazunguka weeeeeeeee hadi location nasahau (it seriously happens au mi mzito sana?Sijui).....japo siku hizi nimepata mbinu ya kupaki Anatoglo kule

Asante lakini wacha tuongeze matumizi ya simu tutoe ushamba....
 
Very useful

Mnaoshangaa kua unawezaje kusahau ulipopaki it happens sometimes....kwa sie wenye vichwa vizito...
Hahaha watu hawajui tu ukiwa unamiliki sare ya taifa IST halafu upaki sehemu kama kariakoo au parking ambayo ina magari mengi unaweza kujikuta unataka kuondoka na gari la mtu 😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom