Jinsi ya kukopa bank wa biashara ya usafirishaji.

Chiwaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
5,571
2,000
Habari wana JF,
Naomba nikili kuwa hali yangu kiuchumi sio nzuri, na hasa baada ya kuingia white house huyu mzee wa Geita. Naona mambo kama vile yamefungwa kwa makufuli yasiyofunguka.

Kwa kawaida mimi huwa ni mfanyabishara wa biashara ya kuagiza kutoka nje ya Nchi. Kutokana na kila sehemu ya kuingizia mizigo kuwa hazieleweki, nafikiria kubadili biashara kwa kujiingiza kwenye bishara ya usafirishaji, hasa kwa kutumia magari makubwa(Truck/Lorry/Tandam au hata Vipisi).
Tatizo ni kuwa sina Cash, ila naviji assets kama vile nyumba(Zenye Hati na zisizo na Hati), wake.

Ninahitaji Bank waniwezeshe, naombeni mawazo ya jinsi ya kuanza kuchakalikia huo mkopo.
 
Ngwananzengo

JF-Expert Member
Jul 28, 2012
1,911
2,000
Ni NGUMU kupewa mkopo benki sababu mkopo wa benki mara nyingi kama sio zote huwa ni kwa ajili ya kuendeleza biashara. Wao kukukopesha wewe ni kujiingiza kwenye "Risk" kubwa.

Tafuta jinsi uianze hiyo biashara hata kwa kuuza "nyumba yako". Biashara ikisimama watafute benki.

NB: Benki si rafiki wa watu maskini.
 
JembePoli

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
1,323
2,000
Umeshazijua changamoto za usafirishaji mkuu.
Muhimu kujua zamana za mzigo ziko kwako kama afisa usafirishaji inakoma pale tu mzigo unapomfikia muhusika.
Lkn unaweza kuanza kwa kutumia Lori za kukodi ukapakia mizigo ya wafanya biashara wa kati japo ni kazi kidogo maana itakubidi ukusanye mizigo mpaka ijae lori
 
Thanks for advice.
NAomba kujua bei ya HOWO horse na trailer inagharimu kiasi gani ili niweze kupanga bei ya nyumba yangu.
 
Nashukuru Muzee ''JembePoli''.
Ila ninavyofikiria ni rahisi kuwa dalali kama utakuwa na gari lako, kuliko kuwa dalali kwa kuwa huku ukiwa huna gari.
Shukran.

Bonge

JF-Expert Member
Aug 29, 2007
1,078
2,000
Kipindi hiki usafirishaji kwa mwenye lori moja ni mgumu kama huna contract ya uhakika....kuuza nyumba kwa ajili ya usafirishaji ni risk kubwa kipindi hiiya awamu ya tano.
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
50,054
2,000
Nashukuru Muzee ''JembePoli''.
Ila ninavyofikiria ni rahisi kuwa dalali kama utakuwa na gari lako, kuliko kuwa dalali kwa kuwa huku ukiwa huna gari.
Shukran.
NAomba kujua bei ya HOWO horse na trailer inagharimu kiasi gani ili niweze kupanga bei ya nyumba yangu.

Na kwanin usisafirishe mafuta kitu ambacho ni gurantee? Dry goods, containers au loose cargo zimepungua sana bongo. Utakufa kwa presha.
 
maringeni

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,201
2,000
Karibu mdau. Naona unataka pita njia yangu. Karibu. Mi nina transport business ambapo fleet yote ni scanias. Semis na short chasis aka vipisi. Nilinunua used za nje nikajenga bodi nikafanya biashara. Mtaji wa ndani na mikopo. Nilianza na fuso nikahamia scanias kwa sababu ya matengenezo. Magari yasio na ajent na spea usiguse. Biashara ya usafirishaji ni dereva. Usipokuwa na utaratibu mzuri watavunjavunja magari dakika. Maswali zaidi pm.
 
HORSE POWER

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
1,798
2,000
Ni NGUMU kupewa mkopo benki sababu mkopo wa benki mara nyingi kama sio zote huwa ni kwa ajili ya kuendeleza biashara. Wao kukukopesha wewe ni kujiingiza kwenye "Risk" kubwa.

Tafuta jinsi uianze hiyo biashara hata kwa kuuza "nyumba yako". Biashara ikisimama watafute benki.

NB: Benki si rafiki wa watu maskini.
Huo ndio ukweli.
 
isambe

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
2,195
2,000
Karibu mdau. Naona unataka pita njia yangu. Karibu. Mi nina transport business ambapo fleet yote ni scanias. Semis na short chasis aka vipisi. Nilinunua used za nje nikajenga bodi nikafanya biashara. Mtaji wa ndani na mikopo. Nilianza na fuso nikahamia scanias kwa sababu ya matengenezo. Magari yasio na ajent na spea usiguse. Biashara ya usafirishaji ni dereva. Usipokuwa na utaratibu mzuri watavunjavunja magari dakika. Maswali zaidi pm.
Transporter yoyote huko, Tanzania ni mtu ambaye yuko miserable muda wote,sijawahi kumuona transporter Tz hana furaha,yeye huwa anafurahi mara mbili tu,kipindi ananunua gari ma kipindi anauza gari
 
truckdriver

JF-Expert Member
May 7, 2012
552
250
nina semi imepaki tuu kama una uhakika wa kazi uifanyie kazi kwa makubaliano au kama unaweza inunua.
 
CONSULT

Senior Member
May 8, 2011
188
250
Karibu mdau. Naona unataka pita njia yangu. Karibu. Mi nina transport business ambapo fleet yote ni scanias. Semis na short chasis aka vipisi. Nilinunua used za nje nikajenga bodi nikafanya biashara. Mtaji wa ndani na mikopo. Nilianza na fuso nikahamia scanias kwa sababu ya matengenezo. Magari yasio na ajent na spea usiguse. Biashara ya usafirishaji ni dereva. Usipokuwa na utaratibu mzuri watavunjavunja magari dakika. Maswali zaidi pm.
Shukran kwa kumtia moyo pia ushauri mzuri, ikiwezekana tunaweza wasiliana kwa kubadilishana Ideas na njinsi ya kupambana na changamoto za transport sector
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom