Jinsi ya kukabiliana na ushindani wa wanaume wengine kwa mwenza wako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya kukabiliana na ushindani wa wanaume wengine kwa mwenza wako

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Sep 25, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  KATIKA uhusiano wa kimapenzi hakuna kosa kubwa kwa wanaume kama kutojiamini na mbaya zaidi kutomwamini mwenza wake. Kumekuwa na dhana kuwa tatizo la wivu lipo sana kwa wanawake kuliko wanaume, jambo ambalo si la kweli kwani hata wanaume nao husumbuliwa sana na ugonjwa huo.

  Tofauti ni kwamba wanaume wengi hufahamu namna ya kukabiliana na wivu na asilimia kubwa hujitahidi kutoonesha hisia zao wanapokutwa na hali hiyo.

  Hata hivyo pamoja na jitihada hizo, ni dhahiri kuwa bado wanaume wengi hushindwa kukabiliana na ushindani wa wanaume wenzao hasa wale wanaoonesha kuwa na hisia kwa mwanamke mmoja. Tatizo kubwa linalowasumbua inapotokea jambo kama hilo ni wivu na kutojiamini kama wanaweza kuvuta hisia za mwanamke huyo na kuwashinda wanaume wengine wenye nia kama hiyo.

  Tatizo la kutojiamini mara zote humpa shida mwanamume na kumfanya siku zote awe na mashaka kuwa huenda akaja mwanamume mwingine mwenye sifa kuliko yeye na kumchukua mwenza wake.

  Kwanza tatizo hilo ni kubwa na baya kwa mwanamume kwa vile hutawala mawazo yake na kutengeneza fikra za uongo kuwa hana sifa zinazostahili kuweza kushinda hisia za mwanamke anayempenda. Tatizo hilo huzidi kuwa baya zaidi pale mwanamume huyo anapotoka na mwenza wake huyo na kushuhudia wanaume wengine wanavyomkodolea macho ya kumtamani.

  Hali hiyo huongeza tatizo la kutojiamini kwa mwanamume huyo na kuzaa tatizo lingine kubwa la wivu na hivyo kumfanya mwanamume ashindwe kabisa kukabiliana na ushindani wa wanaume wengine.

  Wivu ni hisia kubwa ambayo humtawala binadamu, na mara nyingi humfanya mtu afikie hatua ya kumuua ampendaye, hisia hizi si binadamu tu ndiye aliyejaliwa kuwa nazo bali hata wanyama, ni hisia za asili.

  Hata hivyo katika suala la ushindani na mwanamume mwenzako juu ya mwanamke mnayempenda, hisia hizi za wivu hazisaidii kitu zaidi ya kukupatia hasira ambazo zitakufanya usijiamini na kukuharibia kabisa.

  Pamoja na hayo wivu pia unaweza kukufanya ufanye mambo ya kijinga na aibu kama vile kupigana kwa vile hisia hizo huwa na tabia ya kutawala mawazo na matendo yako bila kujali matokeo yake.

  Ili kukabiliana na hali hiyo mwanamume unapokutana na mwanamume mwenzako ambaye anaonesha hisia zake waziwazi kwa mwenza wako usithubutu kuonesha woga au wasiwasi, wivu na kutojiamini. Kwani ukionesha hisia hizo moja kwa moja mwanamume mwenzako atajisikia kuwa ana uwezo mkubwa wa kuwa na mwenza wako kuliko wewe, na mbaya zaidi ni pale mwenza wako atakapogundua kuwa hujiamini.

  Jambo la maana la kufanya ni kujiamini na kuepukana na tatizo la wivu na kubwa zaidi ni kutambua kuwa udhaifu wowote katika hilo unaweza kukupotezea mwanamke umpendaye. Pia jambo jingine la kukabiliana na ushindani wa wanaume wengine ni kwa mwanamume kujiandaa na kutarajia hali kama hiyo kabla hajatoka na mwenza wake, hali ambayo itamfanya asishangae au kuwa na wasiwasi wanaume wengine watakapomtamani mwenza wake.

  Kumbuka ili uweze kujijengea heshima, uwezo na uaminifu kwa mwenza wako ni kuondokana na wasiwasi, woga, kutojiamini na mbaya zaidi wivu hasa unapokuwa na mwenza wako. Kwa hilo hata wanaume wenzako watakuheshimu na kushindwa kumwingia mwenza wako kwa vile umeonesha dhahiri huna lolote la kukupatia hofu mbele yao.
   
 2. N

  Nwaigwe JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 779
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 80
  Haya bwana wamesikia!! wapi yo yo? mkurugenzi Fidel mmesikia hayo?nasikia kwa wivu wazee mpaka mnakondeana
   
 3. A

  Audax JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ahahahahaaaaaaaaaaaa,wivu ni kidonda-ukishiriki tu utakonda!!
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Wivu huua!Unakuua wewe mwenye wivu polepole..ila kabla hujakata roho wawezasababisha madhara kwa wengine.
   
 5. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  hilo tatizo mara nyingi utakuta watu wanapoteza uaminifu ktk mapenzi na hua mwanzo wa kutafuta small nyumba
   
Loading...