Jinsi ya kujua mtoto ni wako au la kwa kutumia DNA ya kimila

Kama ndiyo hivyo basi binadamu wooote tungekuwa na vigqnja vinavyo fanana kabisa maana woote asili yenu ni mtu mmoja, na kifupi huo utafiti si wa kweli maana kumbe katika famili watoto woye mnatakiwa kulingana alama na baba yenu hivyo hata kaka yako au mdogo wako akizaa na mkeo si rahisi kujua ukweli ?? Nadhani hili si la kweli kwa anaye jua kufikiri vizuri au mista mistari inayo ongelewa ni ipi siyo hiyoView attachment 474688
Mkuu kwani mkeo akichapwa na kaka yako wa damu mtoto akizaliwa sio wa kwako .
 
Katika jinsia hizi mbili mme na mke kwa kweli jinsia mke inapata lawama sana tena sana kwa kila jambo hapa Duniani.hivi kweli kuna ulazima mtoto afanane na baba yake jamani wakati kuna muingiliano wa damu mbili mke na mme.siamini huo utaratibu wa kuhisi mtoto si wangu.na hakuna sababu yoyote ya msingi kwa mwanadamu kuangalia vigezo hivyo ,
naona umekugusa sana
 
Mtoa mada itavunja ndoa nying za watu!,ila upo sahihi ninejalibu mkono wangu na vijana wangu wawili hapa majib kweli ni positive maana ni copy and paste!!!
umeniua uliposema nichukue mtoto ambaye nina uhakika mkubwa kuwa ni wangu ndio nifanye hyo test!
 
Hapo nyuma nilikuwa nikiambiwa kuwa Wazee ni dawa na hazina hasa katika kutupatia Maarifa sisi Vijana na Wajukuu zao nilikuwa sitaki kuamini na kuna wakati hata nilikuwa nikimwona tu Mtu Mzee au Bibi basi nawapuuza tu nikiamini kwamba hawana jipya tena.

Hali hii ilibadilika taratibu baada ya kuanza sasa kupenda kukaa na Wazee mara kwa mara ili niweze kuchota hekima na busara zao na kwa kweli tokea nianze kurudisha imani yangu kwa Wazee naona nimefaidika mno katika kupata Elimu dunia ambayo wengi wetu hatuna na tumebaki tu kujikita katika Elimu zetu hizi za Kitaaluma tukidhani kuwa pekee ndizo zitatukomboa Kifikra.

Pamewahi kuwa na nadharia kwamba akina Babu na Bibi wao huweza kujua Mtoto mchanga aliyezaliwa leo kama ni Mjukuu wao kweli au labda Mtoto wao amebambikiwa huyo Mtoto na Mama yake kutokana na usaliti wake ndani ya Mahusiano yao.

Niliamua kufanya mazugumzo yangu ya Kiudadisi kabisa na Wazee wa Mikoa mbalimbali ili tu niweze kujua kama kuna njia yoyote mbadala ( ukiachia ile ya kufanya DNA ambayo wengi wetu ndiyo tumeizoea ) ya Kiutamaduni ya kuweza kujua kama Mtoto aliyezaliwa na Mpenzi au Mke wangu ni wangu au nimebambikiwa.

Ndugu zanguni majibu niliyoyapata kutoka kwa hao Wazee wote yalinifanya nizidi kuamini kuwa kumbe tukiwatumia vizuri hawa Wazee bila kuwadhihaki, kuwadharau na kuwapuuza basi wanaweza kuwa sehemu yetu kubwa sana ya kupata maarifa na hata kutatua changamoto zetu zingine za kimaisha ambazo nyingi zimekuja kutokana na mfumo wetu huu wa Kimaisha ulioratibiwa na utandawazi ambao kimsingi umetuharibu na unaendelea kutuharibu.

Leo naweka hapa hadharani jinsi ya Wewe Mwanaume mwenzangu ambaye una Mtoto au hata upo mbioni kumpata Mtoto kuweza kujua kama huyo Mtoto aliyezaliwa ni wako kweli Kibailojia au umebambikiwa tu. Na nitangulize samahani kama kuna ambao nitawakwaza juu ya huu ukweli wa DNA ya Kiutamaduni ila nia yangu ni kuwaokoa tu Wanaume wenzangu juu ya hii kadhia ambayo imesababisha mitafaruku mingi mno katika Mahusiano na Ndoa.

HUU NDIYO UKWELI WA DNA YA KIUTAMADUNI

Ewe Mwanaume mwenzangu uliye na Mtoto hapo ulipo awe bado mdogo au tayari ameshakuwa Mtu mzima chukua mkono wowote uwe wa Kulia au wa Kushoto wa Mtoto unayeamini kabisa kuwa ni wako kisha kwa umakini kabisa huku ukiwa umetulia angalia pale katikati ya mkono ( katika palm ) linganisha ile mistari iliyopo na ya Mwanao kisha ukimaliza linganisha tena mistari iliyopo katika vidole vyake na vya Kwako.

Kwa mujibu wa hawa Mababu na Mabibi ( Wazee ) wanasema kuwa endapo Wewe Baba ukilinganisha hizo alama nilizokuelekeza hapo juu na kuona kuwa hazifanani na zako basi automatically jua ya kwamba huyo Mtoto siyo wako 100% na kwamba Mpenzi wako / Mkeo amekubambikia tu hivyo cha msingi tu ukishajua huu ukweli piga moyo konde, msamehe na maisha yaendelee.

Wamesema kwamba hata iweje Mtoto wako wa damu yako kabisa akizaliwa ni lazima tu alama zilizopo katika Mikono yake zitafanana na Wewe na wala haziongopi. Na ndipo hawa akina Babu na Bibi wakaenda mbele na kusema kuwa hiyo mbinu ndiyo iliweza kuwafanya wao huko nyuma wasiwe wasaliti na wawe wakweli kwani katika Makabila mengi hiyo mbinu ilishasambazwa na iliendelea kutumika. Na ili kulithibitisha hili ndiyo maana Bibi yoyote au Babu akipelekewa Mjukuu akimbeba tu kisirisiri atawahi kuuangalia mkono wa Mjukuu wake na hasa vidole vyake kisha atajua kuwa Mtoto wao kazalisha au kazalishiwa na wenzake.

MWISHO

Andiko langu hili kamwe halina kusudio la kuharibu Mahusiano yoyote yale bali naomba tulitumie tu kama sehemu ya kujipatia maarifa ambayo nina amini wengi wetu ( Vijana na Mabinti ) wa leo tulikuwa hatuna na kama itatokea umekuta umezalishiwa ( umebambikiwa ) basi ninachokuomba tu samehe, piga moyo konde na songa mbele na ule msemo wa Wahenga kuwa siku zote Kitanda hakizai haramu.

Kwa Dada zangu Wapendwa najua huu uzi utawaudhi na kuwauma ila tuvumiliane tu na pengine huu uzi unaweza ukawa msaada mkubwa sana Kwenu hasa katika kuwafanya mbadilike na muache kuwabambikia Wanaume zenu Watoto ambao siyo wao kwani hata Takwimu za mara ya mwisho za Mkemia Mkuu wa Serikali zinasema kuwa 49% ya Wanaume wa Kitanzania wanalea Watoto wasio wao ( wamebambikiwa ) hivyo mtusamehe na mtuonee huruma sisi Wanaume.

WEWE MPUMBAVU HIVI UNAJUA JUHUDI NILIZOZICHUA NA CHANGAMOTO NILIZOZIPATA HADI MIMI GENTAMYCINE KUJA NA HII TAARIFA AMBAYO WEWE BILA HATA HAYA UMEINAKILI VILE VILE ILIVYO KUTOKA KWANGU? HII NDIYO TABIA YA WAPI? UMESHINDWA BASI HATA TU HAPO CHINI KUNI ACKNOWLEDGE NA BADALA YAKE UMEANZISHA UZI AMBAO KIHAKIKA NA KIUSHAHIDI WA KILA KITU NI WA KWANGU MIMI? NIMESIKITIKA SANA NA KAMA Maxence Melo NA TIMU YAKO NZIMA YA JF HILI JAMBO HAMTALIFANYIA UFUMBUZI WA HARAKA MTATUVUNJA SANA MOYO SISI MEMBERS WENU TUNAOHANGAIKA KWA JUHUDI ZETU WENYEWE NA WAKATI MWINGINE HATA KUHATARISHA MAISHA YETU ILI TU TUWEZE KUJA NA TAARIFA AU MATUKIO MUHIMU HUMU JF NA KUIONGEZEA SIFA NA UMAARUFU MTANDAO WENU. HUYU MEMBER truewor AMENISIKITISHA SANA NA AMENIVUNJA MNO MOYO.

NI HABARI AMBAYO NILIANDIKA HUMU JUMATATU YA WIKI HII YA TAREHE 20, FEBRUARY 2017 MUDA WA SAA 2 NA DAKIKA 31 NA KUIWEKA KATIKA FORUM YA MAHUSIANO, MAPENZI NA URAFIKI HALAFU NA YEYE BILA AIBU KAJA NAYO VILE VILE JANA JUMAMOSI TAREHE 25, FEBRUARY 2017 NA KAIWEKA KATIKA FORUM YA HABARI NA HOJA MCHANGANYIKO.

HILI JAMBO NA HII CHANGAMOTO ISIPOCHUKULIWA HATUA NA MAMLAKA NZIMA YA JAMIIFORUMS MTATUFANYA SISI WENGINE SASA TUBAKI TU KUWA WATAZAMAJI HUMU JF NA KAMWE TUSILETE TAARIFA ZOZOTE ZILE KWANI NI KITENDO KIBAYA NA CHA KIKATILI MNO AMBACHO KIUKWELI KIMESHANIHARIBIA SIKU YANGU KABISA.

NAMSHUKURU SANA MEMBER MWAMINIFU KWANGU AITWAE lukesam AMBAYE KIMSINGI NDIYO AMENISHTUA NA KUNIAMSHA JUU YA HILI. NILIKUWA NAJUA TU KUWA KUNA MEDIA KADHAA NA MITANDAO BAADHI AMBAO HUCHUKUWA TAARIFA ZANGU NINAZOZILETA HUMU JF NA KUZITUMIA KWA FAIDA YAO NA KUJIINGIZIA NAZO KIPATO KUMBE NA LEO NIMEGUNDUA KUWA WAPO MEMBERS BAADHI HUMU HUMU WA MFANO WA HUYU ALIYENAKILI TAARIFA YANGU AMBAO BILA CHEMBE YA UWOGA WANANAKILI KILA KITU CHANGU NA KUJIFANYA WAO NDIYO WAMEKILETA.

NIMESIKITIKA, NIMESIKITIKA NA NIMESIKITIKA.
 
Mkuu GENTAMYCINE Mwizi mwingine huyu..

Akhsante sana Mkuu lukesam na tayari nimeshamripoti kwa Mhusika Mkuu mwenyewe na Timu yake nzima na ni matumanini yangu hatua Kali za Kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake ili iwe fundisho kwa wengine kwani Watu tunajitoa na kuteseka mno kuleta taarifa au matukio humu tena bila ya kutaka chochote kila kutoka JF bali tunafanya hivi kwa Mapenzi yetu makubwa kwa huu Mtandao wa JamiiForums lakini kitendo cha kama huyu Member truewor kinatuvunja mno moyo na kitatuogopesha hata kuhangaika kuinogesha JF yetu. Yaani Mwanamume wa KIZANAKI nimejipinda kabisa kwa kuhangaika kuja na taarifa kama hiyo halafu Mpuuzi mmoja tu anainakili vile vile na kuileta humu. Kwahiyo kumbe anasafiria nyota yangu? Nimalizie tu kwa kumuambia huyo Jamaa kuwa GENTAMYCINE always ni TALENTED and CHARISMATIC na nguvu yangu ni ya Kimungu ambayo Binadamu yoyote haiwezi na nina Nyota ya Kimungu ambayo muda wote inaniweka juu na haita zimwa na Shetani Mtu yeyote.
 
Hapo nyuma nilikuwa nikiambiwa kuwa Wazee ni dawa na hazina hasa katika kutupatia Maarifa sisi Vijana na Wajukuu zao nilikuwa sitaki kuamini na kuna wakati hata nilikuwa nikimwona tu Mtu Mzee au Bibi basi nawapuuza tu nikiamini kwamba hawana jipya tena.

Hali hii ilibadilika taratibu baada ya kuanza sasa kupenda kukaa na Wazee mara kwa mara ili niweze kuchota hekima na busara zao na kwa kweli tokea nianze kurudisha imani yangu kwa Wazee naona nimefaidika mno katika kupata Elimu dunia ambayo wengi wetu hatuna na tumebaki tu kujikita katika Elimu zetu hizi za Kitaaluma tukidhani kuwa pekee ndizo zitatukomboa Kifikra.

Pamewahi kuwa na nadharia kwamba akina Babu na Bibi wao huweza kujua Mtoto mchanga aliyezaliwa leo kama ni Mjukuu wao kweli au labda Mtoto wao amebambikiwa huyo Mtoto na Mama yake kutokana na usaliti wake ndani ya Mahusiano yao.

Niliamua kufanya mazugumzo yangu ya Kiudadisi kabisa na Wazee wa Mikoa mbalimbali ili tu niweze kujua kama kuna njia yoyote mbadala ( ukiachia ile ya kufanya DNA ambayo wengi wetu ndiyo tumeizoea ) ya Kiutamaduni ya kuweza kujua kama Mtoto aliyezaliwa na Mpenzi au Mke wangu ni wangu au nimebambikiwa.

Ndugu zanguni majibu niliyoyapata kutoka kwa hao Wazee wote yalinifanya nizidi kuamini kuwa kumbe tukiwatumia vizuri hawa Wazee bila kuwadhihaki, kuwadharau na kuwapuuza basi wanaweza kuwa sehemu yetu kubwa sana ya kupata maarifa na hata kutatua changamoto zetu zingine za kimaisha ambazo nyingi zimekuja kutokana na mfumo wetu huu wa Kimaisha ulioratibiwa na utandawazi ambao kimsingi umetuharibu na unaendelea kutuharibu.

Leo naweka hapa hadharani jinsi ya Wewe Mwanaume mwenzangu ambaye una Mtoto au hata upo mbioni kumpata Mtoto kuweza kujua kama huyo Mtoto aliyezaliwa ni wako kweli Kibailojia au umebambikiwa tu. Na nitangulize samahani kama kuna ambao nitawakwaza juu ya huu ukweli wa DNA ya Kiutamaduni ila nia yangu ni kuwaokoa tu Wanaume wenzangu juu ya hii kadhia ambayo imesababisha mitafaruku mingi mno katika Mahusiano na Ndoa.

HUU NDIYO UKWELI WA DNA YA KIUTAMADUNI

Ewe Mwanaume mwenzangu uliye na Mtoto hapo ulipo awe bado mdogo au tayari ameshakuwa Mtu mzima chukua mkono wowote uwe wa Kulia au wa Kushoto wa Mtoto unayeamini kabisa kuwa ni wako kisha kwa umakini kabisa huku ukiwa umetulia angalia pale katikati ya mkono ( katika palm ) linganisha ile mistari iliyopo na ya Mwanao kisha ukimaliza linganisha tena mistari iliyopo katika vidole vyake na vya Kwako.

Kwa mujibu wa hawa Mababu na Mabibi ( Wazee ) wanasema kuwa endapo Wewe Baba ukilinganisha hizo alama nilizokuelekeza hapo juu na kuona kuwa hazifanani na zako basi automatically jua ya kwamba huyo Mtoto siyo wako 100% na kwamba Mpenzi wako / Mkeo amekubambikia tu hivyo cha msingi tu ukishajua huu ukweli piga moyo konde, msamehe na maisha yaendelee.

Wamesema kwamba hata iweje Mtoto wako wa damu yako kabisa akizaliwa ni lazima tu alama zilizopo katika Mikono yake zitafanana na Wewe na wala haziongopi. Na ndipo hawa akina Babu na Bibi wakaenda mbele na kusema kuwa hiyo mbinu ndiyo iliweza kuwafanya wao huko nyuma wasiwe wasaliti na wawe wakweli kwani katika Makabila mengi hiyo mbinu ilishasambazwa na iliendelea kutumika. Na ili kulithibitisha hili ndiyo maana Bibi yoyote au Babu akipelekewa Mjukuu akimbeba tu kisirisiri atawahi kuuangalia mkono wa Mjukuu wake na hasa vidole vyake kisha atajua kuwa Mtoto wao kazalisha au kazalishiwa na wenzake.

MWISHO

Andiko langu hili kamwe halina kusudio la kuharibu Mahusiano yoyote yale bali naomba tulitumie tu kama sehemu ya kujipatia maarifa ambayo nina amini wengi wetu ( Vijana na Mabinti ) wa leo tulikuwa hatuna na kama itatokea umekuta umezalishiwa ( umebambikiwa ) basi ninachokuomba tu samehe, piga moyo konde na songa mbele na ule msemo wa Wahenga kuwa siku zote Kitanda hakizai haramu.

Kwa Dada zangu Wapendwa najua huu uzi utawaudhi na kuwauma ila tuvumiliane tu na pengine huu uzi unaweza ukawa msaada mkubwa sana Kwenu hasa katika kuwafanya mbadilike na muache kuwabambikia Wanaume zenu Watoto ambao siyo wao kwani hata Takwimu za mara ya mwisho za Mkemia Mkuu wa Serikali zinasema kuwa 49% ya Wanaume wa Kitanzania wanalea Watoto wasio wao ( wamebambikiwa ) hivyo mtusamehe na mtuonee huruma sisi Wanaume.
Binafsi siamini ulichokiandika hapa naona kama ni upotoshaji tu,kuna vitabu vinavyoeleza kwa umakini kuhusu elimu ya kiganja (palmistry),kwa kuibia kidogo hapo kwenye mkono kuna mistari mbalimbali lakini iliyo muhimu ni line of head,line of heart,line of fate,line of life nk,kupitia mistari hii unaweza kupata informations mbalimbali kutegemeana na mstari unao observe,mfano mtu aliyebobea kwenye elimu hii anaweza akatazama line of life ya mtoto aliyezsaliwa leo akakwambia kama ataishi muda mrefu ama la (huo ni mstari unaozunguka huo mlima chini ya dole gumba) au akatazama line of fate na akajua mtu ataishi maisha ya namna gani kama kutakuwa na misukosuko au la (huu ni mstari unaokatiza katikati ya mkono toka juu bkuelekea chini na unaweza kuelekea kwenye kidole cha shahada,au cha kati au cha pete au kidogo na kila moja katika uelekeo huo kuna tafsiri yake katika fate kama za uongozi,pesa,kuheshimika nk,line of head na line of heart ni hiyo mistari miwili inayokatiza kiganjani toka kulia kwenda kushoto unapachia mkono freely wa juu ni head na wa chini ni heart,hapo napo unaweza kutoa informations nyingi tu zaq mtu mfano issues za ubongo kwa line of head nk.
mistari hii inaweza kutofautiana kwa mzazi na mtoto,mfano line of life ya mtoto mwenye maisha mafupi haiwezi kuwa sawa na ya mzazi mwenye maisha marefu,au line of fate ya mtoto mwenye bahatii ya madaraka haiwezi kufanana na mzazi asiye na kipawa au line of head ya baba na mtoto haziwezi kufanana kama uwezo wao kichwani ni tofauti...elimu hii ni pana lakini kwa ufupi sana hiyo ndio ramani yake mkuu.
 
Unavyosema bibi au babu akiletewa mtoto anaweza akagundua kuwa ni wa damu yao simply kwa kuangalia kiganja cha mtoto.

Swali langu ni je, ni sharti baba mtoto nae awepo au wenyewe wanajua automatically, ina maana kuwa babu au bibi amekariri print za mtoto wake?
 
mleta mada hongera sana but hiki kitu Mimi niliambiwa na marehemu bibi tangu nikiwa standard 6
sababu ya marehemu bibi kunambia ilikuwa hivi
siku moja al-manusura nikatwe mkono kisa nna symbol ya M ktk mkono wangu wa kulia kwa qadari za Allah (mungu wa haqi) nikaponyeka niliporejeshwa nyumbani bibi akanambia mtu akikwambia nionyeshe mkono wako kataa hata baba ako pia ana hiyo alama na hata wafanyakazi wenzake huwa hawaonyeshi na hiyo alama inaonyesha uzao na umiliki halali wa mtoto (alikuwa akikusudia alama za mikononii)
 
Wazee haohao wa zamani ndito walisema na kutuaminisha kuwa "kitanda hakizai haramu"

If u want a stressful life na uishie pabaya, wewe fuatilia tu haya mambo. In absence of DNA the true owner of the baby is its mom, wengine ni viherehere tu.
Nashangaa kwa nini wanawake hawaja like hii post yako.
By the way kwa nini uogope kuujua ukweli kisa eti utapata stress!! Kwa hiyo were ni heei uonekane zombie kuliko kuujua ukweli?
 
Back
Top Bottom