Jinsi ya kujua kama Tovuti unayotembelea ni salama

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Angalia kama Tovuti uliyoifungua au kuitembelea ina alama ya kufuli kwenye 'URL' yake. Alama hii hutokea kabla ya 'link' iliyofungua ukurasa huo

Kufuli hili humaanisha kuwa kuna usalama katika mawasiliano yanayofanyika au yatakayofanyika kupitia Tovuti husika

Aina hii ya ulinzi imewekwa kuhakikisha hakuna Mtu anayeza kuingilia tovuti hiyo na kubadili taarifa zinazotumwa kupitia tovuti husika

Tazama mfano pichani

C5A5C245-B268-429B-8BE4-A5C4224C55AB.jpeg


Hakikisha Tovuti uliyotembelea inaanza na HTTPS badala ya HTTP. HTTPS inasimama badala ya maneno Hypertext Transfer Protocol Secure (HTTPS) neno la msingi hapo ni 'Secure' ikimaanisha usalama

Mfano: Kila kiunganishi kutoka katika Tovuti ya JamiiForums lazima itaanza kusomeka hivi: JamiiForums

Aidha, zipo Tovuti nyingi ambazo bado hazijazingatia usalama huu kwani bado zinatumia mfumo wa HTTP hivyo usalama kuwa mdogo zaidi kwa watumiaji wake

Tazama mfano pichani
DF3431D1-BDE9-47AC-8246-D1F069F3D7B5.jpeg


Lazima Tovuti hiyo itakuwa imeambatanisha Sera ya Faragha (Privacy Policy) kwa ajili ya watembeleaji wake

Sera ya Faragha ni nyaraka inayopatikana kwenye tovuti ikiwaeleza watembeleaji wake ni taarifa zipi zitakusanywa kutoka kwake

Aidha, Sera ya Faragha hueleza jinsi waendeshaji wa tovuti hiyo watakavyo zitumia taarifa hizo

JamiiTalks inakusisitiza kukumbuka kusoma na kuzielewa Sera za Faragha katika Tovuti unazotembelea au kujisajili

Tazama mfano pichani

936EC3BA-8FB2-4974-8B51-0D374719B8F0.jpeg
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom