Fahamu jinsi ya kujua jinsi (sex) ya mtoto tumboni bila ultrasound

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,502
23,581
Habari wan JF,

Leo nimetafakari na kuamua kuandika uzi wa kuhusu maswala muhimu kidogo kwa wanandoa/ wanao tegemea kupata mtoto.

Jambo moja wapo ambao linatia furaha katika maisha ya wazazi/wapenzi ni pale wanapo tegemea mtoto. Mambo chungu nzima hua yanatia hamasa na ushawishi kuhusiana na huyo mtoto, kuanzia jinsia yake kama ni wa kiume au kike na kadhalika. Maandalizi huanza kufanywa kabla hata ya mtoto kuzaliwa, hii ikijumuisha manunuzi ya vitu kwaajili ya mtoto na majina pindi atakapo zaliwa.

Madaktari wana uwezo wa kujua jinsia ya mtoto ambae hajazaliwa wakati wa ULTRASOUND hospitalini. Na wachache hawatambui ya kua mtoto anaweza akahisiwa jinsia yake kutokana na dalili ambazo mama mjamzito huzipata, kuanzia mabadiliko ya kimwili, kulala na mpaka upendo wa vyakula fulani.

Utastaajabu kujua kuna uwezekano wa viashiria kuhusiana na jinsia ya mtoto anaetegemewa, bila kwenda hospitali na kutumia ULTRASOUND.

Kuna dalili nyingi ambazo sinaweza kukupa taarifa kuhusiana na jinsia ya mtoto kabla ya kuzaliwa. Kutokana na utafiti, ume baini haya yafutayo kama viashiria vya kujua jinsia ya mtoto kabla hata hajazaliwa;

18) Umachachari wa mjamzito (Clumsiness)
Kwa kila jinsi mwili/tumbo la mjamzito linavyokua, umachachari hua haukosekani, ila unapopitiliza mipaka kuliko kawaida, basi kuna uwezekano mkubwa wa kujifungua mtoto mwenye jinsia ya KIUME.

17) Kukua kwa Maziwa/Matiti (Breast Size)
Katika kila hatua ya mimba, mwanamke hua anagundua ni jinsi gani maziwa/matiti yake hubadilika kwa kukua. Kama ziwa/titi lake la kulia likitokea kuwa kubwa kuliko la kushoto, basi kuna uwezekano mkubwa wa kujifungua mtoto wa KIUME. Na kama titi/ziwa la kushoto likiwa kubwa kuliko la kulia, basi kuna uwezekano mkubwa wa kujifungua mtoto wa KIKE.

16) Rangi ya Chuchu (Nipple Color)
Rangi ya chuchu kipindi cha ujauzito zinaweza kuashiri jinsia ya mtoto, rangi inapokua ya kiza (darker) kuliko kawaida ni dalili ya kujifungua mtoto wa KIUME, na kama rangi haijabadilika katika hatua za mimba ni dalili ya mtoto wa KIKE.

15) Aina ya Ulalaji (Sleeping Position)
Kupendelea kulalia ubavu wa kulia ni dalili za kujifungua mtoto wa KIUME, na kupendelea kulalia ubavu wa kushoto ni dalili ya kujifungua mtoto wa KIKE.

14) Kuumwa Kichwa (Headache)
Kama mjamzito atakua na matatizo ya kuumwa kichwa mara kwa mara, mtoto wa KIUME yupo njiani kuja. Na kama hatokua na matatizo ya kichwa, basi uwezekano wa mtoto wa KIKE kuzaliwa.

13) Uzito wa Baba (Dad's Weight)
Kama mzazi wa kiume akiongezeka kilo, ni dalili za mama mjamzito kujifungua mtoto wa KIKE, na kama mzazi wa kiume asipo ongezeka kilo/au kupungua kilo ni dalili za mtoto wa KIUME.

12) Tumbo la Uzazi Kua Juu au Chini (Carrying High or Low)
Kama tumbo la mjamzito litakua juu, ni dalili za kuzaliwa mtoto wa KIKE, na kama tumbo la uzazi litakua chini basi inaashiria mtoto wa KIUME.

11) Tamaa ya Chakula (Food Craving)
Tamaa ya kupendelea vyakula vya chumvi/ukali basi ni dalili ya kupata mtoto wa KIUME, na kupendelea kula vyakula vya sukari ni dalili ya mtoto wa KIKE.

10) Miguu Kuvimba (Foot Swelling)
Kama miguu ya mjamzito haivimbi, basi inaashiria mtoto wa KIKE, kwani mtoto wa KIUME ana uwezo wa kumwongezea mjamzito uvimbaji wa miguu, mara mbili ya size ya huyo mjamzito miguu yake.

9) Joto la Nyayo za Miguu (Foot Temperature)
Kama nyayo za miguu zitakua za baridi, kuna dalili ya kujifungua mtoto wa KIUME, na kama nyayo hazijabadilika joto lake halisia ni dalili za mtoto wa KIKE.

8) Kugawanyika Kwa Uzito Mwilini (Weight Distribution)
Kama mjamzito ataongezeka kilo/uzito mwili mzima, ni dalili za kujifungua mtoto wa KIKE. Na kama ataongezeka uzito kwenye tumbo tu ni dalili za mtoto wa KIUME kuwa njiani.

7) Nywele za Mwilini (Body Hair)
Nywele za mwilini kukua kwa haraka na kua imara, ni dalili za mtoto wa KIUME kuzaliwa, wakati dalili za mtoto wa KIKE hua nywele hazioti mwilini.

6) Unawiri wa Nywele Kichwani (Hair Texture)
Nywele nzito na zenye mafuta/kunawiri ni kiashiro cha kujifungua mtoto wa KIUME, na nywele kavu/kukatika/kukosa mvuto/rough ni dalili ya kujifugua mtoto wa KIKE.

5) Kipimo Cha BAKING-SODA (The Baking Soda Test)
Chukua vijiko viwili vya baking soda na kisha changanya na mkojo wa mjamzito, kama baking soda itatoa mapovu ya gas na mliokama wa kuchemka (fizzes), ni mtoto wa KIUME anakuja. Kinyume na hapo basi atakua wa KIKE.

4) Mstari Tumboni (Linea Nigra)
Huu ni msitari ambao hutokea katika tumbo la mjamzito, mstari huu ukitokea na kuishia chini ya kitovu, basi inaashiria ujio wa mtoto wa KIKE, na kama ukipitiliza mpaka juu ya kitovu, ni kiashirio cha kuja kwa mtoto wa KIUME.

3) Furaha/Muwako/Kunawiri Usoni (The Glow)
Ni mtoto wa KIUME pekee ndio ambae humpa muwako/sura ya furaha/kunawiri kwa uso wa mama mjamzito. Mtoto wa kike humchosha sura mama yake muda wote.

2) Chunusi (Acne)
Kubemba mimba ya mtoto wa KIKE huwaletea wajawazito chunusi usoni, ni dalili moja wapo. Vinginevyo, atakua mtoto wa KIUME.

1) Mabadiliko Ya Ngozi (Skin Changes)
Kama ngozi ya mjamzito ikibadilika na kua yenye mafuta (oily skin) ni dalili za kuashiria mtoto ajae ni wa KIKE, na kama ngozi ikibakia kua kavu (dry skin) ni dalili za ujio wa mtoto wa KIUME.

Ahsanteni,
 
Kweli kabisa, sema bwana mkubwa watoto wakike wamekuwa TOO MUCH miaka ya hivi karibuni.
.
Mtaa mmoja wenye wanawake 20 waliozaa kati ya hao 4-5 wakiume wengine ni KE kwanini? Tutafutie majibu mkubwa
Dr. Shettles, mwandishi wa kitabu kiitwacho "How to Choose the Sex of Your Baby" (Jinsi gani kuchagua jinsia ya mtoto wako) , anaamini manii/mbegu za kiume/shahawa za kuleta mtoto wa jinsia ya KIUME na ya jinsia ya KIKE zinaurithi/uwezo tofauti.

Akimaanisha manii/mbegu za mwanaume/shahawa za jinsia ya mtoto wa KIUME ni dhaifu sana kiafya, haziishi kwa muda mrefu, lakini zina spidi kubwa ya kuogelea katika sehem za siri za wanamama katika hatua za kwenda kwenye yai la mwanamke, pia ni ndogo kimaumbiele kuliko za jinsia ya KIKE.

Aligundua manii/mbegu za mwanaume/shahawa za jinsia ya KIKE zina ustahamilivu, na uwezo wa kuishi muda mrefu ndani ya mwili wa mwanamke baada ya tendo la ndoa.

Akauliza swali katika hicho kitabu chake, na kisha kujijibu yeye mwenyewe: Je ni kipi unaweza ukafanya ili kuzipa manii/mbegu za kiume/shahawa zenye jinsia ya kupata mtoto wa KIUME nafasi nzuri/kubwa ya kwenda kuliivisha yai la mwanamke?

Majibu yake yalikua,

1) Position ya kufanya mapenzi.

Dr. Shettle anaamini katika utafiti wake mambo matatu,

Kwanza, POSITION ya ufanyaji mapenzi ni muhimu kusaidia manii yenye jinsia ya KIUME kwenda kuivisha yai. Position zenyewe muhim ni zile za kuwezesha UUME kuzama ndani kabisa ya UKE (Deep Penetration).

Inaweza isiingie akilini, ila alicho maanisha ni kwamba kadri UUME unapokua karibu na sehemu YAI linapotengenezwa/kuhifadhiwa ndani ya sehemu za siri za mwanamke, basi manii ya KIUME yanakua na nafasi kubwa ya kuliwahi yai la mwanamke na kuliivisha. Aliainisha style hizi,

a) Doggy Style.
b) Kusimama (Hii inazipa nafasi mbegu zenye jinsia ya KIUME kuogelea zaidia ya mbegu za jinsia za KIKE).
c) Straddling style (Mwanaume kukaa/kulala na kisha mwanamke kumkalia kwa juu, inasababisha uume kuzama ndani zaidi (deep penetration).

Jambo la pili, Timing ya kupevuka kwa yai la mwanamke katika yale masiku 28 (Cycle Timing).

Kwakua manii yenye jinsia ya KIUME hua na spidi kuliko jinsia ya KIKE, Dr. Shettles anashauri kufanya tendo la ndoa la kusababisha UUME kua karibu na OVERY ya mwanamke kadri iwezekanavyo katika masiku hatari (Danger Cycle).

Na kama ukifanya tendo la ndoa siku kadhaa kabla ya kuiva kwa yai la mwanamke, basi manii yasiokua na uimara (jinsia ya KIUME) yatakufa, na kuacha manii ya jinsia ya KIKE kuliivisha yai litakapo kua tayari.

Jambo la tatu, nguo za ndani anazovaa mwanaume (boxer/chupi).

Itakua umeshasikia kua nguo za ndani za mwanaume zina uwezo wa kuathiri utengenezwaji wa manii/mbegu za kiume/shahawa. Kitu ambacho hakuma mwanaume anaeweza akakichukulia kwa urahisi/masihara/utani pindi anapotaka kutafuta mtoto.

Kama imani inavyokua, mwanaume anaevaa nguo za ndani za kaptura (short boxer) inasemekana ndio bora zaidi kwa utengenezaji wa manii imara, kwasababu korodani hazipati joto kali na kuathiri utengenezwaji wa manii/shahawa (Restricting Sperm Production).

Nguo za ndani za kubana zinasemekana kusaidia kubakisha manii/shahawa zenye jinsia ya KIKE, na kuua zenye jinsia ya KIUME. Pia joto likizidi kutokana na boxer/chupi za kubana linapunguza/kusimamisha utengenezwaji wa manii yenye afya.

Natumai umeridhika na jibu.

Ahsante,
 
Dalili hzo zinaanza katika kipnd kip!? Katika umri upi wa ujauzito?
Dalili hua zinaanza kujitokeza kuanzia Miezi Miwili na kupanda juu mkuu. Ila kuna baadhi zinachelewa, mfano wa hio kuongezeka kilo/mimba kua juu au chini.
 
Huu uzi ngoja niuhifadhi kwaajili ya matumizi ya mda mchache ujao..

Ila kwanini dalili nzuri nzuri ndio zi ahusishwa na kuzaliw wakiume na zile mbaya mbaya ni wakike? Kuna sababu za kisayansi hapo mkuu?
Kisayansi sijawahi kukutana na swala kama hilo mkuu,

Ila kimaisha, siku zote mtoto wa kiume kwa mama hua hapindui (au katika familia ya upande wa mama). Mtoto wa kike mara nyingi pasua kichwa vs mama yake, nahisi anaanza kumchimba biti mama yake mapema, kabla hajatia timu.
 
Correction, mkuu... ni nje ya mada ila ningependa kukuweka sawa kidogo ni kwamba... gender haionekani... ila "sex" ndio inaonekana... huwezi kuona gender... ila unaweza kuona jinsia "sex" ya mtu kama ni mvulana au msichana.
 
Back
Top Bottom