Jinsi ya kujua jinsia (gender) ya mtoto tumboni bila ultrasound

Beef Lasagna

JF-Expert Member
Mar 30, 2015
16,572
2,000
Mashallah, hongera sana dada na mie nasubiri nikijifungua salama inshallah nilete mrejesho naona dalili kama tatu zinalingana jaman hongera sana Allah atukuzie binti yetu inshallah
πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™ asante Sana, inshaalaah na wewe utajifungua Salama.
 

TATA MKURIA

Senior Member
Apr 6, 2015
177
250
Mkuu,
Dr. Shettles, mwandishi wa kitabu kiitwacho "How to Choose the Sex of Your Baby" (Jinsi gani kuchagua jinsia ya mtoto wako) , anaamini manii/mbegu za kiume/shahawa za kuleta mtoto wa jinsia ya KIUME na ya jinsia ya KIKE zinaurithi/uwezo tofauti.

Akimaanisha manii/mbegu za mwanaume/shahawa za jinsia ya mtoto wa KIUME ni dhaifu sana kiafya, haziishi kwa muda mrefu, lakini zina spidi kubwa ya kuogelea katika sehem za siri za wanamama katika hatua za kwenda kwenye yai la mwanamke, pia ni ndogo kimaumbiele kuliko za jinsia ya KIKE.

Aligundua manii/mbegu za mwanaume/shahawa za jinsia ya KIKE zina ustahamilivu, na uwezo wa kuishi muda mrefu ndani ya mwili wa mwanamke baada ya tendo la ndoa.

Akauliza swali katika hicho kitabu chake, na kisha kujijibu yeye mwenyewe: Je ni kipi unaweza ukafanya ili kuzipa manii/mbegu za kiume/shahawa zenye jinsia ya kupata mtoto wa KIUME nafasi nzuri/kubwa ya kwenda kuliivisha yai la mwanamke?

Majibu yake yalikua,

1) Position ya kufanya mapenzi.

Dr. Shettle anaamini katika utafiti wake mambo matatu,

Kwanza, POSITION ya ufanyaji mapenzi ni muhimu kusaidia manii yenye jinsia ya KIUME kwenda kuivisha yai. Position zenyewe muhim ni zile za kuwezesha UUME kuzama ndani kabisa ya UKE (Deep Penetration).

Inaweza isiingie akilini, ila alicho maanisha ni kwamba kadri UUME unapokua karibu na sehemu YAI linapotengenezwa/kuhifadhiwa ndani ya sehemu za siri za mwanamke, basi manii ya KIUME yanakua na nafasi kubwa ya kuliwahi yai la mwanamke na kuliivisha. Aliainisha style hizi,

a) Doggy Style.
b) Kusimama (Hii inazipa nafasi mbegu zenye jinsia ya KIUME kuogelea zaidia ya mbegu za jinsia za KIKE).
c) Straddling style (Mwanaume kukaa/kulala na kisha mwanamke kumkalia kwa juu, inasababisha uume kuzama ndani zaidi (deep penetration).

Jambo la pili, Timing ya kupevuka kwa yai la mwanamke katika yale masiku 28 (Cycle Timing).

Kwakua manii yenye jinsia ya KIUME hua na spidi kuliko jinsia ya KIKE, Dr. Shettles anashauri kufanya tendo la ndoa la kusababisha UUME kua karibu na OVERY ya mwanamke kadri iwezekanavyo katika masiku hatari (Danger Cycle).

Na kama ukifanya tendo la ndoa siku kadhaa kabla ya kuiva kwa yai la mwanamke, basi manii yasiokua na uimara (jinsia ya KIUME) yatakufa, na kuacha manii ya jinsia ya KIKE kuliivisha yai litakapo kua tayari.

Jambo la tatu, nguo za ndani anazovaa mwanaume (boxer/chupi).

Itakua umeshasikia kua nguo za ndani za mwanaume zina uwezo wa kuathiri utengenezwaji wa manii/mbegu za kiume/shahawa. Kitu ambacho hakuma mwanaume anaeweza akakichukulia kwa urahisi/masihara/utani pindi anapotaka kutafuta mtoto.

Kama imani inavyokua, mwanaume anaevaa nguo za ndani za kaptura (short boxer) inasemekana ndio bora zaidi kwa utengenezaji wa manii imara, kwasababu korodani hazipati joto kali na kuathiri utengenezwaji wa manii/shahawa (Restricting Sperm Production).

Nguo za ndani za kubana zinasemekana kusaidia kubakisha manii/shahawa zenye jinsia ya KIKE, na kuua zenye jinsia ya KIUME. Pia joto likizidi kutokana na boxer/chupi za kubana linapunguza/kusimamisha utengenezwaji wa manii yenye afya.

Natumai umeridhika na jibu.

Ahsante,
Kumbe ndo maana nimepata ME babies watatu mfululizo, na KE mmoja. Okay mkuu. Nimekupata sasa
 
Top Bottom