Jinsi ya kujiunga na Bima ya afya kwa mtu asiyekua mwajiriwa sehemu yeyote

chief 1

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
260
101
Heshima kwenu wana jamvini, naomba msaada kwa anayejua utaratibu na namna ya kujiunga na huduma ya Bima ya afya kwa mtu asiye muajiriwa, je ni hatua gani za kufuata na ni katika ofisi gani inahusika na huduma hizo? natanguliza shukrani.
 
kuna prv company znatoa huduma hiyo ila inabidi ulipie laki 9 kwa mwaka.utatibiwa ww n ur family can uhakika inakua watu wangapi,but utatibiwa kwa ugonjwa wowote ule ata u cost milioni ngapi,ntauliza zaidi kuhusu hiyo ofisi then ntakujulisha
 
Kweli Ugonjwa hauna siku wala hodi.
Maana laki 900,000 aisee hata kwa alieajiriwa kazi pevu.

Maana mie na familia yangu hata laki moja kwa mwaka hatuimalizi kwenye magonjwa,lakini siku likitokea kubwa ndio nitaisoma.

Mie nahisi kiwango cha pesa wakiangalie upya.Unaweza kukuta mifuko baadhi baada ya muda ikafa kabisaa.
Kuwe na Packages fulani kwenye hilo,lakini kwa mfumo huu ni wale wenye pesa ya maana ndio watakaojiunga
 
Laki Tisa ni nyingi sana yaani zaidi ya bima ya Gari. Haitakuwa hela zote hizo. Icheki salary slip yako uione kwa mwezi hela ngapi kisha zidisha mara 12 utapata jibu.
 
Ni sahihi kabisa ni TSH 965,000/= mume, mke na dependants 4 hii ni kama unakwenda kama mtu binafsi na siyo mwajiriwa
lakini iwapo umeajiriwa wanataka 3% ya Basic salary yako kila mwezi na mwajiri anaweka 3% kufikisha 6% hata hivyo kiwango cha basic pay hakipaswi kuwa chini ya TSH 250,000/= pm ambapo utachangia TSH 15,000/( 3% + 3%).
Kuna baadhi ya magonjwa ambayo kama ukijiunga kama mtu binafsi hayatibiwi kwa mwaka wa kwanza km cancer, nk
ingia kwenye tovuti yao kuna namba zao za simu utapata more details
 
Na wao wajiongeze kwa kuja kutoa ufafanuzi kwenye mitandao. Sio mpaka mtu afunge safari kwenda kuuliza vitu vinavyoweza kujulikana. Utaratibu huu wa kuokoteza taarifa sio poa nawakati kwenye hizo taasis watu wa IT wapo.
 
Mfuko wa bima ya afya wa taifa ambao ni wa serikali sasa unatoa bima kwa mtu asiye mtumishi anaitajika kuchangia shilingi elfu kumi kwa mwaka katika hiyo elfu kumi ni bima ya afya inayojumuisha watu sita yani ukilipia hiyo elfu kumi utatakiwa uandikishe watu sita ambao watanufaika na hiyo bima hao watu sita wote gharama ni hiyo hiyo elfu kumi yani unatoa elfu kumi kisha unandikisha watu sita

Hii bima ya elfu kumi unaweza kutibiwa ndani ya wilaya yako tu uliyojiandikishia mfano wewe ni mkazi wa tunduru basi utaweza kutibiwa ukiwa ndani ya tunduru tu

Hii bima ni nzuri kwa mtu yoyote mwenye familia na asiye na familia kwani maradhi hayanaga odi


Kujua kama Huduma hii ipo mkoani kwako au wilayani kwako tembelea kituo cha afya kilicho karibu nawe

Kuhusu bima hii mtu akiwa nayo anatibiwa magojwa yepi na yepi kiukweli bado sijajua kwaiyo itakuwa vizuri mtu anayejua aelezee zaidi
 
Kwa walio maeneo ya mwenge.ofis zipo jengo linalotazamana na majembe Auction.
Kwa wasio waajiri kujaza form na kujiunga wewe N family ya watu wanne.(mke.mume.na watoto 2 ni 1.5 million
Mwenye jibu la uhakika tafadhali kuna mtu pia kaniomba nimuulizie hili swala.
 
Back
Top Bottom