Jinsi ya kuja kusoma ulaya(Germany+France and some Scandinavian)

Mkuu edwayne endelea kufunguka basi mkuu vp hakuna namna ya kuingia Germany sio kwa kusoma ila ukifika ndo tufanye michongo ya kuapply?

Sent using Jamii Forums mobile app
hapo uje kama kimbizi au kuna program inatitwa aupair unakbaby sit watoto for a year i think then after that unaweza endelea na shule au mishe zako nyingine
 
Mkuu kwa wale waliosoma diploma na matokeo ya form four yako vizuri, gpa ya 4 kuna namna ya kusoma bachelor huko?
 
Baada ya watu Jana kuniomba niwaelezee jinsi ya kupata nafasi kusoma ulaya.
Kwa ujumla nchi nyingi ulaya hazilipishi ada kwa wanafunzi(ufaransa +Germany+ Finland+Norway{not sure}[Belgium ipo ila sio kubwa]).

Tuanze na Germany
Germany ina high education institution zipatazo 400(15 tu ndo Private) na ulaya kwa ujumla vyuo vinavyoheshimika na public kusoma private ni kujisababishia kukosa kazi hamna MTU anayeviamini. Vyuo vyote ujerumani unaweza kujiunga summer semester (april-july) au winter semester (October-feb). Ndio hamna ada ila utalipia kiwango kidogo kwa semester ambayo inategemea na chuo na chuo ambayo huu mchango ni ticket yako ya semester nzima na student government serikali haichukui chochote kazi yake ni kusomesha watu from kindergarten to PhD.

Bachelor kuna small range ya English program ila kwa masters English courses ni nyingi sana utachoka wewe kuapply.

Gharama kubwa ya ujeramani ni malazi na health insurance baada ya hapo maisha yanaenda na kuna chance ya kufanya kazi ... Kuhusu kazi ukiwa miji mikubwa utachoka wewe kuapply na kukataa kazi maana utaitwa sehemu nyingi.. Hakuna sehemu Ina kazi kama Germany.
Itaendelea sijatulia sana kwa sasa unaweza acha maswali nitaedit hii thread kujibu hayo maswali.

Pia ntaelezea jinsi ya kusoma France ila Finland sina uzoefu nao sana.
Guten tag
================================================================================================UPDATE:
Fees structure: in Germany kuna semester contribution ambayo unalipa kila semester kulingana na chuo From 72€-500€ hii inainclude usafiri na nyingine inaenda kwa student government .
Admission inatofautiana kulingana chuo na chuo ila for masters ni bora uwe na second upper class, coz their grading system ipo tofauti na ya bongo. Then unatakiwa kuangalia chuo chako kama kipo kwenye list ya vyuo vinavyotambulika dunia chuo chako kinatakiwa kiwe ranked H+ in following website Zentralstelle für ausländisches Bildungswesen ).
Then kuna english proficiency test unatakiwa upate from 5 to 9 for ILETS(it depends on chuo ila kuwa safe side unatakiwa upate 6+,pia kama una other english test unaweza attach sema mimi najua hiyo ILETS ndo niliyoifanya.NB: kama degree yako umesoma in english unaweza kuwa exempted)
Kozi: zipo kozi nyingi sana kwa kingereza just ingia hii link utaweza kuchagua unayotaka (International Programmes - DAAD - Deutscher Akademischer Austauschdienst). Nakushauri tumia PC au tablet kupata better version ya hiyo site. Zipo kuanzia bachelro mpaka PHD though Masters na PhD ndo nyingi za english
muda wa kuaaply: application for summer semster(April-july) ni kuaniza mid-october to 15 jan it depends na chuo. For winter(may-july). Unaweza apply online kupitia website ya chuo or central application system kwa ujerumani nzima[ Start ] utalipia hii then after application unadownload document unaadd your supporting document unatuma chuoni au hapo uni-assist kwa posta I suggest use EMS.
Kuhusu scholarship: hakuna scholarship nyingi kwasababu ni free education ila unaweza jisupport kupitia student job ukiwa mii mikuu hutokosa. Lakini kupenda scholarship ni ujinga tuu mtu mwenye nguvu anatakiwa apambani aendeshe maisha yake though for phd nahisi ni automatic scholarship unalipwa na serikali maana ni kama public servant cause your trying to find a solution to an existing problem.
Kama unamaswali zaidi yaweke ntayajibu nikipata muda ntaongezea na kuhusu ufaransa. Pia maisha kwa ujumla ya ujerumani.
Ndoto yangu kubwa Ni kuja kusoma nje ya nchi baada ya kumaliza shahada.vipi gharama zinaweza kua kubwa kiasi gani Kama utakosa scholarship? I mean usafiri wa kurudi Tanzania wakati wa likizo na vitu vinginevyo
 
Mzee baba kuna kitu hapo umekisahau ambapo wabongo wengi tumeona kusoma German ni simple Ila kitu kitu inaitwa

Blocked account
Yan ww ambae ni international students ambaye non-EU lazima udiposit euro 14200 kwenye blocked account ambayo branch ya hiyo bank ipo German then ndio upate visa

Na utaruhusiwa kuchukuwa euro 720 tu kwa mwezi kwa ijili ya matumizi

Sasa basi euro 14200×2578= ?
Hapo ndio utajamba cheche
 
Back
Top Bottom