Jinsi ya kuja kusoma ulaya(Germany+France and some Scandinavian)

edwayne

JF-Expert Member
Apr 5, 2013
5,649
2,000
Baada ya watu Jana kuniomba niwaelezee jinsi ya kupata nafasi kusoma ulaya.
Kwa ujumla nchi nyingi ulaya hazilipishi ada kwa wanafunzi(ufaransa +Germany+ Finland+Norway{not sure}[Belgium ipo ila sio kubwa]).

Tuanze na Germany
Germany ina high education institution zipatazo 400(15 tu ndo Private) na ulaya kwa ujumla vyuo vinavyoheshimika na public kusoma private ni kujisababishia kukosa kazi hamna MTU anayeviamini. Vyuo vyote ujerumani unaweza kujiunga summer semester (april-july) au winter semester (October-feb). Ndio hamna ada ila utalipia kiwango kidogo kwa semester ambayo inategemea na chuo na chuo ambayo huu mchango ni ticket yako ya semester nzima na student government serikali haichukui chochote kazi yake ni kusomesha watu from kindergarten to PhD.

Bachelor kuna small range ya English program ila kwa masters English courses ni nyingi sana utachoka wewe kuapply.

Gharama kubwa ya ujeramani ni malazi na health insurance baada ya hapo maisha yanaenda na kuna chance ya kufanya kazi ... Kuhusu kazi ukiwa miji mikubwa utachoka wewe kuapply na kukataa kazi maana utaitwa sehemu nyingi.. Hakuna sehemu Ina kazi kama Germany.
Itaendelea sijatulia sana kwa sasa unaweza acha maswali nitaedit hii thread kujibu hayo maswali.

Pia ntaelezea jinsi ya kusoma France ila Finland sina uzoefu nao sana.
Guten tag
================================================================================================UPDATE:
Fees structure: in Germany kuna semester contribution ambayo unalipa kila semester kulingana na chuo From 72€-500€ hii inainclude usafiri na nyingine inaenda kwa student government .
Admission inatofautiana kulingana chuo na chuo ila for masters ni bora uwe na second upper class, coz their grading system ipo tofauti na ya bongo. Then unatakiwa kuangalia chuo chako kama kipo kwenye list ya vyuo vinavyotambulika dunia chuo chako kinatakiwa kiwe ranked H+ in following website🙁 Zentralstelle für ausländisches Bildungswesen ).
Then kuna english proficiency test unatakiwa upate from 5 to 9 for ILETS(it depends on chuo ila kuwa safe side unatakiwa upate 6+,pia kama una other english test unaweza attach sema mimi najua hiyo ILETS ndo niliyoifanya.NB: kama degree yako umesoma in english unaweza kuwa exempted)
Kozi: zipo kozi nyingi sana kwa kingereza just ingia hii link utaweza kuchagua unayotaka (International Programmes - DAAD - Deutscher Akademischer Austauschdienst). Nakushauri tumia PC au tablet kupata better version ya hiyo site. Zipo kuanzia bachelro mpaka PHD though Masters na PhD ndo nyingi za english
muda wa kuaaply: application for summer semster(April-july) ni kuaniza mid-october to 15 jan it depends na chuo. For winter(may-july). Unaweza apply online kupitia website ya chuo or central application system kwa ujerumani nzima[ Start ] utalipia hii then after application unadownload document unaadd your supporting document unatuma chuoni au hapo uni-assist kwa posta I suggest use EMS.
Kuhusu scholarship: hakuna scholarship nyingi kwasababu ni free education ila unaweza jisupport kupitia student job ukiwa mii mikuu hutokosa. Lakini kupenda scholarship ni ujinga tuu mtu mwenye nguvu anatakiwa apambani aendeshe maisha yake though for phd nahisi ni automatic scholarship unalipwa na serikali maana ni kama public servant cause your trying to find a solution to an existing problem.
Kama unamaswali zaidi yaweke ntayajibu nikipata muda ntaongezea na kuhusu ufaransa. Pia maisha kwa ujumla ya ujerumani.
 

Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
33,236
2,000
Ukihariri uzi wako itakuwa vyema kiongozi haya mambo yakiwepo.

1. Fees structure ya vyuo vilivyo vingi.

2. Vigezo wanavyoangalia kwenye Admission [kama mitihani ya lughan.k]

3. Vibali vya serikali husika. [Visa]

4. Kozi

5. Wakati mzuri wa kufanya Maombi.
 

Kaisari

JF-Expert Member
Nov 13, 2012
3,645
2,000
Unaweza kunipatia mwongozo namna ya kusoma u dakitari wa binadamu,.
Chuo kizuri,. Ada yake,. Jinsi ya kuomba na kupata nafasi. Na gharama zake
 

edwayne

JF-Expert Member
Apr 5, 2013
5,649
2,000
Unaweza kunipatia mwongozo namna ya kusoma u dakitari wa binadamu,.
Chuo kizuri,. Ada yake,. Jinsi ya kuomba na kupata nafasi. Na gharama zake
Ada ni free ila nahisi udaktari Germany na ufaransa ni complicated sana najua kuhusu France.. Kwenda kusoma udaktari ipo hivyi
Mfano wale watu wote waliopata one advance national exam wanapiga pepa lengine la kitabe watakaofaulu vizuri ndo wanapelekwa kusoma udaktari na hapo serikali ina kulipa kama mfanya kazi Wa uma.
 

kamarah

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
839
1,000
Ada ni free ila nahisi udaktari Germany na ufaransa ni complicated sana najua kuhusu France.. Kwenda kusoma udaktari ipo hivyi
Mfano wale watu wote waliopata one advance national exam wanapiga pepa lengine la kitabe watakaofaulu vizuri ndo wanapelekwa kusoma udaktari na hapo serikali ina kulipa kama mfanya kazi Wa uma.
Daaah hongera zao, yaani unalipwa mshahara huku unapiga kitabu
 

vutakamba

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
201
250
Ada ni free ila nahisi udaktari Germany na ufaransa ni complicated sana najua kuhusu France.. Kwenda kusoma udaktari ipo hivyi
Mfano wale watu wote waliopata one advance national exam wanapiga pepa lengine la kitabe watakaofaulu vizuri ndo wanapelekwa kusoma udaktari na hapo serikali ina kulipa kama mfanya kazi Wa uma.
Nimefurahi sana kwa moyo wako wa kizalendo ktk kuwaelimisha na kuwasaidia watanzania ktk dunia ya leo wapo wachache wa aina yako. Nina kijana wangu anataka kuchukua Phd in anthropology and cultural tourism au social science. Hasa Germany. Hebu nipe darasa kidogo ndugu yangu.
 

Melkiard Junior

Senior Member
Aug 12, 2018
150
225
Mtoa Mada ukirudi utudadavulie vizuri basi kwa hizo nchi ambazo una uelewa nazo. na pia utusaidie, je; pamoja na kuwa fee free je haiwezekani kupata kind of ufadhili kwa ajili ya maladhi na chakula pia?
Thanx
 

Mzaleee

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
1,190
2,000
Mkuu vp naweza kuja kusoma halafu nikapata kibarua chochote tofauti na mambo ya kitaalumu nikafanya kwa mda was ziada na vipi ubaguzi??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom