Jinsi ya kuhesabu m-cycle kwa couple | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya kuhesabu m-cycle kwa couple

Discussion in 'JF Doctor' started by KAPECHA, Jul 9, 2009.

 1. K

  KAPECHA Member

  #1
  Jul 9, 2009
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HI ALL,

  Sisi wakatoliki kabla ya kwenda kanisani huwa tunapewa angalau kwa ufupi semina ya siku mbili na baada ya hapo huwa tunashauriwa kuhudhuria semina zozote zile zinazo endesha kuhusu familia.

  Suala la kujuana kimwili ni moja ya mada kuu ambayo huwa wanapewa wanandoa watalajiwa. kwa leo nitaanza na kuelezea m -cycle.

  wanawake wanatofautiana na sana kwa m-cycle na wako kama ifuatavyo

  1:16 days abnormal
  2:18 days abnormal
  3: 21 day cycle abnormal

  4: 28 day cycle which is normal

  5:30 days cycle which is normal

  6: 32 days cycle which is normal

  7: 33 , 35, 40 or more this is abnormal


  How to calculate 16 day m -cycle

  mfano: umeanza kubleed leo tarehe 9 / 7/2009 kwa hiyo chukua daftari na andika na hesabu moja. hesabu kuanzia hapo mpaka utakapo fika 16 na ujua siku ya kumi na sita itaangukia tarehe ngapi? utakuja kuona siku ya 16 inaangukia tarehe 24/7/2009 hivyo your next bleed should start 25/7/2009. hivyo hivyo utaanza kuhesabu kutoka tarehe 25/7/2009 mpaka kumi na sita na utakuja kungundua kuwa siku ya kumi na sita itakuwa ni tarehe 9/8/2009. hivyo inatakiwa uanze kubleed tarehe 10/8/2009. hivyo utakuwa unahesabu vivyo kila mwezi.

  Hivyo basi wanawake wanaobleed within 18 days and below huwa wana matatizo hivyo wanatakiwa waende kumuona daktari kwani kitaalamu sio sahihi. hivyo ikitokea mke wako anableed for 18 DAYS CYCLE MPELEKE hospitali akapate ushari.

  Angalisho: kuna wanawake wanaokuwa na cycle ya 24 or 26 days
  [U]
  WANAWAKE WANAOBLEED 28 DAYS HOW TO CALCULATE SAFE DATE AND SIKU ZA MIMBA AS OTHERS SAID BEFORE[/U]


  MFANO
  UMEANZA KUBLEED LEO TAHERE 9/7/2009 NA UNA MZUNGUKO WA SIKU 28


  9, 10,11,12,13,14,15,16,17,18,19,20,21,22,23,24,25,26,27,28,29,30,31/JULY
  1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23

  1, 2, 3, 4, 5/AUGUST
  24 25 26 27 28

  HIVYO THE NEXT BLEED WILL BE TAREHE 6/AUGUST 2009
  RED MEANS SIKU ZA HATARI

  HIVYO BASI SIKU SALAMA NI BAADA YA DAMU KUKATA UNAWEZA KUANZA KUMTUMIA MAMA LAKINI IKIFIKA SIKU YA KUMI NA TATU YAI KUWA LIKO YATARI NA HUANZA KUSHUKA. KIPINDI HIKI MAMA HUTOKWA NA UTE MZITO WA KUNATA AMBAO HUWA NI DAWA KWA AJILI YA KULINDA NA KUTENGENEZA MJI WA MIMBA KUWA TAYARI KUPOKEA MBEGU ZA KIUME KWA AJIRI YA URUTUBISHO .HIVYO MBEGU ZA BABA HUWEZA HUSAFIRI KWA URAHISI ZAIDI KATIKA MAJI MAJI HAYA.

  WANAWAKE WENYE SIKU 30 CYCLE

  ASSUME AMEANZA LEO TAREHE 9/7/2009

  9,10.11.12.13,14,15,16,17,18,19,20,21,22,23,24,25,26,27,28,29,30,31/JULY
  1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23

  1, 2, 3, 4, 5, 6, 7 /AUGUST
  24 25 26 27 28 29 30

  HIVYO THE NEXT BLEED ITAKUWA TAREHE 8/8/2009

  ANGALIA TOFAUTI KATI YA MTU ANAYEBLEED KWA SIKU 28 NA 30. MY LOGIC IS YAI HUCHUKUA SIKU KUMI NA NNE KUHARIBIKA BAADA YA KUKOSA KIRUTUBISHO. HIVYO HATA MWANAMKE AWE ANA CYCLE YA 16,18,20,24,26,28.30.32.34 OR 40 OR MORE. ITACHUKUA SIKU KUMI NA NNE ILI YAI LAKE LIWEKE KUHARIBIKA. NA SIKU YA KUMI NA TANO NDIO HUWA SIKU YA KWANZA KUANZA KUBLEED YAANI YAI LIMEKOSA KIRUTUBISHO.

  VIVYO ANZA KUHESABU KUANZIA SIKU YA TAREHE 28 KURUDI NYUMA UTAKUTA KUWA SIKU YA KUMI NA NNE NI TAREHE 23. HIVYO SIKU YA HARATARI ITAKUWA TAREHE 22 LAKINI KWA KUWA YAI HUCHUKUA SAA 72 WAKATI LIKISUBIRI KIRUTUBISHO NDIO MAANA TUNAANZA NA SIKU YA 13 , 14, 15 TOKEA PALE ULIPOBLEED.

  NA KWA MWANAMAMA ANAYECHUKUA SIKU 30 UKIHESABU KUANZIA 30 KURUDI NYUMA UTAGUNDUA KUWA SIKU YA 14 NI TAREHE 25/7

  HIVYO SIKU YA HATARI NI TAREHE 24/7 NA KWA SABAU YAI HUKAA SIKU TATU HIVYO TAREHE 23,24, NA 25/7 /2009 AMBAZO NI SAWA NA SIKU YA 16, 17, NA 17 KATIKA KUHESABU CYCLE

  YULE WA SIKU THELATHINI NA MBILI ITAKIWA SIKU YA HATARI NI YA 18 NA SIKU ZAKE TATU ZA HATATI NI 17, 18 NA 19 AMBAZO TAREHE 25,26,27/JULY KAMA SIKU ZAKE ZA HATARI

  NATUMAI NIMEELEWEKA KWA SISI WAKATOLIKI HATURUHUSIWI KUTUMIA KONDOMU WALA KUMWAGA MBEGU NJE KUFANYA HIVYO NI SAWA NA KUFANYA DHAMBI NYINGINE. HIVYO KWETU SISI WANANDOA KALENDA NI MUHIMU SANA NA TUNASEMA KUWA TENDO LA NDOA NI TAKATIFU SANA HIVYO KUNA WAKATI UNATAKIWA KUJINYIMA ILI UWE MTAKATIFU ZAIDI. HASA SIKU ZA HATARI. ILI KUEPUSHA MIMBA.

  ASANTENI
   
 2. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu hongera sana kwa kufuatilia semina kwa umakini mkubwa ingawa kuna mapungufu mengi yaliyomo kwenye mafunzo uliyo yapata na kwa mtu atakeyefuata mafunzo yako uwezekano wa kupata ujauzito ni 80%.

  Ningependa kukusahihisha katika mambo yafuatayo:
  Njia mnayotumia Ninyi wakatoliki Inaitwa Rhythm method of contraception au Billing Ovulatory Method (BOM) na wala sio hiyo uliyo ielezea wewe.
  Vitu vinavyozingatiwa kwenye hiyo njia ni Mzunguko wa mwanamke (Calender Rythm),Ute unaotoka ukeni ( mucus rythm) na Joto la mwili (temperature rythm). Nadhani mwalimu wako ali overlook hizo rythm mbili ambazo ni muhimu sana kupredict ovulation ya mwanamke.

  Kitu kingine ambacho hakipo sawa ni pale uliposema kwamba yai la mwanamke huishi kwa masaa 72. Ukweli ni kwamba ni masaa 12 hadi 24 tu.
  Lakini pia katika darasa ulilo tupa umesahau kumwangalia pia mwanaume Kwa sababu mbegu ya kiume inauwezo wa kuishi masaa 72 kwa maana hiyo basi kuweka siku za hatari kwa tatu tu kwenye mzunguko ni kumwatararisha mama na mimba zisizo tarajiwa.

  Kwa watu wanaotumia njia hii 20% ( failure rate of 20%) kwa sababu kuna watu ambao wanapata zaidi ya ovulation moja kwenye mzunguko mmoja,mama anaye nyonyesha, Kuna wengine pia mizunguko yao hubadilika kutokana na sababu mbali mbali kama chakula, kubadilisha mazingira, stress nk kwa hiyo ndugu yangu ni vizuri kuwa makini sana unapo tumia hii njia na uwe tayari kwa malezi yasiyotarajiwa.
   
 3. K

  KAPECHA Member

  #3
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa mganga

  how many days does egg take from ovary to uterus.

  Three days of which iam talking is inclusive of from ovary via fallopian tube to the uterus. As you are aware that sperm ya kiume inaweza kutoka kwa haraka sana na huwa haiwezi kusafiri umbali mrefu hivyo inaweza kufa njiani. Hivyo kama yai bado lipo kwenye fallopian tube mbegu hii itabidi ilisubili yai lishuke ndio ipate kufertilize kama itakuwa na nguvu inaweza kwenda kumate kwenye fallopian tube na kusababisha mimba nnje ya kizazi.
   
 4. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa kawaida mimba hutungwa kwenye mirija wakati yai linakuwa kwenye ampula na safari ya yai kutoka kwenye mirija hadi kwenye kizazi ni siku nne. kwenye kizazi ni implanatation tu hufanyika utungisho (fertilization) huwa tayari umeshafanyika kwenye mirija. Sababu za mimba ku implant nje ya kizazi (ectopic pregnancy) siyo sababu ya spidi kubwa ya sperm.
  Kuna sababu nyingi sana lakini kubwa kuliko zote ni matatizo ya mirija ya kupitishia egg(ovum), kama kutakuwa na blockage ya aina yoyote au mortility ya cillia ambazo ziko ndani ya mirija itakuwa siyo nzuri. Implantaion itatokea nje ya kizazi. Kwa sababu by 6th day implantation hufanyika bila kujali ile zygote itakuwa wapi.
  Tukirudi kwenye mada Mh. Kapecha naomba uzingatie marekebisho ya awali hapo juu ili kubaoresha ufanisi. Pia uzingatie failure rate ya Rythm method na kwamba haiko 100% perfect.
  Asante
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  nimewapata wakuu!
   
 6. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nashukuru kwa mtalaam aliyetoa mada hii na wote waliochangia. Swali langu je,
  1. utajuaje kama yai limeshanyakuliwa kwenye mirija (Fallopian tube)?
  2. Mwanamke ataonesha dalili gani?
  3. Ute mwepesi na mzito unaashilia nini?
   
 7. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Dalili za ovulation ( kunyakuliwa kwa yai) ni nyingi ambazo ni pamoja na:
  maumivu ya upande mmoja wa nyonga( one sided mid circle pelvic pain) hii pia huashiria ni ovary ya upande gani ambapo yai hutokea. joto la mwili huongezeka, some emotional changes wengine hupata furaha sana euphoria na wengine huwa wakali (hasira) sana kipindi hiki na kwahiyo wengine ashki ya kufanya tendo la ndoa huwa juu ingawa kwa baadhi wachache huwa chini.
  Hutoa ute mwingi laini, Ambao husaidia kusafirisha mbegu pia hurahisisha mbegu kupenya kwa urahisi kwenye mlango wa uzazi (cervix). na kwa baadhi ya wanawake hupata maumivu kidogo kwenye matiti.
  nadhani nimejaribu kujibu swali lako naomba na wataalamu wetu wachangie
   
 8. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Dah! Kwa ufafanuzi huo, ninaamini itasaidia wanawake wengi kuelewa mambo hayo.
   
 9. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Asante sana Mganga wa Jadi aka kalumanzila

  Ili Mbegu za kiume ziwe na uwezo wa Kurutubisha zinatakiwa ziwe na Sifa ipi, namaanisha mwanaume unatakiwa usikutane na mkeo kwa kipindi kama una mpango wa kumpa mimba au unatakiwa Ufululize

  Asante
   
 10. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #10
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Asante kwa elimu hiyo lakini nina maswali .

  1.Je naweza kuamua nipate mtoto gani kwa kutumia tarehe hizo za hatari,kama ni wa kike au wa kiume?

  2.Naweza kutumia utaalamu huo wa kuhesabu tarehe niweze kupata watoto mapacha?
   
 11. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #11
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Swali lako la pili ningependa hata mm nijue kwa kweli.
   
 12. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #12
  Aug 28, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  lalia mkono wa kushoto wakati wa tendo utapata jike,lalia mkono wa kulia utapata dume,kunywa cactus tree juice about the time of ovulation,chances ni kwamba utapata franternal twins
   
 13. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #13
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hayo unayosema umeshayafanyia practical? au biology ya wapi hii?
   
 14. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Aisee! hiyo kali... Je utafiti huo umeshaufanyia kazi na kupata matokeo?.
   
 15. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #15
  Aug 28, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  america ya kati,hasa mexico utumia njia hizi
   
 16. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #16
  Aug 28, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  hii ya kupata dume au jike imeandikwa ktk kitabu kiitwacho 'KAMASUTRA'
   
 17. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #17
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ss ufafanuzi kidogo.
   
 18. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #18
  Apr 13, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  wadau nataka nijue wakati muafaka wa mzazi kufanya tendo la ndo, ni miezi mingapi ikipita tangu ajifungue?
   
 19. Inno laka

  Inno laka JF-Expert Member

  #19
  Dec 24, 2013
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 1,592
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  Kwan ukipiga kila siku mimba haiingii
   
 20. L

  LEOMWANA Member

  #20
  Aug 9, 2014
  Joined: Nov 26, 2013
  Messages: 26
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbegu za kiume zinakua hazijakomaa hivyo huwezi kurutubisha yai(no fertilization)
   
Loading...