Jinsi ya Kuhalalisha Viwanja vya Ndege vya Kimataifa Migodini - Fikra za Watawala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya Kuhalalisha Viwanja vya Ndege vya Kimataifa Migodini - Fikra za Watawala

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 6, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Yote tisa, hivi huu mtindo wa kampuni za madini kuwa na viwanja vya ndege ambapo wanaweza kusafirisha dhahabu moja kwa moja hadi nje ya nchi una manufaa gani kwa taifa? Hivi ni kweli hawa watu kutoka Geita wanashindwa kuruka hadi uwanja wa ndege wa Mwanza ambapo kuna Ushuru na Forodha? Maana hata Meremeta nao walikuwa na uwanja wa ndege vile vile hadi leo hatujua walisafirisha kiasi gani cha dhahabu kwenda Afrika ya Kusini; wameacha mashimo tu!!

  Lakini kuna namna ya kuhalalisha uwepo wa viwanja hivi vya ndege

  - kusafirisha wafanyakazi
  - Kusafirisha vitendea kazi mbalimbali
  - Kusafirisha vipuri

  Hata hivyo nimeshindwa kuelewa kama viwanda vingine navyo vinaweza kutumia sababu hizo hizo kuwa na viwanja vyao vya ndege. Nimejiuliza kwa mfano kwanini tusiweke utaratibu kuwa labda mahali ambapo wanaweza kuwa na uwanja wa ndege ni pale ambapo hapawezi kufikika kwa ndege kati ya saa moja hivi au kulazimisha viwanja hivyo vya ndege visiwe vya makampuni bali kampuni kama ya madini ijenge kiwanja cha ndege cha umma ambacho kitatumiwa na umma vile vile. Kwa mfano hicho cha Geita kisiwe cha kampuni bali chini ya TCAA (sijui kama kilivyo sasa kinamilikiwa na GGM au vipi).

  Sijui ni makampuni mangapi ya madini yana viwanja vyao vya ndege vya kimataifa nchini. Hili linahusu pia kampuni za uwindaji...
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  Nadhani vinatakiwa viwe chini ya TAA.......na isitoshe ni lazima wapitie kwenye viwanja ili wafanye ushuru na forodha...ambavyo viwanja hivyo ni Tabora, Dodoma,Mwanza, Kia, Dar na Zenj.....labda kuwe na utaratibu mpya......
   
 3. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Mwanakijiji, tunapozungumzia uwanja wa ndege katika lugha yetu ya kiswahili ni rahisi sana mtu kufikiria labda ni uwanja wa ndege kama wa Mwanza au JKIA. Tukiweka viwanja vya ndege katika makundi yake kama:

  1. International Airports (mfano KIA, JKIA, na Songwe)
  2. Airports (mfano Mwanza, Arusha, Musoma, n.k)
  3. Aerodromes
  4. Airstrips/Airfield

  Viwanja vilivyoko kwenye migodi ni aina ya kundi la 3 na 4 (Aerodromes na Airstrips), kwa naana kwamba ni runway tu yenye urefu wa 2km hivi inayowezesha ndege ya ukubwa fulani kutua. Mara nyingi kule migodini wanatumia ndege ndogo Cessna au DASH na viwanja ni vya aina ya airstrips au aerodrome.

  Kiutaratibu ndege inayosafirisha dhahabu kutoka migodini inatakiwa ipitie JKNIA (DAR) kwa ukaguzi ndipo iendelee na safari, lakini sishangai kwa jinsi serikali yetu inavyopenda kuwabeba wawekezi, kwamba ndege yenye dhahabu inaweza kuruka moja kwa moja kutoka Geita Mine na kuvuka mipaka ya nchi. Serikali watasema wana ofisa wa TRA pale mgodini kwa ajili ya kukagua, lakini hapo ujue hilo ni changa la macho tu, hakuna uhakiki unaofanyika na haruhusiwi hata kuiona au kuichungulia kuhakikisha kama vipande vilivyoorotheshwa kwenye makaratasi ndivyo vinasafirishwa.

  Wajinga ndio waliwao.
   
 4. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji,

  Big up kwa kuliona hili. Ukweli ni kwamba VIWANJA VYA NDEGE KWENYE MIGODI YA MADINI NI KUHALALISHA WIZI WA RASLIMALI zetu za madini; Dhahabu,Almasi,Tanzanite n.k.

  Haiingiii akilini Mwekezaji awe na kiwanja chake kwenye mgodi. Hili limefanywa maksudi ili hawa WAIZI wa madini yetu wapate loophole ya kuchukua madini yetu bila kuwa checked! Na ndiyo maana NCHI YETU INAZIDI KUBAKIA MASHIMO NA DHAHABU ZIKIENDELEA KWISHA. Nina uhakika katika miaka 50 mingine ijayo kwa wale watakaokuwepo HILI RI NCHI RITAKUWA NI MASKINI KULIKO LILIVYO SASA NA LITAKUWA LIMEBAKIZA MIJISHIMO TU!!

  HALI NI HIYO HIYO KWENYE MBUGA ZETU ZA WANYAMA. Kwa kasi iliyoko sasa ya kuhamsha wanyama hai kwenda nje kwa njia za udanganyifu,nachelea kusema kuwa katika miongo 2 au 3 ijayo mbuga za wanyama zitakuwa zimegeuzwa KUWA SEHEMU ZA KUCHUNGIA NG'OMBE WA WASUKUMA NA WAMASAI TU!

  Hii ni aibu. Tunahitaji UONGOZI MPYA HAPA TANZANIA ILI KUWEZA KUBADILISHA MWELEKEO WA TAIFA HILI LINALOENDA KUFILISIKA KATIKA SIKU CHACJE ZIJAZO.
   
 5. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Rejea thread yangu"Nasikia Malalamiko Kanda ya Ziwa"
  Mwanakijiji, Kwanza Kanda ya ziwa haina Uwanja wa ndege wa Kimataifa, kuna strip ya ndege za Jeshi na majengo yanayofanana na shule ya kata tu mkuu.
  Si jambo jipya kwa migodi yote TZ kuwa na viwanja vya ndege, hata hivyo kwani hufahamu ya kuwa hata ktk mbuga zetu za wanyama kuna viwanja vya ndege mkuu?

  There's no place like Tanzania
   
 6. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Kuna usemi..."ukiona manyoya......." ndo ivo tena
   
 7. d

  dotto JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  NA pia ya vigogo hupitia huko huko.
   
 8. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Nduguyangu ukisikia sarakasi za hihi serekali unaweza ukawa kichaa
   
 9. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Aaghhhh!!!! inaudhi sana kusikia ndege inabeba dhahabu kupeleka nje ya nchi tena chini ya Ulinzi wa majeshi yetu ya Tanzania.

  Chaaaa!!! Huzuni yangu na iwe juu yao wanaoasababisha haya!!
   
 10. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #10
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kweli safari bado ni ndefu .Changamoto uliyoitoa ina mashiko,Ila kwa kuwa tumekuwa wavivu wa kufikiri na viongozi wetu huwa wanajifikiria wao na familia zao kwanza,ni vigumu kuyafanyia kazi mawazo kama haya.
   
 11. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Naomba mungu anijalie uchawi niwaloge wote wanaohujumu uchumi wa nchi yangu niipendayo wakati hata wao hawafaidiki na utajiri huu wanaoupoteza wanachofaidi ni sifa za kijinga (mazingira mazuri ya uwekezaji) na kuendelea kuitia nchi katika umaskini wakati mungu ametujalia rasilimali za kutosha kuitwa super power kutokana na rasilimali.
   
 12. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ukifuatilia kwa kina mambo yanayoendelea bongo unaweza kuzimia hata ukimwagiwa maji kutaamka!!!!!!!!! Ni Bongo ambapo tuna viwanja wa ndege kwenye mbuga za wanyama, migodini, na hata wamiliki wa viwanda vya samaki pale mwanza hupeleka wale samaki Kenya kwa njia za magari kisha kusafirishwa nje! Nilifika mwenyewe Buhemba kujionea kile kilichoachwa na Meremereta ni huzuni milima na mashimo ya kutisha dhahabu imeenda watu wamebaki na ufukara wao. watu hata uwezo wa kununua kiatu cha yebo yebo hawana dhahabu yao imeenda!. Bongo mchawi wake alikufa siku nyingi.
   
 13. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #13
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Jamani basi mnanitia uchungu na kujiona mimi kama mtanganyika ni mjinga
   
 14. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  MMM.....
  Siamini kama umesahau kuwa wale wanyama wetu walipitia pale KIA!
  Ahsante kwa uangalizi makini lakini tatizo letu ni zaidi tu ya wapi viwanja vikae....
  Naamini wakati tunajadili haya tujiandae kwa tukio jingine kubwa zaidi tena litapigiwa hapa JKNIA
   
 15. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #15
  Jan 6, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji unafikiri hata kama wangesafirisha hayo madini kupitia viwanja vikubwa kama DAR and KIA wangeshindwa kuyaiba? Mbona wanyama walipitishwa live pale KIA na hakuna kilichofanyika? Chukulia kwa mfano biashara ya pembe za ndovu kati ya Tanzania, China na Mashariki ya Kati imeshamiri sana na wanasafirisha hizo pembe kupitia viwanja vya ndege vya kimataifa. Kama biashara haramu kama ya pembe za ndovu inaweza kufanyika kupitia international airports, biashara halali ya madini itashindikana kweli?

  Kuna allegations kwamba "Chinese embassy officials smuggle ivory out of [Tanzania] in diplomatic bags that don't get checked." Pia kuna allegations kuwa "when President Hu Jintao came on a state visit to Tanzania in February 2009, his officials left with up to 200 kilos of illegal, smuggled ivory." Hao wote walipitia viwanja vya ndege vya kimataifa. Kwa hiyo, linapokuja suala la madini, hata tukipiga marufuku aerodromes na airstrips kwenye sehemu za madini bado madini yatapitishwa kwenye international airports kiulaini.

  Unreported World - 4oD - Channel 4: The poaching of elephants in East Africa
   
 16. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,164
  Likes Received: 1,167
  Trophy Points: 280
  Tuna kila sababu za kuubadili uongozi hilo kila mtanzania antakiwa ilijuwe asieliju nijukumu langu na wewe kumfahamisha. kwa kutumia njia yoyote ile inayoweza kutufikisha kwenye lengo la ustawi halisi wa jamii ya mtanzania tutambue kuwa uongozi uliopo sasa hivi ndicho kikwazo cha ustawi wetu haiwezekani yale tunayo yaona kama makosa tunao waita viongozi wanaona ni mafanikio. Tumelia na mikataba mibovu lakini wao wanazidi kuwabinafsishia migodi mipya tena watu walewale kwa makubaliano yaleyale ambao jana tuliwalalamikia kuwa wanatupunja!, :hatari::hatari::hatari:
   
 17. M

  Moses msisia Member

  #17
  Jan 6, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  basi nimeishiwa nguvu nalala.
   
Loading...