Jinsi ya kufikisha kuku 1000 wa asili ndani ya muda mfupi

Problem is wafugaji wengi sio wafuatiliaji kuna njia nyingi za kupunguza gharama za uzalishaji
Mfano kuzalisha vunza njia ya asili kama chanjo cha protein kuna matokeo chanya .
Kutumia biogas kama unafuga na ngmbe. hapo unaweza kupungza gharama za umeme .
Kutengeneza incubator za asili .
Kutumia dawa za asili kama njia ya kuzuia na kujikinga na magonjwa ya kuku .
Kutumia mifumo kama nusu huria utapunguza gharama za chakula pia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa.
Kutengeneza chakula chako mwenyew n.k
Hiya mambo yanaketa tija kwenye ufugaji wa kuku wa asili.
Mkuu zungumzia kuhusu chakula zaidi. Maana hao ni kuku wa kiasili. Kwamba watalishwaje na bajeti ikoje. Maana chakula ni asilimia 70 ya gharama za uendeshaji. Unapokuwa na kuku 1000 wa kiasili unawalishaje na uendeshe vipi huo mradi. Asante.
 
sokoni kuna dawa, chanjo feki ambazo hazina ubora, madactari wa mifugo wamekaa kipesa zaidi. mfugaji jitahidi uongeze maarifa juu ya lishe na matibabu ya mifugo yako, kuwa na dactari mwenye uadilifu na kazi yake. tumekuwa tukilia kuna mwagonjwa mengi na mengine hayatibiki kwa sababu mamlaka za kudhibiti ubora wa madawa zimelala
 
Mm nimeanza kufuga hivi karibuni lakin kuna kitu nimejifunza. Kuhusu haya maneno ya ndugu.
Kuku hawa 1000 ni jambo rahisi kuwafikisha ukiwa na tetea 20 ila usiwe na hela za mawazo sana , na uwe mfuatiliaji mzuri na uwe na banda Nzuri la juu .
Kwa ushauri wangu ukipata mayai totolesha kwa mashine, Lea vifaranga weeks 4 walishe starter na wake dawa zote.
Kulea vifaranga hakikisha usafi angalau kila siku ubadilishe magazeti kwa weeks 2 za kwanza. Wake maji masafi kama unayokunywa. Wawekee chanzk chanzo cha joto vifaranga vitakua vizuri, na uwalinde na mbuu.
Ukiwa na kuku 20 unaweza kupata tray 5-6 kwa mwezi na ukitotolesha unaweza kupata on average 150 kwa mwezi. Kingine usipende kuingiza kuku wapya kwenye banda lako wanaweza kuja na magonjwa. Banda Lowe juu lisiguse chini kuzuwia wadudu na unyevunyevu
 
Hongereni wafugaji

Kama unahitaji kuagiza incubator from abroad tuwasiliane

Ufugaji unalipa
 
Mkuu mayai yakikaa sana percentage za kutotolewa huwa chini ya 40%...yai lisikae chini ya siku 7 ..zamani nilikua nabisha...sasa hv nakisanya mayai kwa siku 5 napeleka incubator..yanatoka zaidi ya 98%..ukiyaweka kwa 14 yanatoka 80% chunguza hilo...! Sio rahisi kama ulivyoandika...unaweza wapa chanjo zote lakini unakuta vifo bado vinatokea....changamoto iko hapo
Naomba kujua uzoefu wako kwenye matumizi ya incubator. Hasa kama ni home made au toka nje,utumiaji wa nishati, n.k.
Nataka siku zijazo nitafute incubator ya mayai machache kwa matumizi yangu.
Hawa wauza vifaranga wataniua.
 
Mkuu incubator ya mayai 2000-2500 shilling ngapi, iwe automatic
Hiyo Mayai 4000 bei 1,850,000/=

1621087121183.png
 
Naomba kujua uzoefu wako kwenye matumizi ya incubator. Hasa kama ni home made au toka nje,utumiaji wa nishati, n.k.
Nataka siku zijazo nitafute incubator ya mayai machache kwa matumizi yangu.
Hawa wauza vifaranga wataniua.
Mie sina incubator mkuu..ila kuna jirani anayo ndo nampelekea anatotolesha
 
Njia nyepesi ya kupata kuku 1,000 kwa muda mfupi saana ni kukusanya mayai ya pure kienyeji - lets say tray 50 ambayo kila tray ina mayai 30 - Jumla mayai 1500 - Kila tray ya kienyeji ni Tshs 10,000 mikoani Plus usafirishaji pamoja na packaging fanya 20,000. Jumla ya Pesa yote 1,000,000/=

Mayai yatotoreshe kwenye Incubator with average ya 70% both Hatching & fertility
Kutotoresha tray 1 = 10,000 tray 50 = 500,000.

Baada ya siku 21 utapata vifaranga 70% times 1500 = 1050.

Utawatunza hawa kwa wiki 12, wiki nne za mwanzo ukiwapa chanjo za Gombolo na Newcastle na wiki ya 5 ukichanja ndui.

Chakula na matunzo yao kwa wiki hizo 12 ni 1.5m (Chanjo & Chakula)

Wiki ya 13 - utawahamishia shambani kwako - Free range zone.... hapo utawapatia supporting food tu wakati wa jioni kama Pumba & Mashudu kidogo.

Baada ya wiki ya 20 wataanza kutetea na vijogoo vitaanza kuwika. Wiki ya 24 wataanza kutaga - baadhi ya majogoo utaanza kuuza kwa 20,000.

Hii ndiyo njia nyepesi kuliko ile ya mwanzo ila hii utahitaji kuwa na walau 5m ili uwe confortable - anayehitaji kufanya hii ani PM nitamuunganisha na jamaa.
 
Back
Top Bottom