Jinsi ya kufanikiwa na dunia ya kiuchumi kupitia mtandao.

Wakipekee

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
5,354
9,217
Habari zenu wadau ?? Bila shaka mu wazima kama una tatizo pole sana Mungu akufanyie wepesi urudi kwenye hali yako ya kawaida.

Nimekuwa nikifatilia sana kuhusu maswala ya kutengeneza fedha kupitia mtandao. Kulingana na ukuaji wa sayansi na tekinolojia na mimi nikaona nisibaki nyuma. Nikaanza kufatilia njia mbalimbali, kwa bahati nzuri humu JF kuna nyuzi nyingi nzuri sana ambazo zimefafanua vizuri hili swala lakini kuna mmoja ulinivutia sana. Huyu mtu alielezea sana njia nyingi ambazo ni hizi.

1• Freelencing

2• Dropshipping

3• Blogging

4 • Affiliate Marketing

5 • Paid survey

6 • Websites zinazolipa kwa kuangalia matangazo (Ads).

Nashukuru sana huyu kijana alielezea kila njia kwa kina kiasi ila nilitokea kuvutiwa na blogging.


Nikajipa kazi ya kufatilia blogging ni nini na anafanya kazi vipi na vipi unaweza kunufaika nayo. Naamini humu kuna wadau ambao walitangulia kujua haya maswala hivo nikaona nami niombe msaada. Hivo mambo ambayo ningepata kujua au kushauriwa ni haya.

1. Mimi kama mwanafunzi kabisa wa haya mambo ya blogg nifanye kitu gani kuanzisha blogg bora?

2. Je blogg za kiswahili nazo pia zinalipa? Maana niliwahi kusoma mahali hazitambuliki na malipo ya Google.

3. Nahitaji vifaa gani?


Karibuni sana wadau msaada wako ni muhimu ili kujenga nchi. Ahsanteni sana.
 
Back
Top Bottom