Habari wana JF
mwaka 2013 unaisha je umewahi kutathimini ni mambo mangapi umefanikiwa? mangapi umeshindwa? kwa nini?naomba niwashirikishe uzoefu wangu ktk maisha.
Jua hv hakuna jambo lolote linalotokea bila KUPANGA.kupanga ni kuamua unataka ufanye nini....na kama hujapanga ni vigumu kujua umefanikiwa au umeshindwa..kupanga kumenisaidia toka nikiwa olevel mpaka nikamaliza vyuo vikuu.na kufanikiwa ktk maisha yani Elimu,Kiuchumi,Familia nk.sasa narudi kwenye kiini cha uzi huu.tunapoingia mwaka 2014 fanya yafuatayo kama una lengo la kufanikiwa ktk maisha yako
1.PANGA
Hakikisha umepanga mambo ya kufanya hapa uwe na diary au note book ili uandike usije sahau kuna mipango ya mda mfupi hii inafanyika ndani ya mwaka na ya mda mrefu zaidi ya mwaka mfano kujenga kuoa nk
2.AMINI
Hakikisha unaamini kwamba utayafanikisha malengo yako kwa 100%
3.MUDA
Hakikisha unaweka mda wa kukamilisha malengo yango kumbuka wakati ni ukuta ukipita umepita haujirudii
4.TATHMINI(evaluation)
hakikisha unacheki mara kwa mara kama umefanya yale uliyopanga ainisha vikwazo kisha amua kuvikabili sio kuacha au kukubali kushindwa
5.USIKATE TAMAA
Hakikisha unazikabili changamoto sio kukimbia
kwa sababu utakuwa umejifunza makosa hivyo utakaporudia utafanya vizuri sana jua hata waliotengeneza ndege magari nk walikosea walirudia sana mpaka wakafanikiwa
Samahani ntarudi badaye