Jinsi Ya Kufahamu Uwekezaji Wa Ardhi/Majengo Ambayo Ni Hatarishi Mwaka 2022

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Sio kila kiwanja kinaweza kukutengezea fedha. Sio kila nyumba ya kupangisha inaweza kukutengezea kipato kikubwa na kipato endelevu kwa kila mwaka. Kwa sababu hii, unahitaji kufanya tathmini kabla ya kufanya uwekezaji kwenye ardhi/nyumba.
flyerdesign_04062022_154003.png

Kwenye somo hili nimekuandalia mambo ya msingi sana ya kuzingatia ili kumiliki ardhi/nyumba ambazo zina hatari ndogo za kiuwekezaji. Kwa kuzingatia mambo haya, utaweza kupunguza hatari za uwekezaji bila kupunguza jumla ya kipato cha uwekezaji wote.

Hatari (risk) ni moja ya kitu ambacho husahaulika sana kwenye uwekezaji wa majengo ya kupangisha. Faida za kuwekeza kwenye majengo ya kupangisha zinavutia sana, lakini hatari zake ni muhimu kuzingatiwa.

Mambo muhimu ya kuzingatia ni kama ifuatavyo;-

✓ Utakuwa mwenye hekima pale tu utachukua hatua za kutathmini hatari za uwekezaji kabla ya kuwekeza.

✓ Mtaji unatakiwa kuwekezwa tu kwenye uwekezaji ambao hatari zake unakubaliana nazo.

✓ Ni vyema kushughulikia hasara iliyopo kuliko kuendelea kusubiri kuanza kuingiza kipato chanya.

✓ Ikiwa ulitawanya uwekezaji wako inakuwa rahisi sana kuondokana na changamoto unazokutana nazo.

✓ Kila uwekezaji una faida na changamoto zake. Uwekezaji wenye faida kubwa unakuwa hatarishi zaidi ukilinganisha na uwekezaji ambao una faida kidogo. Mtaji wako unakuwa salama zaidi kwenye uwekezaji wenye faida kidogo ukilinganisha na uwekezaji wenye faida kubwa.

Ni rahisi kutathmini hatari za uwekezaji kwenye majengo ya kupangisha kuliko uwekezaji kwenye hisa.

Hatua 5 Za Kupima Hatari Za Uwekezaji.

Moja.

Udhibiti binafsi.

Mwekezaji ambaye hana muda kabisa wa kudhibiti uwekezaji wake atatakiwa kuwekeza kwenye akaunti za benki za kupata riba. Hapa atakuwa anapata kiasi kidogo sana cha faida.

Mwekezaji ambaye ana muda na uzoefu mkubwa wa kudhibiti uwekezaji wake atatakiwa kuwekeza kwenye uwekezaji hatari zaidi na wenye faida kubwa sana.

Kwenye uwekezaji hatari zaidi uwezekano wa kupoteza kila kitu ni mkubwa vilevile.

Kwenye ardhi na majengo, unaweza kulipia bima mtaji wako. Utahusika kutafuta wapangaji bora sana, utakuwa na uwezo wa kuongeza kiasi cha kodi pale inapotakiwa na utakuwa unachagua mtaa ambao unalipa kodi kubwa.

Mbili.

Hatari au faida za uwekezaji husika.

Unatakiwa kupima kiasi cha kodi endapo kitakuwa ni faida kubwa, faida ya kati au hasara. Pia, utatakiwa kupima hali ya mzunguko wa soko la ardhi na majengo kwenye eneo unalotaka kuwekeza.

Hii itakusaidia kuepuka kununua kipindi ambacho nyumba zinakaribia kushuka bei. Jambo lingine ni hali ya kupata mitaji fedha kutoka kwenye vyanzo mbalimbali hasa benki na kampuni za biashara na uwekezaji.

Hali nzuri ya utoaji wa mitaji fedha hupelekea uwekezaji wenye faida kubwa ukilinganisha na sehemu ambapo mitaji fedha hutolewa kwa masharti magumu kwa wawekezaji.

Tatu.

Kupata mikopo ya majengo (leverage), urahisi wa kuuza (liquidity) na kutawanya uwekezaji (diversification).

Haya ni mambo matatu (3) ya msingi sana kwenye upimaji wa hatari za kuwekeza kwenye majengo ya kupangisha.

Kutumia mikopo ya majengo ni moja ya hatari ambayo huukumba uwekezaji kwenye majengo ya kupangisha mara kwa mara.

Kwa wawekezaji wengi sana watahitaji mikopo ya majengo ya 70% hadi 80% kwa sababu hawana mitaji fedha ya kutosha.

Jinsi unavyoweza kupata kiasi kikubwa cha mkopo ndivyo uwekezaji wako unakuwa hatarishi zaidi na wakati huohuo ndivyo unakuwa kwenye nafasi kubwa sana ya kuingiza kiasi kikubwa cha faida kutokana na kodi ya nyumba.

Urahisi wa kuuza nyumba yako ni changamoto nyingine ambayo hupelekea uwekezaji kuwa hatari zaidi.

Unahitaji kutumia nyumba yako kuombea mkopo wa majengo kwa ajili ya kuongeza uwekezaji au kuuza nyumba yako kwa ya kununua nyumba nyingine au zingine zenye faida kubwa zaidi.

Hii ni suluhisho kwa uwekezaji ambao huwezi kupata pesa taslimu kwa urahisi kama ilivyo kwenye uwekezaji wa majengo ya kupangisha.

Ni vigumu sana kupata punguzo la kodi ya nyumba za kupangisha kutoka kwenye nyumba ambazo zipo nyingi kwenye viwanja tofauti tofauti. (Hii ni kwa nchi ya marekani, kwetu sisi hatuna punguzo la kodi serikalini kwenye nyumba za kupangisha).

Njia pekee ambayo mwekezaji anaweza kutawanya uwekezaji wake ni kuwekeza kwenye masoko tofauti tofauti; majengo ya kupangisha, hisa na vipande.

Mfano; mwekezaji ambaye ana mtaji wa milioni 100. Anaweza kuwekeza milioni 30 kwenye majengo ya kupangisha, 20 kwenye hisa na milioni 50 kwenye vipande.

Nne.

Upatikanaji wa mitaji fedha.

Kuna aina ya uwekezaji ambao huhitaji kiasi kidogo sana cha mtaji ili kuanza kuwekeza kama vile uwekezaji kwenye vipande (mfano; UTT-AMIS kwa hapa Tanzania).

Kwa uwekezaji wa majengo ya kupangisha, utahitaji kiasi kikubwa sana cha mtaji fedha ukilinganisha na vipande au hisa.

Pia, aina ya majengo inaweza kuwa ni kikwazo kuanza kuwekeza aina unayotaka kwa sababu ya kiasi kikubwa cha mtaji fedha unaohitajika.

Tano.

Kipato endelevu (cashflow planning).

Kutengeneza kipato endelevu ni jambo la mwisho la kukuongoza kupima hatari ya uwekezaji husika. Hakuna kipato endelevu (kipato cha kila mwezi au wiki) kwenye uwekezaji wa akaunti za kulipwa riba.

Ni muhimu kuzingatia kuwa kipato endelevu ambacho ni chanya ndicho ambacho hufaa zaidi kwa kumnasua mwekezaji kwenye janga la umaskini.

Mwekezaji ambaye anakubali kumiliki nyumba inayoingiza kipato endelevu ambacho ni hasi (kuingia hasara) anakuwa amewekeza kwenye uwekezaji hatarishi zaidi.

Muhimu; jiunge na kundi la UWEKEZAJI MAJENGO kupata masomo ya semina yanayoanza tarehe 13-06-2022. Nipigie kwa maelezo zaidi kupitia namba +255 752 413 711.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi wa ardhi na majengo.
 
Ahsante sana kwa Elimu. Tuko pamoja, nimesubscribe.
Nimefurahi sana kwa maamuzi yako ya kufuatilia maarifa haya mazuri.

Hongera sana rafiki yangu.

Namba yangu ya whatsapp; +255 752 413 711

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi wa ardhi na majengo.
 
Back
Top Bottom